Sunday, August 21, 2011

Ubalozi wetu London wafutarisha wadau, wahimiza ushirikiano na upendo kwa wote


Asalaam Aleikhum,
Ubalozi wa Tanzania Hapa London Ijumaa uliwaalika watanzania kutoka madhehebu na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu. Vyakula vya aina mbalimbali viliandaliwa katika hadhi ya kitanzania. Naibu Balozi Mh Chabaka Kilumanga aliwashukuru wadau wote ambao walioweza kujumuika na kufuturu kwa pamoja. Aidha Mh Kilumanga aliahidi kushirikiana na watanzania kwa ukaribu zaidi kwa hali na mali pia kuwaomba kutoa ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aliendelea kwa kusema Ubalozi upo kwa ajili ya wote hivyo kila mtu na autumie ipasavyo.

Kwa niaba ya URBAN PULSE CREATIVE Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ubalozi wetu kwa namna walivyojitolea kutengeneza futari na kuwakaribisha wadau kuja kufuturu.

Asanteni Sana,

MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
URBAN PULSE CREATIVE
Waalikwa wakiomba dua baada ya kufuturu katika ubalozi wetu London, Ijumaa
Naibu Balozi Mh. Chabaka Kilumanga akitoa shukrani na neno kwa waalikwa
Sehemu ya wageni

Afisa ubalozi Bw. Zamarani akikaribisha wageni kufuturu

Baadhi ya waalikwa kinama wakifuturu
Mkuu wa utawala na fedha ubalozini hapo Da'Carol Chipeta (shoto) akipozi
na Da' Jestina George

No comments: