Thursday, October 6, 2011

Taswira Za Ziara ya Rais Jakaya Kikwete Mkoani Morogoro

Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kumzawadia fedha, mtoto Liano Adamu (7) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ruaha Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro baada ya kuvutiwa na uchezaji wake wa ngoma ya Lizombe ya kabila la Wangoni. Rais yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Nyuma ya Rais ni Mkuu wa Mkoa, Joel Bendera.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mitambo ya kuzalisha umeme katika bwawa la Kidatu,mkoani Morogoro jana .Kushoto ni meneja wa TANESCO wa mkoa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu mafunzo ya uchunguzi na upelelezi kutoka jeshi la polisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa Baraza na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na washiriki wa mafunzo ya uchunguzi na upelelezi baada ya kuwa amefunga mafunzo hayo katika Chuo cha Polisi cha Kidatu, Mogororo,leo, Alhamisi, Okotoba 5, 2011. Pamoja na ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Joel N Bendera na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, Saidi Mwema. Wengine waliokaa ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili, Jaji (mst) Salome Kaganda na Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Jaji (mst) Damin Lubuva.Picha na Mdau John Nditi na Freddy Maro-IKULU


No comments: