Monday, August 15, 2011

Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Atembelea Kituo Cha Ununuzi Wa Karafuu


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,akimsiliza jambo Mtoto Hamadi Hassan wa darasa la Nne Skuli ya msingi Daya Mtambwe,mara baada ya kukitembelea kituo cha ununuzi wa zao la Karafuu cha Daya Mtambwe,pia kuzungumza na wakulima wa zao hilo jana,katika Wilaya ya Wete jana.(13/08/2011)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakijumuika na wakulima wa zao la kafuu kuchambua karafuu zilizochumwa katika kambi ya karafuu Daya Mtambwe,akiwa katika ziara ya kutembelea kambi za wachumaji wa karafuu,Mkoa wa Kaskazini Pemba.(13/08/2011)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiangalia magunia ya karafuu zilizonunuliwa katika kituo cha ZSTC Daya Mtambwe jana walipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho pamoja kambi za wachumaji wa Karafuu,Wilaya ya wete jana,(kushoto) Naibu Mkurugenzi wa ZSTC Pemba Hamad Khamis Hamad,(13/08/2011)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akijumuika na waislamu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Futari maalum aliyowaandalia waislamu hao jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete.(13/08/2011)
Baadhi ya Magunia ya karafii 31 yaliyokamatwa yakiwa katika banda la ZSTC katika bandari ya Wete chini ya Ulinzi mkali ikiwa bado hatua za kuwatafuta wahusikka zinafanywa.(13/08/2011)
Baadhi ya wakulima wa zao la karafuu wakisubiri kuuza karafuu zao katika kituo cha ununuzi wa zao hilo huko Daya Mtambwe,Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,wananchi wengi wamehamasiki kufika katika vituo mbali mbali kuuza karafuu.(13/08/2011).
Picha na Ikulu-Zanzibar


No comments: