Wednesday, August 17, 2011

Mgogoro Wa Ardhi Kijiji Cha Kerege Bagamoyo

Wananchi wakiangalia shamba la ekali 36 mali ya kijiji cha Kerege ambalo limeuzwa kwa mekezaji kinyume na utaratibu.


Sehemu ya ardhi yenye ukubwa wa hekali 36.5 mali ya kijiji cha Kerege, kilchopo wiliyani Bagamoyo ambayo limeuzwa kwa mwekezaji Iinjinia Joackim Msaki.



Mifugo ya mwekezaji ikiwa ikiwa katika shamba hilo.


Siku chache zilizopita kijijini hapa (mjengwablog) tuliripoti kwa ufupi juu ya sakata la mgogoro wa ardhi yenye ukubwa wa hekeli 36.5 mali ya Kijiji cha Kelege, Wilaya ya Bagamo mkoa wa Pwani kudaiwa kuuzwa kwa mwekezaji Joackim Msaki, mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam kinyume na taratibu.


Ardhi inayogombewa ni ile ambayokijiji iliitenga kwa ajili ya shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa Shule, Zahanati


Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo,wanasema kuwa ardhi hiyo ilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari, msingi na zahanati ya kijiji, lakini katika mazingira yanayoashiria kuwepo kwa ufisadi unaohusisha uongozi wa kijiji ardhi hiyo imeuzwa kinyemela kwa mwekezaji anayetaka kujenga Hoteli ya kitalii na wananchi wanaoonesha kukerwa na hatua hiyo, wengi wao wameishia kufunguliwa kesi za kila aina kwa lengo la kunyamazishwa.


Uongozi unaodaiwa kufanya ufisadi huo, tayari umejiuzulu, na kijiji hicho hivi sasa hakina uongozi unaoeleweka. Hii maana yake ni kwamba hakuna huduma ya kiserikali inayoendelea kijijini hapo.
Wananchi hao wanaelezakwamba, licha ya kutokuwepo kwa uongozi wa kijiji, Polisi ambao ndiyo wangekuwa kimbilio lao, wamegeuka kuwa vibaraka wa mwekezaji kwa kuwanyanyasa


Katibu wa Kamati ya matumizi bora ya Ardhi ya Kijiji cha Kerege, Kitongoji cha Amani, Haji Sheja, alisema viongozi wa kijiji wakishirikiana na mwekezaji wamekuwa wakiwatumia Askari Polisi wa Kituo cha Mapinga kuwakamata wananchi na kuwabambikia kesi.
Askari waliotajwa na wananchi hao ni SGT Mapesa na CPL Jeremia. Wanasimulia wananchi hao kuwa Juni 6 mwaka jana, walikamatwa wanakijiji watatu na kuwaweka ndani kwa kosa la kuvamia ardhi ya mwekezaji, lakini cha kushangaza walipojitokeza wadhamini wa watu hao, nao waliwekwa ndani na kufunguliwa shitaka la kutishia kuua.
Katika orodha y watu waliogawiwa ardhi kisheria kijiji hapo, ambayo mwandishi wa habari hizi aliionaa, naonyesha kuwa, mwekezaji Joackim Msaki anayeishi Upanga jijini Dar es Salaam, alimilikishwa ardhi yenye ukubwa wa ekari 20 tu iliyonunuliwa na Andrew Msaki .
“Hata hivyo katika orodha (leja) ya kijiji hicho iliyoandikwa mwaka 1984 inaonesha, Andrew Msaki alipewa ardhi ya Kijiji hicho yenye ukubwa wa ekari 20.



“Hapa mnapotuona watoto wetu wanatembea kilometa zaidi ya 11 kwenda shule kila siku kutokana na kutokuwepo kwa shule, tulikuwa na mipango ya kuhakikisha tunakuwa na shule lakini ndoto hizo zimeyeyushwa na viongozi wetu walioamua kuuza ardhi kwa manufaa binafsi,” alisema Sheja


Aidha, uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi wilayani Bagamoyo ambayo inahusisha ‘vigogo’ serikalini wakiwemo baadhi ya watuhumiwa wa EPA ambao wanadaiwa kumiliki ardhi maeneo hayo kinyume na taratibu.
Natoa wito kwa mamlaka zinazohusika kwenda kijijini Kerege, kukutana na wananchi na kujui ukweli wa sakata hilo na kulitafutia ufumbuzi haraka. Kinyume cha hayo upo uwezekana mkubwa siku za usoni, kukajitokeza vurugu kubwa zitakazosababisha uvunjifu wa amani kijini hapo.
Habari na Picha, Victor Makinda

No comments: