Monday, August 1, 2011

WANAFUNZI WAFANYA MITIHANI KATIKA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU MKOANI MOROGORO

Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Bungo ya mkoani Morogoro,akisimamia mtihani leo asubuhi.Wanafunzi wakiendelea na mtihani huo.

wengine wakitafakari na kufikili kwa umakini

KATIKA hali isiyo ya kawaida, wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bungo ya mkoani Morogoro, leo asubuhi walinaswa na mtandao huu wakiwa wametapakaa kwenye uwanja wa mpira wakifanya mtihani huku wakiwa chini ya uangalizi mkali wa mwalimu wao.

Alipohojiwa na mwanidshi wa mtando huu juu ya wanafunzi hao kufanya mtihani kwenye uwanja huo, mwalimu aliyejitambulisha kwa jina moja la Mazinda, alisema uongozi wa shule hiyo uliwapeleka wanafunzi hao kufanya mtihani huo uwanjani hapo kwa lengo la kuwapa nafasi ili wasiangaliane majibu.

'Tumeamua wafanye mtihani huu wa majaribio hapa kiwanjani kwa lengo la kuwapa uhuru zaidi kwani pale darasani huwa wanabanana, lakini sambamba na hilo, hali hii itasadia kwa wale wanafunzi wenye tabia ya kunakiri majibu kutoka kwa wenzao washindwe kufanya hivyo,' alisema mwalimu huyo kwa kujiamini.

Hata hivyo, mwandishi wetu alishuhudia wanafunzi hao wakifanya mtihani huo kwa shida kubwa kwani walilazimika kuinama kwa muda wote wakiwa hapo.
Habari Na Picha Kwa Hisani Ya DUNSTAN SHEKIDELE, /GPL, MOROGORO

4 comments:

Anonymous said...

Imagine shangingi moja tu la mbunge wao linawezaje kubadilisha maisha ya hawa wanafunzi na walimu wao? Je serikali inajali?

Anonymous said...

wanajali kupitisha bajeti za miradi yenye manufaa kwa matumbo yao na si kwa faida ya vizazi vya kesho.

Anonymous said...

That is ridiculous and shameful!!!!!

Anonymous said...

Hii kali jamani serekali inaona kweli mambo haya? Taifa la kesho ndo linavyopata elimu, hii aibu kubwa sana kwa Tanzania, wanajali kuwa na majumba mazuri magari mazuri wabunge wakiwa bungeni kazi yao kusinzia tu na allowanse nyingi shame to you Tanzania.....