Thursday, July 21, 2011

GRAND MALT YAIMWAGIA TIMU YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZNZ VIFAA VYA MICHEZO

Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abdilah Jihad akionesha na baadhi ya viatu walivyokabidhiwa na Meneja wa Grand Malt Bi Consolata Adam. Waziri wa Habari, Utalii,Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad (kushoto) akipokea jezi kutoka kwa Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam kwa ajili ya timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar itakayopambana na timu ya Klabu ya Wazee ya Arusha Septemba 8, mwaka huu. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Baraza, Mbarouk Mussa. Grand Malt ambayo imetoa vifaa hivyo vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10, ni wadhamini wa bonanza litaloshirikisha pia vilabu vingine vya veterani. Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad akitangaza rasmi kuwa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt kimeruhusiwa kudhamini michezo na shughuli mbalimbali kisiwani Zanzibar. Alitangaza jana mjini Zanzibar wakati Grand Malt ilipotoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10 kwa ajili ya bonanza la veterani litakalofanyika Arusha Septemba 8, mwaka huu. Kulia ni Meneja wa kinywaji hicho, Consolata Adam na Makamu Mwenyekiti wa timu ya baraza, Mbarouk Mussa. (PICHA NA MARTIN KABEMBA) Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam (kulia) akihutubia katika hafla hiyo. Baadhi wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo

No comments: