Picha juu ni za Timu ya wakongwe wa muziki wa dansi Wakijisua kisawasawa kwa ajili ya Tamasha la Sauti za Kale litakalofanyia leo jijini Dar es Salaam
--
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAMASHA LA SAUTI ZA KALE
21/07/2011
Timu ya wakongwe wa muziki wa dansi nchini inayowakusanya wanamuziki akiwemo Kingkikii, Mafumu Bilali, Kasongo Mpinda, john Kitime, Abdul Salvador, Babu Njenje, Mzee Waziri na wengineo, wanatarajia kufanya tamasha lao ambalo hufanyika kila mwaka na safari hii liko njiani kuelekea kileleni kwani linatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Selander Bridge maeneo ya Upanga tarehe 22 Julai 2011.
Lengo la tamasha hilo ni kuhuisha uwepo wa wanamuziki wa zamani kwa kudhihirisha kuwa uwezo wao kisanii bado uko juu, halikadhalika mchango wao katika kudumisha sanaa ya muziki wa Tanzania upo pale pale na pia kuikumbusha jamii kuwa walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo.
Nia yao nyingine, ni kuweka daraja baina ya wanamuziki wakongwe na wasasa ili kutengeneza muendelezo mzuri unaotokea kwenye chimbuko la muziki wa kitanzania na kuwaonesha vijana wanaochipukia kisanii kuwa muziki umetoka wapi, unaenda wapi na umefika wapi.
Siku hiyo inatarijiwa kuwa ni siku ya aina yake kwani wakongwe hao wanatarajia kutambulisha wimbo wao mmoja na mpya kati ya nyimbo tatu walizorekodi, na wimbo huo unajulikana kwa jina la Tanzania, wakiwa wame urudia katika midundo ya kisasa,kwani wenyewe ulipigwa na Atomic Jazz Band chini ya utunzi wake Steven Hiza mnamo mwaka 1965.
Wakongwe hao wameshakamilisha nyimbo zao tatu ikiwepo hiyo Tanzania, Miaka Hamsini ya uhuru pamoja na Kilimo kwanza na zote hizo chini ya usimamizi wake Prodyuza Allan Mapigo wa Metro Studio.
Kwa kuwapa Saport wakongwe hao ni kuchangia kwa kiasi kikubwa kuuinua muziki wa watanzania.
Wote Mnakaribishwa
SAUTI ZA KALE.
No comments:
Post a Comment