Thursday, August 18, 2011

MAWAKALA WA PEMBEJEO RUVUMA WALIA NA SERIKALI


Mkuu wa Wilaya ya Songea Thomas Oley Sabaya


MAWAKALA wa Vocha za Pembejeo mkoani Ruvuma wameilalamikia serikali kupitia wizara ya Kilimo na Chakula kwa kushindwa kuwalipa fedha zao zaidi ya sh.milioni 700 ambazo walifanyia kazi ya kusambaza pembejeo za kilimo kwa wakulima wa Mkoa huo katika kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu.
Wakizungumza na mwandishi wa matandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mkoani Ruvuma Stephano Mango , wafanyabiashara hao walisema kuwa serikali hadi sasa haijawalipa fedha jambo ambalo limewafanya waishi katika mazingira magumu na wengine walikuwa na mikopo kwenye taasisi za fedha na kusababisha mikopo hiyo liba kuongezeka siku hadi siku.
Issaya Mbilinyi wakala wa kusambaza pembejeo katika halimashauri ya manispaa ya Songea na Songea vijijini alisema kuwa katika kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu amesambaza pembejeo kwa wakulima zenye thamani ya sh. Milioni 150 lakini mpaka sasa hajui hatima ya malipo yake kwani amejaribu kufuatilia mala nyingi wilayani bila ya kuwa na mafanikio.
Alisema kuwa katika kipindi hicho amesambaza pembejeo katika vituo 60 ambavyo viko ndani ya manispaa ya Songea na Songea vijijini lakini anapofuatilia uongozi wa kilimo Wilaya na Mkoawamekuwa na ahadi ya kuwakata wawe na subira serikali itawalipa licha ya kuwa madhala wanayoyapata ni makubwa.
“Ndugu waandishi serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM) mpaka sasa inashindwa kuwalipa mawakala wa pembejeo za kilimo na hapa tupo zaidi ya 70 ambao tulifanya kazi kubwa ya kusambaza mbolea vijijini kwa wakulima na kufanikisha wakulima kupata mavuno mazuri mwaka huu, sasa kwa msimu wa kilimo wa mwaka ujao mawakala tuna shindwa kujianda kutafuta mbolea kwani fedha hatuna kwani mtaji wote umebaki serikalini.”alisema Mbilinyi.
Naye Willy Kayombo ambaye ni wakala wa pembejeo za kilimo wilayani Songea alisema kuwa kutokana na serikali kushindwa kulipa fedha zao wanazodai kwa wakati tayari umevuruga utaratibu wa usambaji wa mbolea kwa msimu wa kilimo wa mwaka 20011 na 2012.
Kayombo ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Mkoa wa Ruvuma alisema kuwa mawakala wamekuwa na utaratibu wa kujipanga mapema kutafuta pembejeo kabla hazijapanda bei kwenye makampuni ya mbolea makubwa ili kuweza kufanikisha zoezi ima la usambazaji wa mbolea kwa wakulima.
Hata hivyo alibainisha kuwa kutokana na serilikali kuchelewesha malipo hayo kumesabisha bei ya mbolea kupanda kwa mfuko mmoja wa UREA wenye uzito wa kilo 50 kutoka sh. 40,000 hadi 60,000 CAN mfuko wa kilo 50 kutoka sh. 39,000 hadi 45,000, SA mfuko wa kilo 50 kutoka sh.38, 000 hadi sh.40,000 na DAP mfuko wa kilo 50 unauzwa sh.70,000 na hii ni kutokana na kushuka kwa shilingi.
Naye Anjelo Mwalongo alisema kuwa serikali inatakiwa iwalipe pesa zao mapema ili waweze kusambaza pembejeo kwani uzalishaji wa zao la mahindi hauwezi kuongezeka bila kutambua mchango wa mawakala wa pembejeo ndio wanao wawezesha wakulima kufanikisha azimio la kilimo kwanza hasa ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa sita inayotegemewa kwa kilimo cha zao hilo hapa Nchini.
Mwalongo ameitaka serikali kulipa mapema fedha zao vinginevyo msimu ujao wa kilimo kwa umoja wao watagoma kusambaza pembejeo za kilimo kwa Mkoa wa Ruvuma na kujiondoa kwenye orodha ya mawakala nchini kwani usumbufu wanaoupata ni mkubwa licha ya ugumu wa kazi yao ya kusambaza pembejeo mkoani humo.
Alipopigiwa simu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Christin Ishengoma kama anataarifa zozote za madai ya mawakala wa pembejeo za kilimo hakuweza kupatikana kwani yuko Bungeni Dodoma.
HABARI KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN

No comments: