Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Mhe. Eddison Lobao (kulia) October 5, 2011 kwenye Ofisi za wizara hiyo zilizoko Brasilia. Mhe Pinda Yuko katika ziara ya kikazi nchini humo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu picha ya wafugaji wa kabila la Wamasai aliyomzawadia Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Mhe. Eddison Lobao (kushoto) October 5, 2011 baada ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za wizara hiyo zilizoko Brasilia. Yuko katika ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Mary Nagu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Brazil Mhe. Jorge Alberto Portanova wakati alipowasili kwenye ofisi za Wizara hiyo zilizoko Brasilia kwa mazungumzo ya kiserikali akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Mhe. Eddison Lobao (kulia) October 5, 2011 kwenye Ofisi za wizara hiyo zilizoko Brasilia. Yuko katika ziara ya kikazi nchini humo. Picha na Hilary Bujiku wa PMO.
BRAZIL YAAHIDI KUSAIDIA KUTATUA KABISA TATIZO LA UMEME
BRAZIL imeahidi kuisaidia Tanzania kondokana moja kwa moja na shida ya umeme
kwa kutoa teknolojia na uwezo wake chini ya uhusiano na ushirikiano baina ya
nchi hizi mbili.
Ahadi hiyo ilitolewa jana Jumatano Okt. 5, 2011 na Waziri wa Madini na
Nishati wa Brazil, Bw. Edson Lobao katika mazungumzo rasmi ofisini kwake
mjini Brasilia, makao makuu ya Serikali ya Brazil, na Waziri Mkuu Mizengo
Pinda ambaye anaitembelea nchi hiyo.
Bw. Lobao alisema Brazil ina uzoefu mkubwa katika teknolojia ya kufua umeme
na akasema ataliagiza Shirika la Nishati ya Mafuta la Brazil, PETROBRAS,
kuangalia namna gani ya kushirikiana na Tanzania katika eneo hilo.
PETROBRAS, ambayo pia inashughulikia uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya
maji,tayari inatafuta mafuta na gesi nchini Tanzania kwenye pwani ya Mtwara.
Brazil tayari imeonyesha nia ya kuisaidia kiufundi Tanzania katika ujenzi wa
kinu kikubwa cha kufua umeme kwa nguvu ya maji kwenye eneo la Stegler’s
Gorge, kwenye mto Rufiji.
Jana hiyo hiyo, Waziri Mkuu Pinda pia alikuwa na mazungumzo na Waziri wa
Kilimo na Mifugo wa Brazil, Bw. Jorge Alberto Portanova Mendes Ribeiro Filho
na Waziri wa Maendeleo Vijijini, Afonso Florence.
Leo Alhamisi Okt. 6 atatembelea kituo cha Utafiti wa Kilimo cha EMBRAPA
na kesho Ijumaa Okt. 7 atatembelea mji mwingine mkubwa wa Brazil , Rio de
Janeiro.
Tayari alikwishatembelea Sao Paulo ambako, pamoja na mambo mengine
alitembelea Makao Makuu ya Kampuni ya ABIMAQ inayotengeneza zana za Kilimo
na kiwanda cha sukari cha Costa Pinto ambacho pia hutengeneza kutokana na
miwa kemikali ya *Ethanol* inayotumika kwa nishati.
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment