Balozi Juma .V. Mwapachu,
----
African Barrick Gold plc (“ABG”)
UTEUZI WA MJUMBE WA BODI
ABG inafuraha kutangaza kuteuliwa kwa Balozi Juma .V. Mwapachu, Mtanzania, kama
Mkurugenzi Huru, kuanzia Julai, 14, 2011. Balozi Mwapachu ana shahada ya Sheria na alianza taaluma yake katika sekta ya jamii nchini Tanzania kama Wakili wa Serikali na baadae alitumikia Ofisi ya Mambo ya Nje.
Baada ya kipindi cha kufanya kazi kama mshauri wa maswala ya menejimenti ya kampuni ya Coopers & Lybrand Associates, ambayo kwa sasa inajulikana kama PriceWaterhouse Coopers, alifanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa moja kati ya Makundi makuu ya biashara katika sekta isiyo rasmi nchini Tanzania, kabla ya kuanzisha kampuni yake binafsi ya kutoa ushauri.
Wakati wote katika shughuli zake za kazi amekuwa ni mtetezi mkuu wa kuundwa kwa sekta isiyo rasmi yenye nguvu na ari nchini Tanzania. Alikuwa ni Katibu Mwandamizi Mwanzilishi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo mwaka 1988 na alitumikia kama Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda , Tanzania kati ya mwaka 1996 na 2000 na pia kama Mwenyekitii wa Baraza la Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kuanzia mwaka1999 hadi 2000.
Wakati wa kipindi chake, pia alitumikia nafasi kadhaa katika Tume za Rais zilizoimarisha uchumi wa Tanzania kibiashara na zilizochangia katika kuleta mfumo wa vyama vingi vya siasa. Alikuwa mmoja wa timu iliyounda Mtazamo wa Maendeleo wa Tanzania wa 2025. Baadae aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, nafasi aliyoishikilia kuanzia mwaka 2002 hadi 2006.
Kufuatia kurudi kwake Tanzania, amekuwa mstari wa mbele katika shughuli za Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia nafasi yake aliyoishikilia mpaka hivi punde ya Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, nafasi aliyoitumikia kwa miaka mitano hadi mwisho wa Aprili mwaka huu.
Akitoa maoni yake kuhusu uteuzi huo, Mwenyekiti wa ABG, Aaron Regent, amesema, “Bodi inafurahia kumkaribisha Balozi Mwapachu kama mjumbe mpya mwenye upeo wa hali ya juu”. Uzoefu wake nchini Tanzania na kwa upana zaidi katika Afrika, utaongeza upeo mpya kwenye Bodi na kuongeza mchango yakinifu katika kukabili changamoto za utekelezaji wa malengo ya biashara”.
Hayo vilevile ndio yalikuwa maoni ya Mkurugenzi Huru Mkuu, Derek Pannell ambaye aliongeza, “ Katika majadiliano yetu katika miezi iliyopita, nimefurahishwa na uelewa wa Balozi Mwapachu wa mazingira yetu ya kazi na changamoto zinazotukabili, pamoja na hamasa yake ya kuiona Tanzania na Afrika kwa ujumla ikifanikiwa. Ari yake na utaalamu utaiongezea Bodi nguvu na ninamatarijio makuu ya kufanya nae kazi pamoja.”
Uteuzi wa Balozi Mwapachu utafanya jumla ya wajumbe wa Bodi kuwa kumi,ambapo sita ni
Wakurugenzi Huru.
Teweli K. Teweli | PR & Communications | African Barrick Gold (Pty) | Phone: (+255 22) 216 4229 | Mobile: (+255) 767 308 600 | Fax: (+255 22) 2600 210 | Address: African Barrick Gold, Plot 1736 Kahama Rd/Hamza Aziz Rd, Msasani Peninsula, Dar es Salaam, Tanzania | Email: tteweli@ africanbarrickgold.com
No comments:
Post a Comment