Taarifa zilizo tufikia muda huu kutoka Arusha zinasema Mgomo unaendelea, Madereva hao wanasema polisi wamekuwa wanawanyanyasa sana na wamekuwa wakibambikizwa kesi ambazo haziwahusu ,hali haikuwa nzuri asubuhi kwani wananchi wengi wa Arusha wengi walitembea kwa miguu,pikipiki zilipanda bei leo,wengine walitumia baskeli za kukodi, Mdau mmoja alie kuwepo eneo hilo alisema "nilitaka kuwapa watu lift kwenye gari langu nikaonywa kwani kunabaadhi waliotangulia kutaka kufanya hivyo walitaka kuvunjiwa magari" Lakini hata hivyo mpaka sasa makondaa na drives wanalinda vituo vya basi kuhakikisha hakuna mtu anatoa hiyo huduma.. Habari zaidi itawajia baadae
No comments:
Post a Comment