Sunday, July 17, 2011

*MICHAEL NA REHEMA WAMEREMETA, MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, SPIKA ANNE MAKINDA WAHUDHURIA SHEREHE YA NDOA YAO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwapongeza maharusi, Michael Deo Sanga na Rehema, wakati wa sherehe yao ya harusi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam jana jioni. Maharusi wote ni Wakinga kutoka mkoani Iringa, Michael ni mtoto wa Mbunge wa Njombe Kaskazini, Mkoa wa Iringa, Deo Sanga al-maarufu kama 'Jah People Mtu wa watu'
Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga 'Jah People Mtu wa Watu', akiwapongeza maharusi Michael na Rehema, wakati wa sherehe ya ndoa yao jana.
Wataalamu wa kufungua 'Champeign' wakiwajibika mbele ikiwa ni sehemu ya kusherehekea harusi hiyo.
Michael na Rehema, wakinyweshana Shampein, ikiwa ni ishara ya upendo na amani mara baada ya kuyaanza maisha mapya ya ndoa yao.
Maharusi wakipita kwenye meza ya waheshimiwa kugonganisha grasi, ikiwa ni ishara ya kutakiana amani na upendo.
Michael, akimlisha keski mkewe Rehema kwa staili pekee ya heshima aliyoitoa Bi Rehema mbele ya mumewe na wageni waalikwa ilimfurahisha kila mmoja aliyekuwapo ukumbini hapo. Masanja alisema wengine msijaribu kuiga staili hii ya kutembea na magoti kwani kwa binti huyu kwake ni kawaida kulingana na utamaduni wa kabila lake na anakotoka.....
Masanja Mkandamizaji, naye hakuwa mbali katika kutoa burudani ya kuvunja mbavu kwa maharusi na wageni waalikwa, hapa akiwavunja watu mbavu kwa vijichekesho vyake....
Deo Sanga Baba wa Bwana harusi na mkewe, wakisimama na kushangilia wakati wa utambulisho..
Baada ya kumaliza kuwavunja watu mbavu, Masanja naye alifika Meza kuu na kuaga kwa kutoa mkono kwa waheshimiwa.
Habari kwa hisani ya Sufiani