Friday, April 20, 2012

Hakuna mionzi yoyote katika simu: TCRA yakanusha vikali uvumi wa kuwepo kwa mionzi kwa watumiaji wa simu za mikononi nchini


Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) imetoa taarifa usiku huu juu ya ujumbe mfupi wa simu uliokuwa ukisambazwa kwa watumiaji wa simu za mikononi hapa nchini uliokuwa ukieleza kuwa ifikapo saa tano usiku (kwa masaa ya Afrika Mashariki) watumiaji wa simu hizo wanatakiwaa kuzizima simu zao kutokana na mionzi ya Sarari moja ambayo ingepita karibu na Dunia na ambayo inasemekana kutokana na mionzi hiyo watu watumiao simu hizo wangeweza kupoteza maisha au kupatwa na madhara makubwa kama wasingekuwa wamezima simu zao.

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) imekanusha vikali taarifa hizo na kusema taarifa hizo ni za uongo na kuifananisha taarifa hii na ile ya miaka kadhaa iliyopita ilikuwa ikisema kuwa kuwa makini na ujumbe mfupi wa mionzi.

TCRA imewataka wananchi woote na watumiaji wa simu za mkononi nchini,kuzipuuza taarifa hizo kwani hazina ukweli wowote na zimeanzishwa na mtu ambaye hana lengo zuri kwa watumiaji wa simu za mikononi.

No comments: