Saturday, July 23, 2011

Eliakim Chacha Maswi kukaimu nafasi ya katibu mkuu wizara ya nishati na madini





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Kufuatia Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Bwana David K. Jairo, kupewa likizo kwa muda, Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L. Luhanjo, amemteua Bwana ELIAKIM CHACHA MASWI, kuwa KAIMU KATIBU MKUU, Wizara ya Nishati na Madini kuanzia leo tarehe 22 Julai, 2011. Bwana MASWI, kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.Imetolewa na Premi Kibanga,Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,Ikulu.Dar es salaam.22 Julai, 2011

No comments: