Friday, July 22, 2011

MWANDISHI NA MPIGA PICHA WA GAZETI LA SANI ATOA SHUKURANI ZAKE


Ninawashukuru wote mliokuwa pamoja nami kwenye kipindi chote cha matatizo yaliyonikumba huko Manzese baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira na hatimaye kupasuliwa kichwa nikiwa katika harakati za kutimiza wajibu wangu wa uandishi wa habari.




Hii kwangu naipokea kama changamoto katika kuendelea kuchapa kazi, kwani taaluma yangu ya uandishi wa habari iko ndani ya moyo wangu hivyo ninaichukulia kama wito.bado nitaendelea kuwatumikia.


Nakushukuru sana kaka yangu, ndugu yangu rafiki yangu John Bukuku na mtandao wako pendwa wa fullshangwe kwa ushirikiano wako ikiwa ni kuchapisha tamko la Chama cha Wapiga picha za habari Tanzania juu ya tukio hilo.


Shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wa chama hicho Mroki Mroki ambaye kwa uchungu mkubwa na kuonesha jinsi anavyotujali waandishi wenzake aliona upo umuhimu kwa chama kutoa tamko la kulaani kitendo hicho cha wananchi wa Manzese kushambulia waandishi wa habari.


Natoa shukrani kwa mitandao yote na ukiwemo wa Michuzi Junior, Global Publishers, Super D, na mtu yoyote aliyeguswa na tukio hilo kwani lilinipa faraja wakati wote wa matatizo na kuniongeza ujasiri.Shukrani za dhati,Sasa nimepona na nimerejea mtaani.
Christopher Lissa a.k.a Rais wa udaku Mwandishi wa gazeti la SANI.Hivi ndivyo nilivyopewa kipondo.

No comments: