Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
_____________
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 1977
(Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977,
limezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Katiba
ya Muungano tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000.
Dar es Salaam, A.J.
CHENGE
1 Novemba, 2000 Mwanasheria Mkuu
2000
KIMEPIGWA CHAPA NA MPIGACHAPA WA SERIKALI
DAR ES SALAAM - TANZANIA
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
2
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
YA MWAKA 1977
____________
YALIYOMO
_____________
Ibara Kichwa cha Habari
UTANGULIZI
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NA
SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA
SEHEMU YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO NA WATU
1. Kutangaza Jamhuri ya Muungano.
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano.
3. Tangazo la nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi.
4. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi.
5. Haki ya kupiga kura.
SEHEMU YA PILI
MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO
WA SHUGHULI ZA SERIKALI
6. Ufafanuzi.
7. Matumizi ya Masharti ya Sehemu ya Pili.
8. Serikali na Watu.
9. Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea.
10. [Imefutwa na Sheri Na. ……… ibara ya ……..].
11. Haki ya kufanya kazi, kupata elimu, na nyinginezo.
SEHEMU YA TATU
HAKI NA WAJIBU MUHIMU
Haki ya Usawa
12. Usawa wa Binadamu.
13. Usawa mbele ya sheria.
Haki ya Kuishi
14. Haki ya kuwa hai.
15. Haki ya uhuru wa mtu binafsi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
3
16. Haki ya faragha na ya usalama wa mtu.
17. Uhuru wa mtu kwenda atakako.
Haki ya Uhuru wa Mawazo
18. Uhuru wa maoni.
19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.
20. Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.
21. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.
Haki ya Kufanya Kazi
22. Haki ya kufanya kazi.
23. Haki ya kumiliki mali.
24. Haki ya kupata ujira wa haki.
Wajibu wa Jamii
25. Wajibu wa kushiriki kazini.
26. Wajibu wa kutii sheria za nchi.
27. Kulinda mali ya Umma.
28. Ulinzi wa taifa.
Masharti ya Jumla
29. Haki na wajibu muhimu.
30. Mipaka kwa haki, uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu.
Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi
31. Ukiukaji wa Haki na uhuru.
32. Madaraka ya kutangaza hali ya hatari.
SURA YA PILI
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
RAIS
33. Rais wa Jamhuri ya Muungano.
34. Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.
35. Utekelezaji wa shughuli za Serikali.
36. Mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu wa kushika nafasi za madaraka.
37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais n.k.
38. Uchaguzi wa Rais.
39. Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais.
40. Haki ya kuchaguliwa tena.
41. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais.
42. Wakati na muda wa kushika madaraka ya Rais.
43. Masharti ya kazi ya Rais.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
4
44. Madaraka ya kutangaza vita.
45. Uwezo wa kutoa msamaha.
46. Kinga dhidi ya mashtaka na madai.
46A. Bunge laweza kumshtaki Rais.
46B. Wajibu wa viongozi Wakuu wa vyombo vya Mamlaka ya Utendaji
kudumisha Muungano.
SEHEMU YA PILI
MAKAMU WA RAIS
47. Makamu mmoja wa Rais, kazi na Mamlaka yake.
48. Wakati wa Makamu wa Rais kushika madaraka.
49. Kiapo cha Makamu wa Rais.
50. Muda wa Makamu wa Rais kushika Madaraka.
SEHEMU YA TATU
WAZIRI MKUU, BARAZA LA
MAWAZIRI NA SERIKALI
51. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
52. Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu.
53. Uwajibikaji wa serikali.
Baraza la Mawaziri na Serikali
53A. Kura ya kutokuwa na imani.
54. Baraza la Mawaziri.
55. Uteuzi wa Mawaziri.
56. Kiapo cha Mawaziri na Naibu Mawaziri.
57. Wakati na muda wa Mawaziri kushika madaraka.
58. Masharti ya kazi ya Mawaziri.
59. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
60. Katibu wa Baraza la Mawa ziri.
61. Wakuu wa Mikoa.
SURA YA TATU
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
BUNGE
62. Bunge.
63. Madaraka ya Bunge.
64. Madaraka ya kutunga Sheria.
65. Muda wa Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
5
SEHEMU YA PILI
WABUNGE, WILAYA ZA UCHAGUZI NA UCHAGUZI
WA WABUNGE
66. Wabunge.
67. Sifa za mtu kuwa Mbunge.
68. Kiapo cha Wabunge.
69. Tamko rasmi la Wabunge kuhusu maadili ya Viongozi.
70. Wabunge kutoa taarifa ya mali.
71. Muda wa Wabunge kushika madaraka kama Wabunge.
72. Watu wenye madaraka Serikalini kukoma utumishi wanapochaguliwa.
73. Masharti ya kazi ya Wabunge
74. Tume ya Uchaguzi
75. Majimbo ya Uchaguzi.
Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge
76. Uchaguzi katika Majimbo ya Uchaguzi.
77. Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge wa Majimbo ya Uchaguzi.
78. Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge Wanawake wa kuchaguliwa na Bunge.
79. Utaratibu wa uchaguzi wa Wabunge wa kuchaguliwa na Baraza la
Wawakilishi.
80. [Imefutwa na Sheria Na.4 ya 1992 - ib.27].
81. Utaratibu wa kupendekeza majina ya wagombea uchaguzi wa Wabunge
Wanawake.
82. [Imefutwa na Sheria Na.4 ya 1992 - ib.29].
83. Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge au sivyo.
SEHEMU YA TATU
UTARATIBU, MADARAKA NA HAKI ZA BUNGE
Spika na Naibu wa spika
84. Spika na Mamlaka yake.
85. Naibu wa Spika.
86. Utaratibu wa kumchagu Spika na Naibu wa Spika.
Ofisi ya Bunge
87. Katibu wa Bunge.
88. Sekretariati ya Bunge.
Utaratibu wa shughuli Bungeni
89. Kanuni za Kudumu za Bunge.
90. Kuitishwa kwa mikutano ya Bunge na kuvunjwa kwa Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
6
91. Rais aweza kulihutubia Bunge.
92. Mikutano ya Bunge.
93. Uongozi wa vikao vya Bunge.
94. Kiwango cha vikao vya Bunge
95. Viti vilivyo wazi katika Bunge.
96. Kamati za Kudumu za Bunge.
Utaratibu wa Kutunga Sheria
97. Namna ya kutumia madaraka ya kutunga sheria.
98. Utaratibu wa kubadilisha Katiba hii na baadhi ya sheria.
99. Utaratibu wa kutunga Sheria kuhusu mambo ya fedha.
Madaraka na Haki za Bunge
100. Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuli.
101. Kuhifadhi na kutilia ng uvu uhuru wa majadiliano na wa shughuli.
SURA YA NNE
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,
BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR NA
BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
NA RAIS WA ZANZIBAR
102. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka yake.
103. Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na madaraka yake.
104. Uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
SEHEMU YA PILI
BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR
105. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Kazi zake.
SEHEMU YA TATU
BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
106. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na madaraka ya kutunga Sheria za
Zanzibar.
107. Madaraka ya Baraza la Wawakilishi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
7
SURA YA TANO
UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO,
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO, TUME
YA KUAJIRI YA MAHAKAMA YA TANZANIA BARA,
MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR, MAHAKAMA
YA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO NA
MAHAKAMA MAALUM YA KATIBA YA
JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO
107A. Mamlaka ya Utoaji Haki.
107B. Uhuru wa Mahakama.
SEHEMU YA PILI
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO
108. Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.
109. Majaji wa Mahakama Kuu na uteuzi wao.
110. Muda wa Majaji wa Mahakama Kuu kushika madaraka.
111. Kiapo cha Majaji.
SEHEMU YA TATU
MADARAKA YA KUAJIRI MAHAKIMU NA WATUMISHI
WENGINE WA MAHAKAMA ZA TANZANIA BARA NA TUME YA
KUAJIRI YA MAHAKAMA
112. Tume ya Kuajiri ya Mahakama.
113. Madaraka ya kuajiri Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama.
113A. Uanachama katika Vyama vya Siasa.
SEHEMU YA NNE
MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR
114. Mahakama Kuu ya Zanzibar.
115. Mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.
SEHEMU YA TANO
MAHAKAMA YA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO
116. Tafsiri.
117. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Madaraka yake.
118. Majaji wa Mahakama ya Rufani na uteuzi wao.
119. Mamlaka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
8
120. Muda wa Majaji wa Mahakama ya Rufani kushika madaraka.
121. Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Rufani.
122. Kiwango cha vikao vya Mahakama ya Rufani.
123. Mashauri yanayoweza kuamuliwa na Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani.
SEHEMU YA SITA
UTARATIBU WA KUPELEKA HATI ZA KUTEKELEZA
MAAGIZO YALIYOMO KATIKA HATI ZILIZOTOLEWA
NA MAHAKAMA
124. Utekelezaji wa maagizo ya Mahakama utafanywa nchini Tanzania kote.
SEHEMU YA SABA
MAHAKAMA MAALUM YA KATIBA
YA JAMHURI YA MUUNGANO
125. Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
126. Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Katiba
127. Muundo wa Mahakama Maalum ya Katiba
128. Utaratibu katika vikao vya Mahakama Maalum ya Katiba.
SURA YA SITA
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
NA SEKRETARIET YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
SEHEMU YA KWANZA
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
129. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
130. Majukumu ya Tume na Taratibu za Utekelezaji.
131. Mamlaka ya Tume na utaratibu wa shughuli zake.
SEHEMU YA PILI
SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
132. Sekretarieti ya Maadili.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
9
SURA YA SABA
MASHARTI KUHUSU MCHANGO WA SERIKALI NA MAMBO
MENGINEYO YA FEDHA ZINAZOINGIA KATIKA HAZINA YA
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
MCHANGO NA MGAWANYO WA MAPATO YA
JAMHURI YA MUUNGANO
133. Akaunti ya Fedha ya Pamoja.
134. Tume ya Pamoja ya Fedha.
SEHEMU YA PILI
MFUKO MKUU WA HAZINA NA FEDHA
ZA JAMHURI YA MUUNGANO
135. Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
136. Masharti ya kutoa fedha za matumizi kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya
Serikali.
137. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu
wa Hazina ya Serikali.
138. Masharti ya kutoza kodi.
139. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya sheria ya matumizi
kuanza kutumika.
141. Mfuko wa Matumizi ya dharura.
142. Deni la Taifa.
142. Mishahara ya watumishi fulani wa Serikali kudhaminiwa na Mfuko Mkuu
Wa Hazina ya Serikali.
143. Mdhibiti wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya
Muungano.
144. Kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.
SURA YA NANE
MADARAKA YA UMMA
145. Serikali za Mitaa.
146. Kazi za Serikali za Mitaa.
SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI
146. Marufuku kuunda majeshi ya ulinzi yasiyo majeshi ya ulinzi ya Umma.
148. Madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu.
SURA YA KUMI
MENGINEYO
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
10
149. Maelezo ya mambo yanayohusika na madaraka ya kazi mbalimbali
zilizoanzishwa na Katiba hii.
150. Maelezo kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka ya kazi katika Utumishi
wa Serikali.
152. Ufafanuzi.
152. Jina kamili la Katiba, tarehe ya kuanza kutumika na
NYONGEZA YA KWANZA
NYONGEZA YA PILI
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
11
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA YA MWAKA 1977
UTANGULIZI
MISINGI YA KATIBA
Sheria ya 1984
Na.15 ib.3
KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi
yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na
amani:
NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika
jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na
Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha
wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu
wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo
kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na
kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:
KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE
MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii
kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania
inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia
na ujamaa.
SURA YA KWANZA
Sheria ya 1984
Na.15
ib.5
JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA,
WATU NA SIASA YA UJAMAA NA
KUJITEGEMEA
SEHEMU YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO NA WATU
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
12
Kutangaza
Jamhuri ya
Muungano
Sheria ya 1984
Na.15 ib
1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
Sheria ya 1992
Na.4 ib.3
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge:
Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais
wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika
Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.
Tangazo la nchi
yenye Mfumo wa
vyama vingi
Sheria ya 1992
Na.4 ib.5
3.-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na
ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji
wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa
ajili hiyo.
Utekelezaji wa
shughuli za
Mamlaka ya Nchi
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
4.-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri
ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili
vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka
ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye
mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa
shughuli za umma.
(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki
vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na
kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni
Bunge na Baraza la Wawakilishi.
(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma
katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa
madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa
katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama
yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
13
mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na Mambo yasiyo
ya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo Mambo
ya Muungano.
(4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa
na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengine
yaliyomo katika Katiba hii.
Haki ya kupiga
kura
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
Sheria ya 2000
Na.3 ib.4
5.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka
kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi
unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa
kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti
mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini
Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.
(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti
yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana
na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo-
(a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;
(b) kuwa na ugonjwa wa akili;
(c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;
(d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa
kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama
mpiga kura,
mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyote
inayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.
(3) Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuweka
masharti kuhusu mambo yafuatayo-
(a) kuanzisha Daftari la Kudumu la Wapiga kura na
kuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katika
Daftari hilo;
(b) kutaja sehemu na nyakati za kuandikisha wapiga
kura na kupiga kura;
(c) utaratibu wa kumwezesha mpiga kura
aliyejiandikisha sehemu moja kupiga kura sehemu
nyingine na kutaja masharti ya utekelezaji wa
utaratibu huo;
(d) kutaja kazi na shughuli za Tume ya Uchaguzi na
utaratibu wa kila uchaguzi ambao utaendeshwa
chini ya uongozi na usimamizi wa Tume ya
Uchaguzi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
14
SEHEMU YA PILI
MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO
WA SHUGHULI ZA SERIKALI
Ufafanuzi
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
6. Katika Sehemu hii ya Sura hii, isipokuwa kama maelezo
yahitaji vinginevyo, neno "Serikali" maana yake ni pamoja na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka
au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote.
Matumizi ya
masharti ya
Sehemu ya Pili
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
7.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali,
vyombo vyake vyote na watu wote au mamlaka yoyote yenye
kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria
au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa
kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya
Sehemu hii ya Sura hii.
(2) Masharti ya Sehemu hii ya Sura hii hayatatiliwa nguvu ya
kisheria na Mahakama yoyote. Mahakama yoyote nchini
haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda au
kukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote, au kama
sheria, au hukumu yoyote, inaambatana na masharti ya
Sehemu hii ya Sura hii.
Serikali na watu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(2) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vyombo
vyake na uendeshaji wa shughuli zake, utatekelezwa kwa
kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya kukuza
umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
15
Ujenzi wa
Ujamaa na
Kujitegemea
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
Sheria Na.4
ya 1992 ib.6
9. Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa
chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na
kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitiza
utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira
yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya
Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na
shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-
(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu
zinaheshimiwa na kuthaminiwa;
(b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
(c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia
ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa
unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa
manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia
mtu kumyonya mtu mwingine;
(d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa
na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi
anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli
yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;
(f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na
kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la
Dunia kuhusu Haki za Binadamu;
(g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma
vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa
waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya
mtu;
(h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi,
rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
(i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo
maendeleo ya wananchi na hasa zaidi
yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha
umaskini, ujinga na maradhi;
(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia
zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia
kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache
binafsi;
(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya
demokrasia na ujamaa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
16
Nafasi na
mamlaka ya
Chama
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
10. [Ibara ya 10 ya Katiba imefutwa na Sheria Na.4 ya
1992].
Haki ya kufanya
kazi, kupata
elimu na
nyinginezo
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
11.-(1) Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili
ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya
kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii
wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali
nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi. Na bila kuathiri haki hizo,
Mamlaka ya Nchii itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba
kila mtu anaishi kwa jasho lake.
(2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia
atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia
upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.
(3) Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu
wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata
elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo
vinginevyo vya mafunzo.
SEHEMU YA TATU
HAKI NA WAJIBU MUHIMU
Haki ya Usawa
Usawa wa
binadamu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
12.-(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na
kuthaminiwa utu wake.
Usawa mbele
ya Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,
bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
sheria.
Sheria ya Na.4
ya 1992 ib.8
Sheria ya 2000
Na.3 ib.5
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka
yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo
ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya
watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa
mujibu wa sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
17
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au
mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria
yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya
Mamlaka ya Nchi.
(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii
neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji
mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao,
kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,
jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina
fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na
kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa
aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida
iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno
"kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali
kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha
matatizo katika jamii.
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,
Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia
misingi kwamba -
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji
kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo
kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na
haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na
pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya
kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au
chombo hicho kingenecho kinachohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka
itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa
hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya
kitendo chohote ambacho alipokitenda hakikuwa ni
kosa chini ya sheria, na pia kwamba ni marufuku kwa
adhabu kutolewa ambayo ni kubwa kuliko adhabu
iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendwa;
(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,
heshima ya mtu itatunzwa katika shughuli zote
zinazohusu upelelezi na uendeshaji wa mambo ya
jinai na katika shughuli nyinginezo ambazo mtu
anakuwa chini ya ulinzi bila uhuru, au katika
kuhakikisha utekelezaji wa adhabu;
(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama
au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
18
Haki ya Kuishi
Haki ya kuwa hai
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
14. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii
hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.
Haki ya Uhuru
wa mtu binafsi
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
15.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama
mtu huru.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na
kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini,
kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake
vinginevyo, isipokuwa tu-
(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na
sheria, au
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu
iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na
mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.
Haki ya faragha
na usalama wa
mtu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi
kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na
unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na
mawasiliano yake ya binafsi.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa
ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu
hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya
usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza
kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.
Uhuru wa mtu
kwenda atakako
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya
kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika
sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya
kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri
ya Muungano.
(2) Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenye
madhumuni ya -
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
19
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako na
kumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu
kwenda anakotaka ili-
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;
au
(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibu
wowote anaotakiwa na sheria nyingine
kuutimiza; au
(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla au
kuhifadhi maslahi fulani mahususi au
maslahi ya sehemu fulani ya umma,
kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyo
haitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara
hii.
Haki ya Uhuru wa Mawazo
Uhuru wa
Maoni Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.
Uhuru wa mtu
kuamini dini
atakayo Sheria
ya 1984
Na.15 ib.6
Sheria ya 1992
Na.4 ib…
19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani
na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya
Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza
dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na
maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo
nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
20
Uhuru wa mtu
kushirikiana na
wengine Sheria
ya 1984 Na.14
ib.6
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,
kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo
hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au
mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au
kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa
halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho
kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu
watokeapo, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya
Jamhuri ya Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:
(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au
mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya
kisiasa;
(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake
za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya
Muungano;
(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na
kwa njia za kidemokrasia.
(3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti
yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na
vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu
uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.
(4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku
kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au
shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa
kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.
Uhuru wa
kushiriki
shughuli
za umma
Sheria ya 1984
Na.15
ib.6
Sheria ya 1994
Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67
ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya
kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki
katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya
Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa
nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi
waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia
utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
21
(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu
katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha
yake au yanayolihusu Taifa.
Haki ya Kufanya Kazi
Haki ya kufanya
kazi
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
22.-(1) Kila mtu anayo haki ya kufanya kazi.
(2) Kila raia anasta hili fursa na haki sawa, kwa masharti ya
usawa, ya kushika nafasi yoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyo
chini ya Mamlaka ya Nchi.
Haki ya kupata
ujira wa haki
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
23.-(1) Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote,
anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu
wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo
kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.
(2) Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya
haki.
Haki ya kumiliki
mali
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
24.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria za nchi
zinazohusika, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya
hifadhi kwa mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), ni marufuku
kwa mtu yeyote kunyang'anywa mali yake kwa madhumuni ya
kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria
ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili
Wajibu wa
kushiriki kazini
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
25.-(1) Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii,
ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu. Na kila
mtu anao wajibu wa-
(a) kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi
halali na ya uzalishaji mali; na
(b) kutimiza nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikia
malengo ya uzalishaji ya binafsi na yale ya pamoja
yanayotakiwa au yaliyowekwa na sheria.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1),
hakutakuwapo na kazi ya shuruti katika Jamhuri ya Muungano.
(3) Kwa madhumuni ya ibara hii, na katika Katiba hii kwa
jumla, ifahamike kwamba kazi yoyote haitahesabiwa kuwa ni kazi
ya shuruti au kazi ya kikatili au ya kutweza endapo kazi hiyo, kwa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
22
mujibu wa sheria ni-
(a) kazi inayobidi ifanywe kutokana na hukumu au amri
ya mahakama;
(b) kazi inayobidi ifanywe na askari wa jeshi lolote katika
kutekeleza majukumu yao;
(c) kazi ambayo mtu yeyote inabidi aifanye kutokana na
kuwapo hali ya hatari au baa lolote linalotishia uhai
wa ustawi wa jamii;
(d) kazi au huduma yoyote ambayo ni sehemu ya-
(i) majukumu ya kawaida ya kuhakikisha ustawi
wa jamii;
(ii) ujenzi wa taifa wa lazima kwa mujibu wa
sheria;
(iii) jitihada za taifa za kutumia uwezo wa kila
mtu kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha
jamii na uchumi wa taifa na kuhakikisha
maendeleo na tija ya kitaifa.
Wajibu wa kutii
sheria za nchi
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
26.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na
sheria za Jamhuri ya Muungano.
(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na
sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba
na sheria za nchi.
Kulinda mali ya
umma
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri
ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote
inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali
ya mtu mwingine.
(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya
mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu
na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama
watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.
Ulinzi wa Taifa
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
28.-(1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na
kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.
(2) Bunge laweza kutunga sheria zinazofaa kwa ajili ya
kuwawezesha wananchi kutumikia katika majeshi na katika ulinzi
wa taifa.
(3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenye
mkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi,
wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko
wa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
23
eneo la taifa na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa,
hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri
ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia
nchi.
(4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa
la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.
Masharti ya Jumla
Haki ya wajibu
muhimu
Sheria
ya 1984 Na.15
ib.6
29.-(1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya
kufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu
kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilzivyofafanuliwa katika
ibara ya 12 hadi ya 28 za sehemu hii ya Sura hii ya Katiba.
(2) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya
kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.
(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,
hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi
wake.
(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo
maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi
ya nasaba, jadi au urithi.
(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na
Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli
zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu
wengine au maslahi ya umma.
Mipaka kwa
haki
na uhuru na
hifadhi kwa haki
na wajibu
Sheria ya 1984
Na.15
ib.6
Sheria ya 1994
Na.34 ib.6
30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake
imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -
(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine
au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi
mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya
maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya
madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
24
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya
umma;
(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya
mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai
au la jinai;
(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au
maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri
mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza
heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;
(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,
uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya
watu binafsi nchini; au
(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo
linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.
(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii
ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au
wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na
mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza
kufungua shauri katika Mahakama Kuu.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
Katiba hii, Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa
mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake
kwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka
sheria kwa ajili ya-
(a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa
mujibu wa ibara hii;
(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza
mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;
(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya
Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru
na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
25
(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria
yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au
mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu
muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, na
Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika,
kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha
Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi
ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua
hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili
ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha
hitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusika
katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na
sheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa ni
halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda
uliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupi
zaidi ndio uzingatiwe.
Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi
Ukiukaji wa haki
na uhuru
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
31.-(1) Mbali na masharti ya ibara ya 30(2), sheria yoyote
iliyotungwa na Bunge haitakuwa haramu kwa sababu tu kwamba
inawezesha hatua kuchukuliwa wakati wa hali ya hatari, au
wakati wa hali ya kawaida kwa watu wanaoaminika kuwa
wanafanya vitendo vinavyohatarisha au kudhuru usalama wa
taifa, ambazo zinakiuka masharti ya ibara ya 14 na ya 15 za
Katiba hii.
(2) Ni marufuku kwa hatua zilizotajwa katika ibara ndogo ya
(1) ya ibara hii kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria yoyote wakati
wa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa mtu yeyote,
isipokuwa tu kwa kiasi ambacho ni lazima na halali kwa ajili ya
kushughulikia hali iliyopo wakati wa hali ya hatari au wakati wa
hali ya kawaida kushughulikia hali iliyosababishwa na mwenendo
wa mtu anayehusika.
(3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii
hayataidhinisha mtu kunyang'anywa haki yake ya kuwa hai
isipokuwa tu kwa kifo kama matokeo ya vitendo vya kivita.
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii na ibara zifuatazo za
Sehemu hii "wakati wa hali ya hatari" maana yake ni kipindi
chochote ambapo Tangazo la Hali ya Hatari, lililotolewa na Rais
kwa kutumia uwezo aliopewa katika ibara ya 32, linatumika.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
26
Madaraka ya
kutangaza hali
ya hatari
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
32.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa na
Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza hali ya hatari katika
Jamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.
(2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo-
(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita; au
(b) kuna hatari hasa kwamba Jamhuri ya Muungano
inakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita; au
(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani ya jamii au
kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya
Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni
lazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amani
na usalama; au
(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani ya
jamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katika
Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote
ambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumia
mamlaka ya pekee; au
(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au la
baa ya kimazingira ambalo linatishia jamii au sehemu
ya jamii katika Jamhuri ya Muungano; au
(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri ni
tishio kwa nchi.
(3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika
Jamhuri ya Muungano nzima, au katika Tanzania bara nzima au
Tanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara nakala ya tangazo
hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na
Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ataitisha mkutano wa
Bunge, ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali ya
mambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwa
mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya
wajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatari
lililotolewa na Rais.
(4) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti kuhusu
nyakati na utaratibu ambao utawawezesha watu fulani wenye
kusimamia utekelezaji wa mamlaka ya Serikali katika sehemu
mahususi za Jamhuri ya Muungano kumuomba Rais kutumia
madaraka aliyopewa na ibara hii kuhusiana na yoyote kati ya
sehemu hizo endapo katika sehemu hizi kunatokea yoyote kati
ya hali zilizotajwa katika aya ya (c), (d) na (e) za ibara ndogo ya
(2) na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemu hizo, na pia kwa ajili
ya kufafanua utekelezaji wa mamlaka ya Serikali wakati wa hali
ya hatari.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
27
(5) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais kwa mujibu
wa ibara hii litakoma kutumika-
(a) iwapo litafutwa na Rais;
(b) endapo zitapita siku kumi na nne tangu tangazo
lilipotolewa kabla ya kupitishwa azimio lililotajwa
katika ibara ndogo ya (3);
(c) baada ya kupita muda wa miezi sita tangu tangazo
hilo lilipotolewa; isipokuwa kwamba kikao cha Bunge
cha weza, kabla ya muda wa miezi sita kupita,
kuongeza mara kwa mara muda wa tangazo hilo
kutumika kwa vipindi vya miezi mingine sita kwa
azimio litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wa
kikao hicho wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe
wote;
(d) wakati wowote ambapo mkutano wa Bunge
utalitengua tangazo hilo kwa azimio litakaloungwa
mkono na kura za wajumbe waiopungua theluthi mbili
ya wajumbe wote.
(6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi
au utekelezaji wa masharti ya ibara hii, masharti ya sheria
iliyotungwa na Bunge na ya sheria nyingine yoyote, inayohusu
utangazaji wa hali ya hatari kama ilivyotajwa katika ibara hii,
yatatumika tu katika sehemu ya Jamhuri ya Muungano ambapo
hali hiyo ya hatari imetangazwa.
SURA YA PILI
Sheria ya 1984
Na.15 ib 8
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
RAIS
Rais wa
Jamhuri
ya Muungano
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.
Serikali ya
Jamhuri ya
Muungano na
mamlaka yake
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano
katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote
yahusuyo Tanzania Bara.
(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu
utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote
ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
28
(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya
mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia
juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara,
yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,
madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa
ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu
madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii
hayatahesabiwa kwamba-
(a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria
yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au
mamlaka yoyote ambayo si Rais; au
(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya
kisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlaka
yoyote ambayo si Rais.
Utekelezaji wa
shughuli za
Serikali
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
35.-(1) Shughuli zote za utendaji za Serikali ya Jamhuri ya
Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya
Rais.
(2) Amri na maagizo mengine yanayotolewa kwa madhumuni
ya ibara hii yatathibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katika
kanuni zilizowekwa na Rais, kwa kuzingatia masharti ya Katiba
hii.
Mamlaka ya
kuanzisha na
kuwateua watu
wa kushika
nafasi za
madaraka
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 2000
Na.3 ib.6
36.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
Katiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa na
mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna
mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika
nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za
idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika
kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazo
zimetajwa katika Katiba hii au katika sheria mbalimbali
zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuzi
unaofanywa na Rais.
(3) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), masharti
mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria yoyote
inayohusika, mamlaka ya kuwateua watu wengine wote
wasiokuwa viongozi wala watendaji wakuu, kushika nafasi za
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
29
madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
na pia mamalaka ya kuwapandisha vyeo watu hao, kuwaondoa
katika madaraka, kuwafukuza kazi na mamlaka ya kudhibiti
nidhamu ya watu waliokabidhiwa madaraka, yatakuwa mikononi
mwa Tume za Utumishi na mamlaka mengineyo yaliyotajwa na
kupewa madaraka kuhusu nafasi za madaraka kwa mujibu wa
Katiba hii au kwa mujibu wa sheria yoyote inayohusika.
(4) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) hayatahesabiwa
kuwa yanamzuia Rais kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya
watumishi na utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Utekelezaji wa
kazi na shughuli
za
Rais, n.k Sheria
ya 1984 Na.15
ib.9
Sheria ya 1992
Na.4 ib …
Na.20
ib.12,
Sheria yua
1994 Na.34 ib.6
37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na
shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata
ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale
anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya
jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote.
(2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi
kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili,
laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili
au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio
kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa
mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania,
na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu
kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais
kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba
kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi
itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.
(3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na
masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha
Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo
Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na
shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa
kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama
naye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(b) Spika wa Bunge au, kama nafasi yake iwazi au kama
naye hayupo au ni mgonjwa; basi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
30
(c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya
Muungano.
(4) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (b)
na (c) za ibara ndogo ya (3) atatekeleza kazi na shughuli za Rais
kutokana na sababu kwamba mtu mwingine anayemtangulia
katika orodha hiyo hayupo, basi mtu huyo ataacha kutekeleza
kazi na shughuli hizo mara tu mtu huyo mwingine
anayemtangulia atakaporejea na akashika na kuanza kuteleza
kazi na shughuli za Rais.
(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais
kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais
ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi
cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka
Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na
uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
asilimia hamsini ya Wabunge wote.
(6) Ifahamike kwamba kiti cha Rais hakitakuwa kiwazi na
Rais hatahesabiwa kwamba hayuko katika Jamhuri ya Muungano
endapo-
(a) atakuwa hayupo katika mji ambao ndio makao makuu
ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano kwa
kipindi cha muda wa saa ishirini na nne; au
(c) atakuwa ni mgonjwa lakini anatumaini kuwa atapata
nafuu baada ya muda si mrefu.
(7) Iwapo kutatokea lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika
ibara ndogo ya (6) na Rais akiona kuwa inafaa kuwakilisha
madaraka yake kwa muda wa jambo hilo, basi aweza kutoa
maagizo kwa maandishi ya kumteua yeyote kati ya watu
waliotajwa katika aya ya (a) au ya (b) za ibara ndogo ya (3) ya
ibara hii kwa ajili ya kutekeleza madaraka ya Rais wakati yeye
hayupo au ni mgonjwa, na mtu huyo atakayeteuliwa atatekeleza
madaraka hayo ya Rais kwa kufuata masharti yoyote
yatakayowekwa na Rais; isipokuwa kwamba masharti yaliyomo
katika ibara hii ndogo yafahamike kuwa hayapunguzi wala
kuathiri uwezo wa Rais alionao kwa mujibu wa sheria nyingine
yoyote wa kuwakilisha madaraka yake kwa mtu mwingine yeyote.
(8) Rais aweza, akiona inafaa kufanya hivyo, kumwagiza kwa
maandishi Waziri yeyote kutekeleza kazi na shughuli zozote za
Rais ambazo Rais atazitaja katika maagizo yake na Waziri
aliyeagizwa hivyo kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo,
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
31
aliyeagizwa hivyo kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo,
atakuwa na mamlaka ya kutekeleza kazi na shughuli hizo kwa
kufuata masharti yoyote yaliyowekwa na Rais, lakini bila ya kujali
masharti ya sheria nyingine yoyote; isipokuwa kwamba-
(a) Rais hatakuwa na mamlaka ya kuwakilisha kwa
Waziri kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo
kazi yoyote ya Rais aliyokabidhiwa na sheria yoyote
inayotokana na masharti ya mkataba wowote uliotiwa
sahihi na Jamhuri ya Muungano iwapo kisheria Rais
haruhusiwi kuwakilisha kazi hiyo kwa mtu mwingine
yoyote;
(b) ifahamike kwamba maagizo yanayotolewa na Rais
kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo, ya
kumwagiza Waziri yeyote kutekeleza kazi yoyote ya
Rais, hayatahesabiwa kwamba yanamzuia Rais
kutekeleza kazi hiyo yeye mwenyewe.
(9) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii-
(a) Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanywa kwa ajili
ya kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio kuhusu hali ya
afya ya Rais utahesabiwa kuwa ni mkutano halali
hata kama mjumbe yeyote wa Baraza hilo hayupo au
kiti chake ki wazi, na itahesabiwa kuwa Baraza
limepitisha azimio hilo ikiwa litaungwa mkono kwa
kauli ya wajumbe walio wengi waliohudhuria mkutano
na kupiga kura.
(b) Rais hatahesabiwa kuwa hayupo katika Jamhuri ya
Muungano kwa sababu tu ya kupitia nje ya Tanzania
wakati yuko safarini kutoka sehemu moja ya
Tanzania kwenda sehemu nyingine, au kwa sababu
kwamba ametoa maagizo kwa mujibu wa masharti ya
ibara ndogo ya (7) na maagizo hayo bado
hayajabatilishwa.
(10) Bila ya kujali masharti yaliyoelezwa hapo awali katika
ibara hii, mtu atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais, kwa
mujibu wa ibara hii hatakuwa na madaraka ya kulivunja Bunge,
kumwondoa yeyote kati ya Mawaziri katika madaraka yake au
kufuta uteuzi wowote uliofanywa na Rais.
(11) Mtu yeyote atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais
kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kama ni Mbunge hatapoteza
kiti chake katika Bunge wala hatapoteza sifa zake za
kuchaguliwa kuwa Mbunge kwa sababu tu ya kutekeleza kazi na
shughuli za Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
Uchaguzi wa
Rais Sheria ya
1984 Na.15 ib.9
38.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria itakayoweka
masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
32
kwa kufuata masharti ya Katiba hii.
Sheria ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria ya 1994
Na.34 ib.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha
Rais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi
hiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri
itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo
yafuatayo:-
(a) baada ya Bunge kuvunjwa;
(b) baada ya Rais kujiuzulu bila ya kulivunja Bunge
kwanza:
(c) baada ya Rais kupoteza sifa za kushika nafasi
madaraka ya kuchaguliwa;
(d) baada ya Rais kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa
Katiba hii, na kuondolewa katika madaraka;
(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37 ya Katiba hii kwamba Rais hawezi
kumudu kazi na shughuli zake;
(f) baada ya Rais kufariki.
(3) Kiti cha Rais hakitahesabiwa kuwa kiwazi kwa sababu tu
ya Bunge kupitisha hoja ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu.
Sifa za mtu
kuchaguliwa wa
kuwa Rais
Sheria ya 1992
Na.4
Sheria ya 1994
Na.13 ib…
Sheria ya 1994
Na.34 ib….
Sheria ya 2000
Na.3 ib.7
39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
kodi yoyote ya Serikali.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
33
(2) Bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoni
yake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine na kushiriki
shughuli za umma kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyote
hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano kama si mwananchama na mgombea
aliyependekezwa na chama cha siasa.
Haki ya
kuchaguliwa
tena
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria Na.34 ya
1994 ib.9
40.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena
kushika kiti hicho.
(2) Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika
kiti cha Rais.
(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar hatapoteza sifa za
kuweza kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa
sababu tu kwamba aliwahi kushika madaraka ya Rais Za nzibar.
(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa
mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua
miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,
lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au
zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Utaratibu wa
uchaguzi wa
Rais Sheria
Na.20 ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria Na.34
ya 1994
Na.34 ib.10
41.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jingine
lolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 na
inalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasa
kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha
kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la
mwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombea
katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la
mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi
ya Makamu wa Rais.
(2) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi
wa Rais yatawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi katika siku na
saa itakayotajwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na
mtu hatakuwa amependekezwa kwa halali isipokuwa tu kama
kupendekezwa kwake kunaungwa mkono na wananchi wapiga
kura kwa idadi na kwa namna itakayotajwa na sheria iliyotungwa
na Bunge.
(3) Endapo inapofika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya
kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea
mmoja tu ambaye anapendekezwa kwa halali, Tume itawasilisha
jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au
kumkataa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii na ya sheria
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
34
iliyotungwa na Bunge.
(4) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanywa
siku itakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria
iliyotungwa na Bunge.
(5) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa
Rais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo.
(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.
Wakati na muda
wa kushika
madaraka ya
Rais
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
42.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema
iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa
kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla
ya kupita siku saba.
(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu
aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika
ibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka
mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.
(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti
hicho atakula kiapo cha Rais; au
(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka;
au
(c) siku atakapojiuzulu; au
(d) atakapoacha kushika kiti cha Rais kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii.
(4) Iwapo Jamhuri ya Muungano inapigana vita dhidi ya adui
na Rais anaona kuwa haiwezekani kufanya uchaguzi, Bunge
laweza mara kwa mara kupitisha azimio la kuongeza muda wa
miaka mitano uliotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii
isipokuwa kwamba muda wowote utakaoongezwa kila mara
hautazidi miezi sita.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
35
(5) Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais,
kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine
chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Masharti ya kazi
ya Rais
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
43.-(1) Rais atalipwa mshahara na malipo meingineyo, na
atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au
posho, kadri itakavyoamuliwa na Bunge, na mshahara, malipo
hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho,
vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya
ibara hii.
(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais
havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Madaraka ya
kutangaza vita
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 1992
Na.4 ib.14
44.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa hali
ya vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote.
(2) Baada ya kutoa tangazo, Rais atapeleka nakala ya
tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya
kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndani
ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha
mkutano wa Bunge ili kutafakari hali ya mambo na kufikiria
kupitisha au kutopitisha azimio la kuunga mkono tangazo la vita
lililotolewa na Rais.
Uwezo wa
kutoa msamaha
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
45.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na
hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza
kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa
masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu
yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa
lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au
asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote
kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
36
aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au
kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza,
au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia
ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano.
(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka
utaratibu utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madaraka
yake kwa mujibu wa ibara hii.
(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwa
na kuadhibiwa Tanzania Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa
Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge
inayotumika Tanzania Zanzibar, hali kadhalika, masharti hayo
yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania
Bara kwa mujibu wa sheria.
Kinga dhidi ya
mashataka ya
na madai
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 1992
Na.20 ib…
46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku
kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake
mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka
yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua
mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa
kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au
baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku
thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais
atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi
kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo
kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina
lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa
analodai.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
kwa mujibu wa Katiba hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
37
Bunge laweza
kumshtaki Rais
Sheria ya 1992
Na.20 ib.8
Sheria ya 1995
Na.12 ib.4
46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-
Sheria ya …. (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili
yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais
wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya
namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja
kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu
kama-
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku
thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo
inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa
aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati
Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze
mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa
iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa
masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja
yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja
kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka
Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya
hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na
kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua
theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara
hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye
atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
38
(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa
Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama vya siasa
vinavyowakilishwa Bungeni.
(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum
ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi
na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais
juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa
dhidi yake.
(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi
kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya
Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda
usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa
yake kwa Spika.
(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya
Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi
kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili
taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura
za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote,
Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais
yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha
Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.
(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya
Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti
cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika
kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge
lilipopitisha azimio hilo.
(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na
mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata
malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo
alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
39
Wajibu wa
viongozi wakuu
wa vyombo vya
mamlaka ya
utendaji
kudumisha
Muungano
Sheria ya 1995
Na.12 ib.5
46B.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia uliotajwa katika
ibara ya 28 ya Katiba hii, viongozi wakuu wa vyombo vyenye
mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano vilivyotajwa
katika, ibara ya 4 ya Katiba hii, watawajibika, kila mmoja wao
katika kutekeleza madaraka aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii
au Katiba ya Zanzibar, 1984, kuhakikisha kuwa analinda
kuimarisha na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1), kila
mmojwawapo wa viongozi wakuu wa vyombo vyenye mamlaka
ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano kabla ya kushika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii ataapa kuitetea na
kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii.
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya ibara hii:-
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Zanzibar, na
(d) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
SEHEMU YA PILI
MAKAMU WA RAIS
Mkamu mmoja
wa Rais, kazi
na mamlaka
yake
Sheria ya 1994
Na.34 ib.11
Sheria ya 2000
Na.3 ib.9
47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa
ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya
Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku
hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini
au yuko nje ya nchi.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa
Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa
pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake
wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na
watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais
akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.
(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa
kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano
atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais
atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
40
(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa sheria ya Uraia;
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi;
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
uchaguzi hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama
yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote
ya Serikali.
(5) Chama chochote hakitazuiwa kumpendekeza mtu yeyote
kuwa mgombea kiti cha Makamu wa Rais kwa sababu tu
kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa
Zanzibar au kiti cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
(6) Makamu wa Rais hatakuwa kwa wakati huo huo Mbunge,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, wala Rais wa Zanzibar.
(7) Endapo mtu ambaye ni Waziri Mkuu, au Rais wa Zanzibar
anateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha kiti
cha Waziri Mkuu, au cha Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.
(8) Makamu wa Rais atatekeleza madaraka yake chini ya
uongozi na usimamizi wa Rais, na ataongoza na kuwajibika kwa
Rais kuhusu mambo au shughuli zozote atakazokabidhiwa na
Rais.
Wakati wa
Makamu wa
Rais kushika
madaraka
Sheria ya 1994
Na.34 ibara 11
48.-(1) Makamu wa Rais atashika madaraka ya Makamu wa
Rais siku hiyo hiyo Rais anaposhika madaraka.
(2) Makamu wa Rais aliyeteuliwa kwa mujibu wa ibara ya
50(3) ataapa na kushika madaraka yake baada ya uteuzi wake
kuthibitishwa na Bunge.
Kiapo cha
Makamu wa
Rais.
Sheria
Na.34 ya 1994
ib.11
49. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake
ataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo
cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na
utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
41
Muda wa
Makamu wa
Rais kushika
madaraka.
Sheria ya 1994
Ibara 11. Sheria
ya 1995 Na.12
ibara 6
Sheria ya 2000
Na.3 ib.10
50.-(1) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi,
mtu aliyechaguliwa, au kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 37(5),
kuwa Makamu wa Rais, bila ya kuathiri masharti mengine ya
ibara hii, atashika kiti cha Makamu wa Rais kwa muda wa miaka
mitano tangu alipochaguliwa kuwa Makamu wa Rais.
(2) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi-
(a) muda wake utakapokwisha;
(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka;
(c) atakapojiuzulu;
(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya kiti cha Rais
kuwa wazi;
(e) atakapotiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai
linaloonyesha utovu wake wa uaminifu;
(f) atakapoapishwa Rais mwingine kushika nafasi ya
Rais pamoja na Makamu wake;
(g) atakapoondolewa madarakani baada ya kushtakiwa
Bungeni kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(3) ya ibara hii;
(h) atakapoacha kushika kiti cha Makamu wa Rais
vinginevyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(3) Bunge litakuwa na madaraka ya kumuondoa Makamu wa
Rais madarakani kama yale liliyonayo kuhusiana na Rais,
isipokuwa kwamba hoja yoyote ya kumshtaki Makamu wa Rais
itatolewa tu kama inadaiwa kwamba:-
(a) Rais amewasilisha hati ya Spika inayoeleza kwamba
Makamu wa Rais ameacha au ameshindwa
kutekeleza kazi za Makamu wa Rais;
(b) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(c) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili
yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba; au
(d) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais
wa Jamhuri ya Muungano au kiti cha Makamu wa
Rais,
na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili
tangu hoja hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(4) Ikitokea kwamba kiti cha Makamu wa Rais ki wazi
kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ya 50(3), kifo au
kujiuzulu basi mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote ndani ya
siku zisizozidi kumi na nne baada ya kushika madaraka yake,
Rais atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo
utathibitishwa na Bunge kwa kura za Wabunge walio wengi.
(5) Masharti mengine yote ya ibara ya 46A ya Katiba
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
42
yatatumika pia kuhusiana na Makamu wa Rais isipokuwa tu
kwamba Makamu wa Rais aliyeondolewa tena madarakani chini
ya ibara ndogo ya (3) hatakuwa na sifa tena za kushika nafasi ya
Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wala Rais wa Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
43
SEHEMU YA TATU
WAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI
NA SERIKALI
Waziri Mkuu
Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya
Muungano
Sheria ya
1992 Na.20
ibara 9
51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na
ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais
kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa
na Bunge.
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku
kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua
Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi
anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi
Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge
wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio
wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika
madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa
na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge
walio wengi.
(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri
Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi-
(a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake;
au
(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au
(c) siku atakapojiuzulu; au
(d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa
Waziri Mkuu; au
(e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu
wa masharti mengineyo ya Katiba hii.
Kazi na
mamlaka
ya Waziri
Mkuu Sheria
ya 1984 Na.15
ib.9
52.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,
usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali
Bungeni.
(3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu
atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au
mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
44
Uwajibikaji wa
Serikali
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu
atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli
za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Kura ya
kutokuwa na
imani.
Sheria ya
1992 Na.20
ibara 10
Sheria ya
1995 Na.12
ibara 7
53A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na
Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo na
ikapitishwa kwa mujibuwa wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri
Mkuu haitatolewa Bungeni endapo-
(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri
Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala
hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa;
(c) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo
ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa kuipitisha.
(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
haitapitishwa na Bunge isipokuwa tu kama-
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku angalau kumi
na nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa
Bungeni;
(b) Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili
ya kuleta hoja yametimizwa.
(4) Hoja iliyotimiza masharti ya ibara hii itawasilishwa Bungeni
mapema iwezekanavyo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.
(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu
iwapo inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.
(6) Endapo hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri
Mkuu itaungwa mkono na Wabunge wengi, Spika atawasilisha
azimio hilo kwa Rais, na mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote
vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha azimio la hoja ya
kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu
atatakiwa ajiuzulu, na Rais atamteua Mbunge mwingine kuwa
Waziri Mkuu.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
45
Baraza la Mawaziri na Serikali
Baraza la
Mawaziri
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
Sheria Na.4
ya 1992 ib…
Sheria Na.34
ya 1994 ibara
12
54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe
wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa
Zanzibar na Mawaziri wote.
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye
atkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi
mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili
Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza
Mikutano hiyo.
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya
Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha
kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji
wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na
litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote
litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo
maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.
(4) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria mikutano yote
ya Baraza la Mawaziri na atakuwa na haki zote za mjumbe wa
mikutano hiyo isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura katika
mikutano hiyo.
(5) Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa
na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika
mahakama yoyote.
Uteuzi wa
Mawaziri
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
55.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la
Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada
ya kushauriana na Waziri Mkuu.
(2) Pamoja na Mawaziri waliotanjwa katika ibara ndogo ya (1),
Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua
Naibu Mawaziri. Naibu Mawaziri wote hawatakuwa wajumbe wa
Baraza la Mawaziri.
(3) Rais aweza kuteua idadi yoyote ya Naibu Mawaziri ambao
watawasaidia Mawaziri katika utekelezaji wa kazi na shughuli zao.
(4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka
miongoni mwa Wabunge.
(5) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ikitokea
kwamba Rais anahitajiwa kumteua Waziri au Naibu Waziri baada
ya Bunge kuvunjwa, basi aweza kumteua mtu yeyote ambaye
alikiwa Mbunge kabla ya Bunge kuvunjwa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
46
Kiapo cha
Mawaziri na
Naibu
Mawaziri
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
56. Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka
awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia
kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Mawaziri
kushika
madaraka
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
57.-(1) Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziri
utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.
(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lo
lote kati ya mambo yafuatayo:-
Sheria ya
1992 Na.20
ibara 9
(a) endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufariki
dunia;
Sheria ya
1992 Na.20
ibara 11
(b) ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge
kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa
Bunge;
Sheria ya
1995 Na.12
ibara 8
(c) ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini
mwenye madaraka hayo;
(d) iwapo atachaguliwa kuwa Spika;
(e) iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi
kwa sababu nyingine yoyote;
(f) ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya
Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika
madaraka hayo;
(g) iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha
kwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma.
Masharti ya
kazi
ya Mawaziri
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
58. Mawaziri na Naibu Mawaziri watashika madaraka yao kwa
ridhaa ya Rais, na watalipwa mshahara, posho na malipo
mengineyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
47
Mwanasheria
Mkuu wa
Serikali ya
Jamhuri ya
Muungano
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
Sheria ya
1992
Na.4 ibara 16
59.-(1) Kutakuwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano ambaye katika ibara zifuatazo za Katiba hii
atatajwa tu kwa kifupi kama "Mwanasheria Mkuu" ambaye
atateuliwa na Rais.
(2) Mtu yeyote hatastahili kuteuliwa kushika madaraka ya
Mwanasheria Mkuu isipokuwa tu kama kwa mujibu wa Katiba hii
ana sifa maalum, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ya 109(8)
zinazomwezesha kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya
Jamhuri ya Muungano au Jaji wa Mahakam Kuu ya Zanzibar, na
amekuwa na mojawapo ya hizo sifa maalum kwa muda
usiopungua miaka mitano.
(3) Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo,
atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli
nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria
zitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza,
na pia kutekeleza kazi au shughuli nyinginezo zilizokabidhiwa
kwake na Katiba hii au na sheria yoyote.
(4) Katika kutekeleza kazi na shughuli zake kwa mujibu wa
ibara hii, Mwanasheria Mkuu atakuwa na haki ya kuhudhuria na
kusikilizwa katika Mahakama zote katika Jamhuri ya Muungano.
(5) Mwanasheria Mkuu atakuwa Mbunge kutokana na wadhifa
wake, na atashika madaraka yake mpaka-
(a) uteuzi wake utakapofutwa na Rais au
(b) mara tu kabla ya Rais mteule kushika madaraka ya
Rais, na atalipwa mshahara, posho na malipo
mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katibu wa
Baraza
la Mawaziri
sheria ya 1984
Na.15
ib. 9
60. Kutakuwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri ambaye
atakuwa ndiye mtendaji mkuu katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri,
na atatekeleza shughuli zifuatazo kwa kufuata maagizo ya jumla
au maalum atakayopewa na Rais, yaani:
(a) kuanda ratiba ya mikutano ya Baraza na kutayarisha
orodha ya shughuli za kila mkutano;
(b) kuandika na kuweka kumbukumbu za mikutano ya
Baraza;
(c) kutoa taarifa na maelezo ya maamuzi ya Baraza kwa
kila mtu au chombo cha umma kinachohusika na
uamuzi wowote; na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
48
(d) kutekeleza kazi na shughuli nyingine zozote
atakazoagizwa mara kwa mara na Rais.
Wakuu wa
Mikoa Sheria
ya 1984 Na.15
ib.9
61.-(1) Kutakuwa na Mkuu wa Mkoa kwa kila mkoa katika
Jamhuri ya Muungano ambaye, bila ya kuathiri ibara ndogo ya (3),
atakuwa ni kiongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Bara watateuliwa na
Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.
(3) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Zanzibar watateuliwa na
Rais wa Zanzibar baada ya kushauriana na Rais.
(4) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (5), kila Mkuu
wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na
shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa
aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote
zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au
shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote
yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
(5) Pamoja na wajibu na madaraka yake yaliyotajwa kwenye
masharti yaliyotangulia ya ibara hii, Mkuu wa Mkoa kwa mkoa
wowote katika Tanzania Zanzibar atatekeleza kazi za shughuli za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atakazokabidhiwa na Rais wa
Zanzibar, na kwa mujibu wa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar 1984 au sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi.
SURA YA TATU
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
BUNGE
Bunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.12
62.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo
litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.
(2) Bunge litakuwa na wajumbe wa aina zote zilizotajwa katika
ibara ya 66 ya Katiba hii ambao wote wataitwa Wabunge.
(3) Iwapo jambo lolote lahitaji kuamuliwa au kutekelezwa na
sehemu zote mbili za Bunge kwa mujibu wa masharti ya Katika hii
au masharti ya sheria nyingine yoyote, basi jambo hilo
halitahesabiwa kuwa limeamuliwa au limetekelezwa ipasavyo ila
mpaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na Wabunge na vile
vile na Rais, kwa mujibu wa madaraka yao kuhusu jambo hilo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
49
Madaraka ya
Bunge Sheria
ya 1984 Na.15
ib.12
Sheria ya
1992
Na.4 ib.17
Sheria ya
1992
Na.20 ib.11
63.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza
madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.
(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha
Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa
niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri
ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa
majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge
laweza-
(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu
mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano
ambayo yako katika wajibu wake;
(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano
wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda
mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa
katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya
kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji
kuwapo sheria;
(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri
ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji
kuridhiwa.
Madaraka ya
kutunga
Sheria Sheria
ya 1984 Na.12
ib.12
64.-(1) Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo
mengine yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuw mikononi mwa
Bunge.
(2) Mamlaka yoyote ya kutunga sheria katika Tanzania
Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano
yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi.
(3) Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi
inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini
ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka na
pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo
lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi,
sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka.
(4) Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kuhusu jambo lo lote
haitatumika Tanzania Zanzibar ila kwa mujibu wa masharti
yafuatayo-
(a) sheria hiyo iwe imetamka wazi kwamba itatumika
Tanzania Bara na vile vile Tanzania Zanzibar au iwe
inabadilisha, kurekebisha au kufuta sheria inayotuka
Tanzania Zanzibar; au
(b) sheria hiyo iwe inabadilisha au kurekebisha au kufuta
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
50
sheria iliyokuwa inatumika tangu zamani Tanzania
Bara ambayo ilikuwa inatumika pia Tanzania Zanzibar
kwa mujibu wa Mapatano ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar, ya mwaka 1964 au kwa
mujibu wa Sheria yoyote ambayo ilitamka wazi
kwamba itatumika Tanzania Bara na vile vile Tanzania
Zanzibar; au
(c) Sheria hiyo iwe inahusu mambo ya Muungano, na kila
inapotajwa Tanzania katika Sheria yoyote ifahamike
kuwa sheria hiyo itatumika katika Jamhuri ya
Muungano kwa mujibu wa Ufafanuzi uliotolewa na
masharti ya ibara hii.
(5) Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwa
mujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Tanzania Zanzibar
yasiyo Mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya
sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria
nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii,
Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi
inachokiuka Katiba itakuwa batili.
Muda wa
Bunge Sheria
ya 1984 Na.15
ib.12
65.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,
maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano.
(2) Kwa madhumuni ya Katiba hii maneno "maisha ya Bunge"
maana yake ni ule muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge
jipya limeitishwa kukutana kwa mara ya kwanza baada ya
Uchaguzi Mkuu na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa
ajili ya kuwezesha Uchaguzi Mkuu mwingine wa kawaida
kufanyika.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
51
SEHEMU YA PILI
WABUNGE, WILAYA YA UCHAGUZI NA
UCHAGUZI WA WABUNGE
Wajumbe wa Bunge
Wabunge
Sheria ya
1984 Na.15
Ibara 13
sheria ya 1992
Na.4 Sheria
1992 Na.4
Ibara 18
Sheria ya
1995 Na.12
Ibara 9
Sheria ya
2000
Na.3 ib.11
66.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa
na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya
uchaguzi;
(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia
asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya
(a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume
ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti
la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais,
watakaochaguliwa na vyama vya siasa
vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya
78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama hivyo;
(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la
Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;
(d) Mwanasheria Mkuu;
(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka
miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara
ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya
67(1)(b).
(2) Rais na Makamu wa Rais kila mmojawao hatakuwa
Mbunge.
(3) Endapo Mkuu wa Mkoa atachaguliwa kuwa Mbunge
anayewakilisha wilaya ya uchaguzi au endapo Mbunge
anayewakilisha wilaya ya uchaguzi atateuliwa kuwa Mkuu wa
Mkoa, Bunge litahesabiwa kuwa lina idadi ya Wabunge
inayohitajika na shughuli zake zitakuwa halali ingawaje idadi ya
jumla ya kawaida ya Wabunge kwa mujibu wa masharti ya ibara
hii, itakuwa imepungua kutokana na uchaguzi huo wa Mkuu wa
Mkoa au uteuzi huo wa Mbunge anayewakilisha wilaya ya
uchaguzi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
52
Sifa za mtu
kuwa Mbunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
Sheria ya
1992 Na.4
ib.19 Sheria
ya 1994 Na.34
ib.13 Sheria
ya 1995 Na.12
ib.10
Sheria ya
2000
Na.3 ib.12
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu
yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa
miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na
kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama
yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote
ya Serikali.
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge-
(a) ikiwa mtu huyo anao au kwa hiari yake amejipatia
uraia wa nchi nyingine yote; au
(b) ikiwa kwa mujibu wa sheria inayotumika katika
Jamhuri ya Muungano imethibitishwa rasmi kwamba
mtu huyo ana ugonjwa wa akili; au
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote
katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya
kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi
miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote,
vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa
uaminifu; au
(d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe
ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa
adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu
wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili ya
Viongozi wa Umma;
(e) bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoni
yake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine
na kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa sheria
za nchi, ikiwa mtu huyo si mwanachama na mgombea
aliyependekezwa na chama cha siasa;
(f) ikiwa mtu huyo ana masilahi yoyote katika mkataba wa
Serikali wa aina yoyote aliyowekewa miiko maalum
kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na iwapo
amekiuka miiko hiyo;
(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa
mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza
au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa
Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
(h) ikiwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
53
inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguzi
wa aina yoyote mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha
kama mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi wa
Wabunge.
(3) Mtu hataweza kugombea uchaguzi kuwa Mbunge wa
kuwakilisha jimbo la uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu wowote ikiwa
wakati huo yeye amesimama katika uchaguzi kugombea kiti cha
Rais, wala hataweza kugombea uchaguzi kuwa Mbunge katika
uchaguzi mdogo wowote ikiwa yeye ni Rais.
(4) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti
yatakayomzuia mtu asichaguliwe kuwa Mbuge wa kuwakilisha
jimbo la uchaguzi ikiwa mtu huyo ni mwenye madaraka
yanayohusika na shughuli za kuongoza au kusimamia uchaguzi
wa Wabunge au shughuli za uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili
ya uchaguzi wa Wabungel isipokuwa kwamba Sheria kama hiyo
haiwezi kuweka masharti yatakayomzuia Spika wa Bunge
asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha wilaya ya uchaguzi,
wala masharti yatakayosababisha mtu aliyechaguliwa kuwa Spika
kupoteza kiti hicho cha Spika au kiti chake cha kawaida katika
Bunge.
(5) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti
yatakayomuzia mtu asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha
wilaya ya uchaguzi kwa muda wowote utakaotajwa na Bunge (ili
mradi muda huo usizidi miaka mitano) ikiwa mtu huyo atapatikana
na hatia mbele ya mahakama kwa ajili ya aina yoyote ya makosa
yatakayotajwa katika Sheria hiyo yanayohusika na uchaguzi wa
Wabunge.
(6) Kwa madhumuni ya kutoa fursa ya kukata rufaa kwa
mujibu wa Sheria kwa mtu yeyote aliyethibitishwa rasmi kisheria
kuwa ana ugonjwa wa akili au aliyehukumiwa na kupewa adhabu
ya kifo au ya kufungwa gerezani au aliyepatikana na hatia ya kosa
lolote lililotajwa katika Sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (5) ya
ibara hii, Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka
masharti yatakayoeleza kwamba hiyo hukumu inayopingwa na
mtu huyo haitakuwa na nguvu kwa ajili ya utekelezaji wa masharti
ya ibara ndogo ya (2) au ya (5) ya ibara hii mpaka upite kwanza
muda utakaotajwa katika sheria hiyo.
(7) Kanuni zifuatazo zitatumika kwa ajili ya ufafanuzi wa aya
ya ( c), ya (d) na ya (e) za ibara ndogo ya (2) ya ibara hii, yaani-
(a) ikiwa mtu amepewa adhabu mbili au zaidi za
kufungwa gerezani na imeamuliwa afungwe kwa muda
wa mfululizo, basi adhabu hizo zitahesabiwa kama ni
adhabu mbalimbali iwapo muda uliotajwa katika kila
moja ya adhabu hizo hauzidi miezi sita; lakini iwapo
muda uliotajwa katika adhabu yoyote kati ya adhabu
hizo unazidi miezi sita basi adhabu hizo zote
zitahesabiwa kama ni adhabu moja;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
54
zitahesabiwa kama ni adhabu moja;
(b) ikiwa mtu atapewa adhabu ya kufungwa gerezani
ikifahamika kuwa adhabu hiyo ya kifungo imetolewa
badala ya adhabu ya kutozwa faini au imetolewa kwa
sababu mtu huyo ameshindwa kulipa faini aliyoamriwa
kulipa, basi muda wa kifungo cha namna hiyo
hautahesabiwa.
(8) Katika aya ya (f) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hii
"mkataba wa Serikali" maana yake ni mapatano yoyote ya
mkataba ambayo mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali ya
Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Idara
yoyote ya Serikali hiyo au mtumishi yeyote wa Serikali aliyeshiriki
kwa niaba ya Serikali.
[ibara ndogo ya (9), (10), (11) na ya 12 zimefutwa na Sheria
Na.4 ya 1992 Ib.19 (d)]
(13) Kwa ajili ya ufafanuzi wa maelezo kuhusu sifa za
uchaguzi yaliyomo katika ibara zifuatazo, kila itakapotajwa katika
Katiba hii kwamba utekelezaji wa jambo lolote wahitaji mtu
mwenye sifa za uchaguzi au mtu ambaye hakupoteza sifa za
uchaguzi, basi, isipokuwa kama maelezo yahitajia vinginevyo,
ifahamike kuwa sifa zinazohusika ni zile zinazomwezesha mtu
kuchaguliwa kuwa Mbunge wa kuwakilisha jimbo la uchaguzi
kama ilivyoelezwa katika ibara ndogo ya (a) ya ibara hii.
Kiapo cha
Wabunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
68. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha
uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini
Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa.
Tamko rasmi
la Wabunge
kuhusu
maadili ya
viongozi
Sheria ya
1995 Na.12
ib.11
69.-(1) Kila Mbunge atatakiwa, kabla ya kumalizika siku
thelathini tangu aapishwe kushika madaraka yake kama Mbunge
kuwasilisha kwa Spika nakala mbili za tamko rasmi kwamba
hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d)
ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67.
(2) Tamko rasmi linalotakiwa kuwasilishwa kwa Spika kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii litatolewa kwa kutumia fomu
maalum itakayowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na
Bunge.
(3) Spika atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala moja
ya kila tamko rasmi lililowasilishwa kwake kwa mujibu wa masharti
ya ibara hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
55
(4) Katika ibara hii na katika ibara ya 70 na ya 84 "Kamishna
wa Maadili" maana yake ni Kamishna aliyeteuliwa kuwa kiongozi
wa Sekretariati ya Maadili iliyotajwa katika ibara ya 132 ya Katiba
hii.
Wabunge
kutoa taarifa
ya mali Sheria
ya 1995 Na.12
ib.12
70.-(1) Kila Mbunge atatakiwa kuwasilisha kwa Spika nakala
mbili za taarifa rasmi ya maelezo ya mali yake na kadri
itakavyokuwa, mali ya mke au mume wake. Taarifa itatolewa kwa
kutumia fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa Sheria
iliyotungwa na Bunge na itatolewa mara kwa mara kama
itakavyoagizwa na Sheria hiyo.
(2) Spika atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala moja
ya kila taarifa rasmi iliyowasilishwa kwake kwa mujibu wa masharti
ya ibra hii.
(3) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti
kwa makusudi ya kusimamia hifadhi ya taarifa ya mali
iliyowasilishwa na Mbunge kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, na
kuhakikisha kwamba watu wasioruhusiwa au wasiohusika
hawapati nafasi ya kuona taarifa ya mali wala kujua yaliyomo
katika taarifa ya mali.
Muda wa
Wabunge
kushika
Madaraka
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
Sheria ya
1992
Na.4 ib.22
Sheria ya
1994 Na.34
ib.14
71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake
katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -
(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa
Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au
apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au
kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(b) ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;
(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano
ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(d) ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama
alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa
kuwa Mbunge;
(f) iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa
Makamu wa Rais;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
56
(g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya
mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa
atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa
masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa
mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge,
lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa
jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu
au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika
madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge
litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na
stahili zinazotokana na ubunge wake.
(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti
yatakayomwezesha Mbunge kukata rufaa, kwa mujibu wa sheria
kupinga hukumu ya kuthibitishwa kwake kuwa ni mtu mwenye
ugonjwa wa akili au kupinga adhabu ya kifo au kufungwa
gerezani, au kupinga kupatikana kwake na hatia kwa kosa la aina
iliyotajwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara
ya 67 ya Katiba hii na sheria hiyo yaweza kueleza kwamba hiyo
hukumu iliyopingwa na huyo Mbunge haitatiliwa nguvu kisheria
mpaka umalizike kwanza muda utakaotajwa katika sheria hiyo.
Watu wenye
madaraka
Serikalini
kukoma
utumishi
wanapochagul
iwa Sheria ya
1992
Na.4 ib.23
Sheria ya
1995 Na.12
ib.14
72. Iwapo mtu yeyote mwenye madaraka katika utumishi wa
Serikali, madaraka ya aina iliyotajwa katika ibara ya 67(2)(g)
ataamua:-
(a) kuwa mgombea uchaguzi wa Rais au wa nafasi
nyingine yoyote chini ya Katiba hii;
(b) kugombea uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha
siasa kinyume na masharti ya ajira,
mtu huyo atahesabiwa kuwa utumishi wake umekoma tangu
tarehe yake ya kuwa mgombea uchaguzi au ya kugombea
uongozi katika chama cha siasa.
Masharti ya
kazi
ya Wabunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
73. Wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa
mujibu wa Katiba hii, na watalipwa mshahara, posho na malipo
mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
57
Tume ya Uchaguzi
Masharti ya
kazi
ya Wabunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
Sheria ya
2000
Na.3 ib.14
74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa
na Rais:-
(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya
Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu
anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili
kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama
Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa
na Bunge.
(2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu
anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni
mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
(3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa
Tume ya Uchaguzi yaani-
(a) Waziri au Naibu Waziri;
(b) mtu mwenye madaraka ya aina yoyote iliyotajwa
mahsusi na sheria iliyotunga na Bunge kwamba ni
mwiko kwa mtu mwenye madaraka hayo kuwa
mjumbe wa Tume ya Uchaguzi;
(c) Mbunge, Diwani au mtu mwingine mwenye madaraka
ya aina yaliyotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge
kwa mujibu wa masharti ya aya ya (g) ya ibara ndogo
ya (2) ya ibara ya 67 ya Katiba hii.
(d) Kiongozi wa chama chochote cha siasa.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, Mjumbe
wa Tume ya Uchaguzi atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolote
katika ya mambo yafuatayo-
(a) Ukimalizika muda wa miaka mitano tangu
alipoteuliwa; au
(b) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama
asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya asiweze
kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
(5) Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa
Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi
zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au
kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.
(6) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa niKatiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
58
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura
katika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri
ya Muungano;
(b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa
Rais na Wabunge;
(c) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya
Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya
uchaguzi wa Wabunge;
(d) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura na
uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani;
(e) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa
Sheria iliyotungwa na Bunge.
(7) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake
yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara
huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu
utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu
atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na
kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na
Bunge.
(8) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti
ya kuweka utaratibu wa kusimamia uchaguzi wa Wabunge
wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.
(9) Tume ya Uchaguzi yaweza kutekeleza shughuli zake bila
ya kujali kwamba kuna nafasi miongoni mwa viti vya wajumbe au
kwamba Mjumbe mmojawapo hayupo, lakini kila uamuzi wa Tume
ya Uchaguzi ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi
kati ya Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi.
(10) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka
masharti ya kuweka utaratibu wa kuwateua Wajumbe wa
kusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya
uchaguzi na, bila ya kuathiri masharti ya Sheria kama hiyo au
maagizo ya Tume ya Uchaguzi, madaraka ya Tume ya Uchaguzi
ya kusimamia uchaguzi yaweza kutekelezwa na wajumbe hao.
(11) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii, Tume ya Uchaguzi haitalazimika kufuata
amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali, au
maoni ya chama chochote cha siasa.
(12) Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika
kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(13) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa
Katiba hii, Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano
itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania
Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
59
(14) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi
kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila
mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara
ya 5 ya Katiba hii.
(15) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watu
wanaohusika na uchaguzi ni-
(a) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(c) Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote
wa Tume ya Uchaguzi,
(e) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilaya
zote.
Majimbo ya Uchaguzi
Majimbo ya
uchaguzi
Sheria
ya 1992 Na.4
ib.24
75.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyo katika ibara
hii, Jamhuri ya Muungano itagawanywa katika majimbo ya
uchaguzi kwa idadi na kwa namna itakavyoamuliwa na Tume ya
Uchaguzi baada ya kupata kibali cha Rais.
(2) Bila ya kuathiri sheria yoyote inayotumika kuhusu mambo
hayo, Tume ya Uchaguzi, baada ya kupata kibali cha Rais itakuwa
na mamlaka ya kuweka mipaka ya majimbo ya uchaguzi.
(3) Katika kuweka mipaka ya majimbo ya uchaguzi, Tume ya
Uchaguzi itazingatia ipasavyo upatikanaji wa njia za mawasiliano,
na pia hali ya kijiografia ya eneo linalokusudiwa kugawanywa
katika majimbo ya uchaguzi.
(4) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii na ya sheria yoyote
inayohusika na mgawanyo wa nchi katika majimbo ya uchaguzi,
Tume ya Uchaguzi yaweza mara kwa mara, na angalao kila baada
ya miaka kumi, kuchunguza mgawanyo wa Jamhuri ya Muungano
katika majimbo ya uchaguzi, na yaweza kubadilisha majimbo ya
uchaguzi kama matokeo ya uchunguzi huo au kutokana na
matokeo ya hesabu ya watu wote katika Jamhuri ya Muungano.
(5) Endapo baada ya uchunguzi kufanywa kuhusu mgawanyo
wa Jamhuri ya Muungano katika majimbo ya uchaguzi
kunafanyika mabadiliko katika majimbo ya uchaguzi, au katika
idadi ya Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi au
mabadiliko kwa idadi ya majimbo ya uchaguzi au idadi ya
Wabunge, basi mabadiliko yatakayotokea katika idadi ya
Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi yataanza
kutumika wakati Bunge litakapovunjwa tena baada ya kutokea
mabadiliko hayo ya idadi ya majimbo au idadi ya Wabunge katika
majimbo ya uchaguzi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
60
(6) Bila kujali masharti mengineyo ya ibara hii, hakuna
Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza
jambo lolote lililotendwa na Tume katika utekelezaji wake wa
kugawa Jamhuri ya Muungano katika majimbo ya uchaguzi.
Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge
Uchaguzi
katika
majimbo za
uchaguzi
Sheria
ya 1984 Na.15
ib. 13
Sheria ya
2000
Na.3 ib.15
76.-(1) Kila mara baada ya Bunge kuvunjwa, kutakuwa na
uchaguzi wa Wabunge katika majimbo yote ya uchaguzi.
(2) Hali kadhalika, kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika
jimbo la uchaguzi, ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwa
kuwakilisha jimbo hilo kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote
isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge.
(3) Bila ya kujali masharti ya ibara hii yaliyotangulia, ifahamike
kwamba ikiwa tarehe ya kuvunjwa Bunge imetangazwa au
inafahamika kutokana na matukio yaliyoelezwa katika ibara ndogo
ya (3) ya ibara ya 90, basi uchaguzi wa namna hiyo hautafanywa
katika kipindi chote cha miezi kumi na mbili ya nyuma ikihesabiwa
tangu tarehe hiyo.
Utaratibu wa
uchaguzi wa
wabunge wa
majimbo ya
uchaguzi
Sheria ya
1992
Na.4 ib. 25
77.-(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi
watachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na
vile vile masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa
Katiba hii inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabunge
wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.
(2) Isipokuwa pale ambapo Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii au Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili
hiyo, itaagiza vinginevyo, kutachaguliwa Mbunge mmoja tu katika
jimbo la uchaguzi.
(3) Wagombea uchaguzi katika jimbo la uchaguzi watatakiwa
watimize masharti yafuatayo-
(a) wawe wamependekezwa mmoja mmoja, na chama
cha siasa kinachoshiriki uchaguzi katika jimbo hilo;
(b) wamewasilisha majina yao kwa Tume ya Uchaguzi
kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge au uliofafanuliwa na Tume ya
Uchaguzi kwa mujibu wa sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
61
Utaratibu wa
uchaguzi wa
Wabunge
wanawake
Sheria ya
1992 Na.4
ib.26
Sheria ya
2000
Na.3 ib.16
78.-(1) Kwa madhumuni ya uchaguzi wa Wabunge, Wanawake
waliotajwa katika ibara ya 66(1) (b), vyama vya siasa vilivyoshiriki
uchaguzi, kwa kufuata utaratibu uliowekwa, vitapendekeza kwa
Tume ya Uchaguzi majina ya wanawake kwa kuzingatia masharti
ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vilivyoshinda uchaguzi
katika majimbo na kupata viti Bungeni. Tume ya Uchaguzi
ikiridhika kuwa mtu yeyote aliyependekezwa anazo sifa za kuwa
Mbunge itamtangaza kuwa amechaguliwa kuwa Mbunge, na
masharti ya ibara ya 83 ya Katiba hii yatatumika kuhusu
kuchaguliwa kwa mtu huyo kuwa Mbunge.
(2) Mtu yeyote hataweza kupendekezwa na chama chochote
cha siasa kwa ajili ya uchaguzi kwa mujibu wa ibara hii ila tu iwapo
anazo sifa za kustahili kuchaguliwa zilizotajwa na masharti ya
ibara ya 67 ya Katiba hii.
(3) Majina ya watu waliopendekezwa kwa mujibu wa ibara
ndogo ya (1) na Tume ya Uchaguzi yatatangazwa kama matokeo
ya uchaguzi baada ya Tume ya Uchaguzi kuridhika kwamba
masharti ya Katiba na Sheria yanayohusika yamezingatiwa.
(4) Orodha ya majina ya wagombea wanawake iliyowasilishwa
kwa Tume ya Uchaguzi na kila chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu
ndiyo itakayotumiwa na Tume ya Uchaguzi baada ya kushauriana
na chama kinachohusika, kwa madhumuni ya kujaza nafasi yoyote
ya Mbunge wa aina hii inapotokea wakati wowote katika maisha
ya Bunge.
Utaratibu wa
uchaguzi wa
Wabunge wa
kuchaguliwa
na
79. Baraza la Wawakilishi litaweka utaratibu litakaoufuata kwa
ajili ya kufanya uchaguzi wa Wabunge waliotajwa katika ibara
66(1) ( c) ya Katiba hii.
Baraza la
Wawakilishi
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
80. [Ibara 80 ya Katiba imefutwa na sheria Na.4 ya 1992
Ibara 27].
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
62
Utaratibu wa
kupendekeza
majina ya
wagombea
Uchaguzi wa
Wabunge
wanawake
Sheria
ya 1992 Na.4
ib.29
81. Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Tume ya
Uchaguzi yaweza kuweka masharti yanayofafanua utaratibu
utakaotumiwa na vyama vya siasa kwa ajili ya kuchagua na
kupendekeza majina ya Wabunge wa aina iliyotajwa katika ibara
ya 66(1) (b).
82. [Ibara ya 82 ya Katiba imefutwa na Sheria Na.4 ya
1992 ibara 29.
Uamuzi wa
suala kama
mtu ni Mbunge
Sheria za
1979, Na.14
Ibara 8 1984
Na.15 Ibara 13
1990 Na.14
1992 Na.4
Ibara 30
83.-(1) Kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala -
(a) kama uchaguzi au uteuzi wa mtu yeyote kuwa mbunge
ulikuwa halali au sivyo; au
(b) kama Mbunge amekoma kuwa Mbunge na kiti chake
katika Bunge ki wazi au hapana,
litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuathiri masharti ya
ibara ndogo ya (2) ya ibara hii.
(2) Iwapo Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake
kwa mujibu wa masharti ya ibra ya 41(3) ya Katiba hii
imemtangaza Mbunge yeyote kwamba amechaguliwa kuwa Rais
basi hakuna mahakama wala chombo chochote kingine
kitakachochunguza zaidi suala lolote linalohusu kiti cha Mbunge
huyo kuwa wazi.
(3) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti
kuhusu mambo yafuatayo-
(a) watu wanaoweza kufungua shauri katika Mahakama
Kuu kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala lolote kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii;
(b) sababu na nyakati za kufungua shauri la namna hiyo,
utaratibu wa kufungua shauri na masharti
yanayotakiwa yatimizwe kwa kila shauri kama hilo; na
(c) kutaja mamlaka ya Mahakama Kuu juu ya shauri kama
hilo na kueleza utaratibu wa kuskiliza shauri lenyewe.
(4) Kutakuwa na haki ya kukata rufaa mbele ya Mahakama ya
Rufani ya Tanzania kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya
shauri lolote lililosikilizwa kwa mujibu wa mahsarti ya ibara hii.
SEHEMU YA TATU
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
63
UTARATIBU, MADARAKA NA
HAKI ZA BUNGE
Spika na Naibu wa Spika
Spika na
mamlaka yake
Sheria ya
1984 Na.15
ib.14 Sheria
ya 1992
Na.4 ib.31
Sheria ya
1995 Na.12
ib.15
84.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na
Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au
wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge
na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje
ya Bunge.
(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina
nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa
madhumuni ya ibdara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.
(3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kabla
ya kumaliza siku kumi na tano tangu kuchaguliwa kwake,
kuwasilisha kwa Rais tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za
uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya
(2) ya ibara ya 67. Tamko hilo litatolewa kwa kutumia fomu
maalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge.
(4) Rais atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala moja
ya kila tamko rasmi lililowasilishwa kwake kwa mujibu wa masharti
ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii.
(5) Spika atatakiwa kuwasilisha kwa Rais nakala mbili za
taarifa rasmi ya maelezo ya mali ya huyo Spika na, kadri
itakavyokuwa, mali ya mke au mume wake. Spika atatoa taarifa
hiyo kwa kutumia fomu maalum iliyowekwa kwa ajili hiyo kwa
mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge na atatoa taarifa ya
namna hiyo mara kwa mara kadri itakavyoagiza sheria hiyo.
(6) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) ya ibara ya 70
yatatumika pia, kwa kadri itakavyowezekana, kwa taarifa ya mali
yoyote itakayotolewa na Spika, kwa mujibu wa masharti ya ibara
hii.
(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika
litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -
(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa
Wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwa
sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge;
au
(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama
asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na
sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa
Spika; au
(c) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya
Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa,
lakini masharti ya aya hii yatatumika bila ya kuathiri
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
64
masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara ya 90 ya
Katiba hii; au
(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya
Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na
Wabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili ya
Wabunge wote; au
(e) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais
tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo
(5) ya ibara hii; au
(f) ikiwa mtu huyo atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa
habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria ya
Kanuni ya jinai, kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa
kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara
hii; au
(g) ikiwa mtu huyo atashindwa kuwasilisha kwa Rais
taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo
ya (5) ya ibara hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa
kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliotungwa na
Bunge;
(h) ikiwa itathibitika kuwa mtu huyo amevunja masharti ya
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(8) Hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge
(isipokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao kiti cha
Spika kitakuwa ki wazi.
(9) Mtu yeyote ambaye si Mbunge atakayechaguliwa kuwa
Spika, atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake,
kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu.
Naibu wa
Spika Sheria
ya 1984 Na.15
ib.14
85.-(1) Kutakuwa na Naibu wa Spika wa Bunge ambaye
atachaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwa Wabunge.
(2) Waziri, Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya aina
nyingine yoyote itakayotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa
madhumuni ya ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Naibu wa
Spika.
(3) Wabunge watamchagua Naibu wa Spika nyakati zifuatazo-
(a) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya
Uchaguzi Mkuu au mapema iwezekanavyo baada ya
wakati huo; na
(b) katika kikao cha kwanza cha Bunge baada ya kiti cha
Naibu wa Spika, kuwa wazi kwa sababu yoyote
isiyohusika na Bunge kuvunjwa au mapema
iwezekanavyo baada ya kikao hicho.
(4) Naibu wa Spika, atakoma kuwa Naibu wa Spika na ataacha
kiti cha Naibu wa Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayoKatiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
65
(a) ikiwa mtu huyo atakoma kuwa Mbunge; au
(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo kama
asingekuwa Naibu wa Spika, lingemfanya mtu huyo
asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi
wa Naibu wa Spika; au
(c) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya
Naibu wa spika kwa azimio la Bunge.
Utaratibu wa
kumchagua
Spika na
Naibu wa
Spika
Sheria 1984
Na.15
Ib.14
86.-(1) Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao cha
kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya, na katika kikao
cha kwanza chochote mara baada ya kutokea nafasi katika kiti
cha Spika.
(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu wa Spika wakati wo wote
katika Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya utakaoteuliwa na
Bunge na vile vile katika kikao cha kwanza cha Bunge mara
baada ya kutokea nafasi katika kiti cha Naibu wa Spika.
(3) Uchaguzi wa Spika, na vile vile uchaguzi wa Naibu wa
Spika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
Ofisi ya Bunge
Katibu wa
Bunge Sheria
ya 1984 Na.15
ib.14
87.-(1) Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na
Rais kutoka miongoni mwa watu wenye madaraka ya juu katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Katibu wa Bunge atakuwa ndiye mtendaji mkuu katika Ofisi
ya Bunge na atawajibika kwa utendaji bora wa shughuli za Bunge
kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na ya sheria inayohusika.
Sekretariati ya
Bunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.14
88.-(1) Kutakuwa na Sekretariati ya Bunge itakayokuwa na
nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali kwa idadi
atakayoagiza Rais.
(2) Sekretariati ya Bunge itakuwa na watumishi kwa idadi na
ngazi za utumishi itakavyoamuliwa mara kwa mara na Tume ya
Utumishi inayohusika baada ya kushauriana na Katibu wa Bunge.
(3) Sekretariati ya Bunge chini ya uongozi wa Katibu wa
Bunge itaendeleza kazi na shughuli zote zilizowekwa au
zitakazokuwa ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji bora
wa Bunge na wa Wabunge wa madaraka ya Bunge chini ya Katiba
hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
66
Utaratibu wa Shughuli Bungeni
Kanuni za
kudumu za
Bunge
Sheria ya
1984 Na.14
ib.14
89.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza
kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa
kutekeleza shughuli zake.
(2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hii
zaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuli
za Sekretariati ya Bunge na pia utekelezaji wa Shughuli za Bunge
ndani ya Bunge na zile za Kamati na Kamati ndogo za Bunge.
Kuitishwa kwa
mikutano ya
Bunge na
Kuvunjwa kwa
Bunge
90.-(1) Baada ya Uchaguzi Mkuu Rais ataitisha Mkutano wa
Bunge Jipya ufanyike kabla ya kupita siku saba tangu kutangazwa
matokeo ya huo Uchaguzi Mkuu katika majimbo ya uchaguzi yote
isipokuwa katika majimbo yale ambako uchaguzi umefutwa na
kufanywa upya.
(2) Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati
wowote, isipokuwa tu-
(a) kama Bunge limemaliza muda wa uhai wake kwa
mujibu wa ibara ya 65 ya Katiba hii; au wakati wowote
katika miezi kumi na miwili ya mwisho ya uhai wa
Bunge, isipokuwa tu kama Spika amepokea taarifa
rasmi inayopendekeza kuundwa kwa Kamati Maalum
ya Uchunguzi kwa madhumuni ya kumuondoa Rais
madarakani kwa mujibu wa ibara ya 46A ya Katiba hii;
(b) kama Bunge limekataa kupitisha Bajeti
iliyopendekezwa na Serikali;
(c) kama Bunge limekataa kupitisha Muswada wa sheria
kwa mujibu wa idara ya 97(4) ya Katiba hii;
(d) kama Bunge limekataa kupitisha hoja ambayo ni ya
msingi katika sera za Serikali, na Rais anaona
kwamba njia ya kuendelea kutoka hapo si kumteua
Waziri Mkuu mwingine bali ni kuitisha Uchaguzi Mkuu;
(e) endapo, kutokana na uwiano wa uwakilishi wa Vyama
vya Siasa katika Bunge, Rais anaona kwamba hakuna
uhalali kwa Serikali iliyopo kuendelea kuwapo, na wala
haiwezekani kuunda Serikali mpya.
(3) Muda wa maisha ya Bunge ukimalizika Bunge litahesabiwa
kuwa limevunjwa; isipokuwa kwamba muda huo ukisha wakati
wowote ambapo Jamhuri ya Muungano iko katika vita Bunge
laweza mara kwa mara kuongeza muda huo uliotajwa katika ibara
ya 65 ya Katiba hii kwa muda usiozidi miezi kumi na miwili mara
kwa mara lakini maisha ya Bunge hayawezi kuongezwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara ndogo kwa muda unaozidi miaka
mitano.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
67
(4) Kukitokea hali ya hatari au kama kuna hali ya hatari
ambayo Rais anaona inasababisha kuitisha Mkutano wa Bunge na
iwapo wakati huo Bunge limevunjwa na matokeo ya kura zilizo
nyingi za Uchaguzi Mkuu hayajatangazwa basi Rais aweza kutoa
Taarifa Maalum ya kuitisha Mkutano wa Bunge na kuangiza
kwamba Spika na watu wote waliokuwa Wabunge mara tu kabla
Bunge halijavunjwa wahudhurie Mkutano huo wa Bunge na watu
hao pamoja na huyo Spika, watahesabiwa kuwa ndio Wajumbe
wa Bunge kwa madhumuni ya Mkutano huo na watahesabiwa
hivyo mpaka usiku wa manane wa siku yatakapotangazwa
matokeo ya kura zilizo nyingi za Uchaguzi Mkuu.
Rais aweza
kulihutubia
Bunge Sheria
ya 1984 Na.15
ib.14
91.-(1) Rais atalihurubia Bunge Jipya katika Mkutano wake wa
Kwanza na kulifungua rasmi Bunge hilo.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1); Rais aweza
wakati wowote kulihutubia Bunge au kupeleka kwenye Bunge
taarifa ambayo itasomwa na Waziri.
Mikutano ya
Bunge Sheria
ya 1984 Na.15
ib.14
92.-(1) Bunge litafanywa mikutano yake mahali ambapo ni
desturi kufanya Mikutano hiyo au mahali pengine popote katika
Jamhuri ya Muungano patakapotajwa na Rais kwa ajili hiyo.
(2) Mkutano wa kwanza wa Bunge katika Maisha ya Bunge
utaanza siku ile ambayo Bunge limeitwa kukutana, na kila
Mkutano ufuatao utaanza siku yoytote itakayopangwa na Bunge
lenyewe au siku yoyote itakayopangwa kwa mujubu wa Kanuni za
Bunge.
(3) Rais aweza kuitisha Mkutano wa Bunge wakati wowote.
Uongozi na
Vikao vya
Bunge Sheria
ya 1984 Na.15
ib.14
93. Kila kikao cha Bunge kitaongozwa na mmojwawapo wa
watu wafuatao, yaani-
(a) Spika au;
(b) ikiwa Spika hayupo, Naibu wa Spika, au
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
68
(c) ikiwa Spika na Naibu wa Spika wote hawapo, Mbunge
yeyote aliyechaguliwa na Bunge kwa ajili hiyo, lakini
Waziri, au Naibu Waziri au mtu mwenye madaraka ya
aina yingine yoyote iliyotajwa na Sheria iliyotungwa na
Bunge kwa madhumuni ya ibara hii hataweza
kuchaguliwa kwa mujibu wa mahsarti ya aya hii.
Kiwango cha
vikao vya
Bunge Sheria
ya 1984 Na.15
ib.14
94.-(1) Kiwango cha kila kikao cha Bunge ni nusu ya Wabunge
wote.
(2) Isipokuwa kama imeelezwa vingine katika Katiba hii, kila
swali litakalotolewa kwa ajili ya kupata uamuzi wa Bunge
litaamuliwa kwa kufuata wingi wa kura za Wabunge waliohudhuria
na kupiga kura.
(3) Spika, Naibu wa Spika, au mtu mwingine atakayeongoza
kikao cha Bunge, hatakuwa na kura ya kawaida bali atakuwa na
kura ya uamuzi kukitokea usawa wa kura.
(4) Kanuni za Bunge zaweza kuweka masharti kwamba
Mbunge yeyoyote atakayepiga kura juu ya jambo lolote ambalo
yeye binafsi ana masilahi nalo atahesabiwa kuwa hakupiga kura.
Viti vilivyo
wazi katika
Bunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.14
95. Bunge laweza kutekeleza shughuli wakati wa vikao vyake
bila ya kujali kwamba kuna kiti kilicho wazi miongoni mwa viti vya
Wabunge (iwe kiti hicho kimekuwa wazi tangu Bunge lilipokutana
kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu au kimekuwa wazi
baada ya Mkutano huo wa kwanza) na iwapo katika shughuli hizo
atashiriki mtu yeyote ambaye hana haki ya kushiriki au kama
wakati wa shughuli hizo atakuwapo mtu yeyote ambaye hana haki
ya kuwapo, basi kushiriki kwa mtu huyo au kuwapo kwake
hakutabatilisha shughuli hizo.
Kamati za
Bunge Sheria
ya 1995 Na.12
Ibara 16
96.-(1) Bunge laweza kuunda Kamati za Bunge za namna
mbalimbali kadri litakavyoona infaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa
madaraka yake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
69
(2) Kanuni za Bunge zaweza kufafanua muundo na shughuli
za Kamati za Bunge zitakazoundwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara hii.
Utaratibu wa Kutunga Sheria
Namna ya
kutumia
madaraka ya
kutunga
sheria ya 1984
Na.15 ib.4
97.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
Katiba hii, Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa
kufuata utaratibu wa kujadili na kupitisha Miswada ya Sheria
ambayo hatimaye itabidi ipate kibali cha Rais, na Muswada
hautakuwa Sheria mpaka uwe umepitishwa na Bunge na
kukubaliwa na Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Baada ya Muswada kuwasilishwa kwa Rais kwa ajili ya
kupata kibali chake, Rais aweza kuukubali au kukataa kuukubali,
na iwapo Rais atakataa kuukubali Muswada basi ataurudisha kwa
Bunge pamoja na maelezo ya sababu zake za kukataa kuukubali
Muswada huo.
(3) Baada ya Muswada kurudishwa kwa Bunge kwa mujibu wa
masharti ya ibara hii, hauwezi kupelekwa te na kwa Rais kwa ajili
ya kupata kibali chake kabla kumalizika muda wa miezi sita tangu
uliporudishwa, isipokuwa kama katika hatua yake ya mwisho
kwenye Bunge kabla haujapelekwa tena kwa Rais Muswada huo
umeungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui
theluthi mbili ya Wabunge wote.
(4) Iwapo Muswada umerudishwa kwa Bunge na Rais, halafu
ukaungwa mkono kwenye Bunge na Wabunge ambao idadi yao
haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote kama ilivyoelezwa
katika ibara ndogo ya (3) na kupelekwa kwa Rais kwa ajili ya
kupata kibali chake kwa mara ya pili kabla haujamalizika muda wa
miezi sita tangu uliporudishwa, basi Rais atatakiwa kuukubali
Muswada huo kabla ya kumalizika muda wa siku ishirini na moja
tangu Muswada huo ulipowasilishwa kwake la sivyo basi itabidi
alivunje Bunge.
(5) Masharti yaliyomo katika ibara hii au katika ibara ya 64
ya Katiba hii hayatalizuia Bunge kutunga sheria na kuweka
masharti ambayo yaweza kukabidhi kwa mtu yeyote au kwa idara
yoyote ya Serikali madaraka ya kuweka Kanuni za nguvu ya
kisheria au kuzipa nguvu ya kisheria Kanuni zozote zilizowekwa
na mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
70
Utaratibu wa
kubadilisha
Katiba hii na
baadhi ya
sheria
Sheria ya
1984 Na.15
ib.14
98.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha
masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata Kanuni zifuatazo:-
(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti
yoyote ya Katiba hii (isipokuwa yale yanayohusika na
aya ya (b) ya ibara hii ndogo) au masharti yoyote ya
sheria yoyote iliyotajwa katika Orodha ya Kwanza
kwenye Nyongeza ya Pili utaungwa mkono kwa kura
za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili
ya Wabunge wote;
(b) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti
yoyote ya Katiba hii au masharti yoyote ya Sheria
yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo
yaliyotajwa katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza ya
Pili iliyoko mwishoni wa Katiba hii, utapitishwa tu
iwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge ambao
idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote
kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge
wote kutoka Tanzania Zanzibar.
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo
ya (1) kubadilisha masharti ya Katiba hii au masharti ya sheria
maana yake ifahamike kuwa ni pamoja na kurekebisha au
kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti mengine
badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya masharti
hayo.
Utaratibu wa
kutunga sheria
kuhusu
mambo
ya fedha
Sheria
ya 1984 Na.15
ib.14
99.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo
yanayohusika na ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza
kwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la
Rais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri.
(2) Mambo yanayohusika na ibara hii ni haya yafuatayo:-
(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya lolote kati ya mambo
yafuatayo:-
(i) kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namna
nyingine yoyote isipokuwa kupunguza;
(ii) kuangiza kwamba malipo au matumizi ya
fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali au mfuko wa Serikali
mwingine wowote au kubadilisha kiwango
hicho na namna nyingine yoyte isipokuwa
kupunguza;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
71
(iii) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha
yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali au mfuko wa Serikali
mwingine wowote wakati ikifahamika kwamba
fedha iliyomo katika mifuko hiyo haikupangiwa
itolewe kwa ajili ya malipo au matumizi hayo,
au kuagiza kwamba malipo au matumizi
yanayofanywa kutokana na mifuko hiyo
yaongezwe;
(iv) kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwa
lilipwe kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) hoja au mabadiliko yoyote ya Hoja kwa ajili ya lolote
kati ya mambo yaliyoelezwa katika aya ya (a) ya ibara
hii ndogo.
(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa muswada wowote
uliowasilishwa kwenye Bunge au Hoja yoyote iliyotolewa katika
Bunge na Waziri au Naibu Waziri.
Madaraka na Haki za Bunge
Uhuru wa
majadiliano na
utaratibu wa
shughuli
Sheria ya
1984 Na.15
ib.14
100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na
utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa
na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika
Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.
(2) Bila ya kuahiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine
yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa
shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya
maombi, muswada, hoja au vinginevyo.
Kuhifadhi na
kutilia nguvu
uhuru wa
majadiliano na
wa shughuli
sheria ya 1984
Na.15 ib.14
101. Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka
masharti ya kuwezesha mahakama na sheria kuhifadhi na kutilia
nguvu uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu wa shughuli
katika Bunge ambao kwa mujibu wa ibara ya 100 umedhaminiwa
na Katiba hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
72
SURA YA NNE
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,
BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR
NA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
NA RAIS WA ZANZIBAR
Serikali ya
Mapinduzi ya
Zanzibar na
mamlaka yake
Sheria ya
1980 Na.45
ib.55: na
Sheria ya
1984
Na.15 ib.14:
Sheria ya
1994 Na.34
ib.16
102.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Zanzibar itakayojulikana
kama "Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" ambayo itakuwa na
mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya
Muungano kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii na katika
ibara zifuatazo katika Sura hii ya Katiba hii, Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar itaundwa na itatekeleza madaraka yake kwa mujibu
wa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar, 1984.
Kiongozi wa
Serikali ya
Mapinduzi ya
Zanzibar na
mamlaka yake
Sheria ya
1980 Na.15
ib.14 1994
Na.34 ib.17
103.-(1) Kutakuwa na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ambaye ndiye atakuwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vile vile Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
(2) Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya
kushika madaraka yake ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Zanizibar
kiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na
kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar
kinachohusika na utendaji wa kazi yake, kisha atashika na
kutekeleza madaraka hayo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii
na Katiba ya Zanzibar, 1984.
(3) Pamoja na madaraka yake mengine kiongozi wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ndiye atakayewateua na kuwakabidhi
madaraka Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
73
Uchaguzi wa
kiongozi wa
Serikali ya
Mapinduzi
Zanzibar 1980
Na.1 ib.11 na
1984 Na.15
ib.14 1990
Na.16 ib.2
1992 Na.20
ib.14
104.-(1) Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
atachaguliwa na wananchi katika Tanzania Zanzibar kwa mujibu
wa masharti ya Katiba ya Zanzibar, na kwa kufuata utaratibu
uliowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi la Zanizibar inayohusu uchaguzi kwa ujumla au
uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha
Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kitakuwa ki wazi,
na uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
utafanyika ili kujaza nafasi hiyo kila mara litokeapo lolote kati ya
mambo yafuatayo.
(a) baada ya Baraza la Wawakilishi kuvunjwa;
(b) baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kujiuzulu bila ya kulivunjwa Baraza la
Wawakilishi kwanza;
(c) baada ya kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kupoteza sifa za kushika nafasi ya madaraka
ya kuchaguliwa;
(d) baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kushtakiwa katika Baraza la Wawakilishi kwa
mujibu wa Katiba ya Zanzibar 1984 na kuondolewa
katika madaraka.
(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa Katiba ya
Zanzibar 1984 kwamba Kiongozi wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar hawezi kumudu kazi na
shughuli zake;
(f) baada ya Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kufariki.
SEHEMU YA PILI
BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR
Baraza la
Mapinduzi la
Zanzibar na
kazi zake
105.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar
litakalokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi;
(b) Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(c) Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(d) Wajumbe wengine watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba
ya Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
74
(2) Bila ya kuyaingilia madaraka ya Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi kama kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Baraza la Mapinduzi litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri
Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya mambo yote
yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake ya uongozi na
usimamizi wa shughuli za Serikali ya Zanzibar na pia utekelezaji
wa madaraka yake juu ya shughuli zote za Serikali kuhusu mambo
yote yasiyo mambo ya Muungano, kwa mujibu wa masharti ya
Katiba hii na yale ya Katiba ya Zanizbar.
SEHEMU YA TATU
BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
Baraza la
Wawakilishi
Zanzibar
Madaraka ya
kutunga
Sheria
za Zanzibar
Sheria ya
1980
Na.1 ib.93
106.-(1) Kutakuwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Baraza la Wawakilishi litakuwa na sehemu mbili; sehemu moja
itakuwa ni ya wajumbe wa Baraza hilo waliochaguliwa na
kuteuliwa kwa namna itakavyoelezwa na masharti ya Katiba ya
Zanzibar, ya mwaka 1984, na ambao watajulikana kama wajumbe
Wawakilishi; sehemu nyingine ya Baraza la Wawakilishi itakuwa ni
Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji
wa madaraka yake kwa mujibu wa mahsarti ya Katiba hii na
masharti ya Katiba ya Zanzibar, ya mwaka 1984.
(2) Iwapo kwa mujibu wa mahsarti ya Katiba hii, masharti ya
Katiba ya Zanzibar, ya mwaka 1984, au masharti ya sheria yoyote
iliyowekwa na inayotumika Zanzibar, jambo lolote lahitaji
kuamuliwa au kutekelezwa na sehemu zote mbili za Baraza la
Wawakilishi, basi jambo hilo halitahesabiwa kuwa limeamuliwa na
limetekelezwa ipasavyo ila mpaka liwe limeamuliwa au
limetekelezwa na Wajumbe wawakilishi na vile vile Kiongozi wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanizbar, kwa mujibu wa madaraka yao
kuhusu jambo hilo.
(3) Madaraka yote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya
mambo yote yasiyo Mambo ya Muungano yatakuwa mikononi
mwa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Madaraka ya
Baraza la
Wawakilishi
Sheria ya
1984 Na.15;
ib.20
107.-(1) Rais wa Zanzibar kama sehemu moja ya Baraza
la Wawakilishi la atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na
Katiba hii na pia Katiba ya Zanzaibar kwa ajili hiyo.
(2) Wajumbe wawakilishi kama Baraza la Wawakilishi
watakuwa ndicho chombo kikuu cha Tanzania Zanzibar ambacho
kitakuwa na madaraka kwa lniaba ya wananchi wa Tanzania
Zanzibar, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
75
Zanzibar na vyombo lvyake vyote katika utekelezaji wa majukumu
yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Zanzibar.
(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake
Baraza la Wawakilishi laweza -
(a) kumuuliza Waziri yeyote wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar swali lolote kuhusu mambo ya umma katika
Tanzania Zanzibar yaliyomo katika wajibu wake;
(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa Mkutano wa Baraza
la wawakilishi wa kila mwaka wa bajeti;
(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu
au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa
Tanzania Zanzibar, na kutnga Sheria ya kusimamia
utekelezaji wa mpango huo;
(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji
kuwapo sheria;
(e) kutayarisha au kuagiza itayarishwe na kuwasilisha
kwenye Chama taarifa kuhusu jambo lolote ambalo liko
chini ya mamlaka ya Bunge.
SURA YA TANO
UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO,
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO,
TUME YA KUAJIRI YA MAHAKAMA YA TANZANIA
BARA, MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR,
MAHAKAMA YA RUFANI YA JAMHURI YA
MUUNGANO NA MAHAKAMA MAALUM
YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KKWANZA
UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO
Mamlaka ya
utoaji haki
Sheria ya
2000
Na.3 ib.17
107A.-(1) Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano
itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya
Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Seriikali
wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar
kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.
(2) Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa
kuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo, yaani:
(a) kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
76
au kiuchumi;
(b) kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;
(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana
na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria
mahususi iliyotungwa na Bunge;
(d) kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya
wanaohusika katika migogoro;
Uhuru wa
Mahakama
Sheria ya
2000
Na.3 ib.17
107B. Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakama
zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya
Katiba na yale ya sheria za nchi.
Mahakama
Kuu
ya Jamhuri ya
Muungano na
mamlaka yake
Sheria ya
1979 Na.14
ib.6
SEHEMU YA PILI
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO
108.-(1) Kutakuwa na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano
(itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama Kuu") ambayo
mamlaka yake yatakuwa kama ilivyoelezwa katika Katiba hii au
katika sheria nyingine yoyote.
(2) Iwapo Katiba hii au sheria nyingine yoyote haikutamka wazi
kwamba shauri la aina iliyotajwa mahususi litasikilizwa kwanza
katika Mahakama ya ngazi iliyotajwa mahsusi kwa ajili hiyo, basi
Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kila shauri la
aina hiyo. Hali kadhalika Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa
kutekeleza shughuli yoyote ambayo kwa mujibu wa mila za
kisheria zinazotumika Tanzania shughuli ya aina hiyo kwa
kawaida hutekelezwa na Mahakama Kuu.
Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila
ya kuathiri mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kama
ilivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.
Majaji wa
Mahakama
Kuu
na uteuzi wao
Sheria ya
1979 Na.14
ib.6 1985
Sheria ya
1985 Na.15
ib.22
Sheria ya
1990 Na.14
ib.5
109.-(1) Kutakuwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu
(ambaye katika ibara zifuatzo kwenye Katiba Hii atatajwa tu kwa
kifupi kama "Jaji Kiongozi") na Majaji wengine wa Mahakama Kuu
wasiopungua kumi na watano.
(2) Jaji Kiongozi na Majaji wengineo wa Mahakama Kuu
watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya
Mahakama.
(3) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine
yoyote kuhusu madaraka ya Jaji Mkuu aliyetajwa katika
ibara ya 118, Jaji Kiongozi atakuwa ndiye msaidizi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
77
ibara ya 118, Jaji Kiongozi atakuwa ndiye msaidizi
maalum wa Jaji Mkuu katika utendaji wa kazi katika
Mahakama Kuu na Mahakama nyinginezo zote za ngazi
ya chini yake, na katika madaraka hayo Jaji Kiongozi
atatekeleza kazi na shughuli atakazoagizwa au
kuelekezwa mara kwa mara na Jaji Mkuu, na kwa
madhumuni ya ibara hii, Jaji Kiongozi atajulikana pia
kama Mkuu wa Mahakama Kuu.
(4) Mbali ya madaraka yake ya kawaida ya Jaji wa Mahakama
Kuu kama Majaji wengine wote wa Mahakama Kuu, Jaji Kiongozi
atakuwa pia na mamlaka ya kutekeleza kazi na shughuli zote
zinazoambatana na mamlaka ya Mahakama Kuu ambazo kwa
mujibu wa masharti ya Katiba hii au ya sheria nyingine yoyote au
kufuatana na mila za kisheria zinazotumika hutakiwa zitekelezwe
na Mkuu wa Mahakama Kuu:
Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo hayatatumika
kwa ajili ya utekelezaji wa kazi au shughuli ambazo kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii au ya Sheria nyingine yoyote au kufuatana
na mila za kisheria zinazotumika Tanzania zimetajwa mahususi au
zinafahamika kuwa ni kazi au shughuli zinazotakiwa kutekelezwa
tu na Jaji Mkuu.
(5) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi au
utekelezaji wa masharti ya ibara ndogo ya (3) na ya (4) ya ibara
hii, inatamkwa rasmi hapa kwamba isipokuwa kama masharti ya
Katiba hii au ya sheria nyingine yoyote yameagiza vingine, Jaji
Mkuu atakuwa na uwezo wa kutoa kwa Jaji Kiongozi mara kwa
mara maagizo au maelekezo kuhusu utendaji wa kazi na shughuli
zake kama Mkuu wa Mahakama Kuu: vile vile, Jaji Mkuu atakuwa
na uwezo wa kuwakilisha kwa Jaji Kiongozi baadhi ya madaraka
yake ya uongozi na usimamizi juu ya utekelezaji wa kazi katika
Mahakama Kuu na Mahakama nyinginezo zote za ngazi ya chini
yake, na kila inapohitajika, Jaji Mkuu anaweza kutekeleza yeye
mwenyewe moja kwa moja madaraka yake yoyote aliyowakilisha
kwa Jaji Kiongozi.
(6) Kazi ya Jaji wa Mahakama Kuu haitafutwa wakati yupo mtu
aliyeshika madaraka ya kiti cha Jaji.
(7) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (9) ya ibara hii,
mtu aweza tu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa ana
sifa maalum, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (8) ya
ibara hii, na awe mtu ambaye amekuwa na mojawapo ya sifa
maalum kwa muda usiopungua miaka mitano.
(8) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara ndogo ya (7), ya (9)
na ya (11) ya ibara hii, "sifa maalum" maana yake ni sifa
zilizotajwa katika Sheria ya Mawakili (au Sheria nyingine yoyote
inayobadilisha hiyo sheria ya Mawakili au inayotumika badala
yake) ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo ili
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
78
yake) ambazo ni lazima mtu awe nazo mojawapo ya sifa hizo ili
aweze kukubaliwa kuandikishwa kama Wakili Tanzania Bara.
(9) Iwapo Rais atatosheka kwamba ijapokuwa mtu mwenye
sifa mojawapo ya hizo sifa maalum hakuwa nayo sifa hiyo kwa
muda usiopungua miaka mitano, lakini mtu huyo ana uwezo, ujuzi
na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa
Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili
kukabidhiwa madaraka hayo, basi Rais aweza kutangua lile sharti
la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano, na
baada ya kushauriana na Tume ya Kuajiri ya Mahakama, Rais
aweza kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
(10) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji Kiongozi kitakuwa wazi au
kwamba Jaji Kiongozi atashindwa kutekeleza kazi zake kwa
sababu yoyote, basi kazi hizo zitatekelezwa na Jaji mmojwapo
atakayeteuliwa na Rais kwa ajili hiyo, na na Jaji huyo atatekeleza
kazi hizo mpaka atakapoteuliwa Jaji Kiongozi mwingine na
kushika madaraka ya kiti cha Jaji Kiongozi au mpaka Jaji Kiongozi
mwenyewe ambaye alikuwa hamudu kazi zake atakaporejea
kazini.
(11) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji yeyote kitakuwa wazi au
ikiwa Jaji yeyote atateuliwa kuwa Kaimu Jaji Kiongozi au kama
atashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, au kama
Jaji Mkuu atamshauri Rais kuwa kazi za Mahakama Kuu zilivyo
wakati huo zahitaji ateuliwe Kaimu Jaji, basi Rais aweza, baada ya
kushauriana na Jaji Mkuu kama kawaida, kuteua Kaimu Jaji
kutoka miongoni mwa watu wenye sifa maalum.
Isipokuwa kwamba
(a) mtu hatahesabiwa kuwa hastahili kuteuliwa kwa mujibu
wa masharti ya ibara hii ndogo kwa sababu tu kwamba
ametimiza umri uliotajwa katika ibara ndogo ya (1) ya
ibara ya 61 ya Katiba hii;
(b) kwa madhumuni ya kumteua Kaimu Jaji kwa mujibu wa
masharti ya ibara hii ndogo, Rais aweza kutangua lile
sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua
miaka mitano kwa sababu kama zile zilizotajwa katika
ibara ndogo ya (9) ya ibara hii.
(12) Mtu yeyote atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji kwa mujibu
wa masharti ya ibara ndogo ya (11) ya ibara hii, ataendelea
kufanya kazi kama Kaimu Jaji kwa muda wowote utakaotajwa
wakati wa kuteuliwa kwake au, kama muda haukutajwa, mpaka
uteuzi wake utakapofutwa na Rais, lakini bila ya kujali kwamba
muda wake wa kazi umemalizika au kwamba uteuzi wake
umefutwa, mtu huyo aweza kuendelea kufanya kazi kama Kaimu
Jaji mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka
akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
79
ambayo alikwisha anza kuyasiliza kabla ya muda wake wa kazi
haujamalizika au kabla ya uteuzi wake haujafutwa.
Muda wa
Majaji
wa Mahakama
Kuu kushika
madaraka
Sheria ya
1979 Na.14
ib.6: na
Sheria ya
1985
Na.15 ib.22 na
23
Sheria ya
1995 Na.12
ib.17
110.-(1) Kila Jaji wa Mahakama Kuu atalazimika kuacha kazi
yake atakapotimiza umri wa miaka sitini lakini masharti ya ibara hii
ndogo yatatumika bila ya kuathiri masharti yafuatayo katika ibara
hii.
(2) Jaji yeyote wa Mahakama Kuu aweza kujiuzulu kazi katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wakati wowote
baada ya kutimia umri wa miaka hamsini na tano, isipokuwa kama
Rais ataagiza kwamba asijiuzulu, na iwapo Rais ataagiza hivyo,
basi huyo Jaji atakayehusika na maagizo hayo ya Rais hatakuwa
na haki ya kujiuzulu mpaka upite kwanza muda wowote
utakaotajwa na Rais kwa ajili hiyo.
(3) Iwapo Rais ataona kuwa kwa ajili ya manufaa ya Umma
inafaa Jaji aliyetimiza umri wa miaka sitini aendelee kufanya kazi,
na huyo Jaji mwenyewe anakubali kwa maandishi kuendelea
kufanya kazi, basi Rais aweza kuagiza kuwa Jaji huyo aendelee
kufanya kazi kwa muda wowote utakaotajwa na Rais.
(4) Bila ya kujali kwamba Jaji ametimiza umri ambao
analazimika kuacha kazi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, mtu
anayefanya kazi ya Jaji wa Mahakama Kuu aweza kuendelea
kufanya kazi baada ya kutimiza umri huo mpaka amalize
kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe shughuli
nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwisha anza
kuyasikiliza kabla hajatimiza umri huo wa kuacha kazi.
(5) Jaji wa Mahakama Kuu aweza tu kuondolewa katika
madaraka ya kazi ya kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi
yake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au
kwa sababu ya tabia mbaya inayoathiri maadili ya kazi ya Jaji au
sheria ya maadili ya viongozi wa umma; na hataweza kuondolewa
kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (7) ya ibara
hii.
(6) Iwapo Rais anaona kuwa suala la kumwondoa Jaji kazini
lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa
ifuatavyo:-
(a) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na
Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Na huyo
Mwenyekiti na angalau nusu ya Wajumbe wengine wa
Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji wa
Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi
yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola.
(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa
kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lolote na
itamshauri Rais kama huyo Jaji anayehusika
aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
80
kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na
maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya
tabia mbaya.
(7) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara
ndogo ya (6) itamshauri Rais kwamba jaji ambaye habari zake
zimechunguzwa na hiyo Tume aondolewe kazini kwa sababu ya
kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine
yoyte au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa
kazini Jaji huyo anayehusika.
(8) Ikiwa suala la kumwondoa Jaji kazini limepelekwa kwenye
Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara
ndogo ya (6) ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi Jaji
huyo anayehusika, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi
huo wa kumsimamisha kazi Jaji huyo, na kwa hali yoyote uamuzi
huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba jaji huyo
asiondolewe kazini.
(9) Masharti ya ibara hii yatatumika bila ya kuathiri masharti ya
ibara ndogo ya (12) ya ibara ya 109 ya Katiba hii.
Kiapo cha
Majaji Sheria
ya 1979 Na.14
ib.6
Sheria 1985
Na.15 ib.22
111. Jaji wa Mahakama Kuu hatashika madaraka yake ila
mpaka awe ameapishwa kwanza kiapo cha uaminifu na pia kiapo
kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi
kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungw na Bunge.
SEHEMU YA TATU
MADARAKA YA KUAJIRI MAHAKIMU
NA WATUMISHI WENGINE WA
MAHAKAMA ZA TANZANIA BARA NA
TUME YA KUAJIRI YA MAHAKAMA
Tume ya
Kuajiri
ya Mahakama
Sheria 1985
Na.14 ib.7
Sheria ya
1985
Na.15 ib.22
Sheria ya
1990
Na.14 ib.6
112.-(1) Kutakuwa na Tume ya Kuajiri kwa ajili ya Mahakimu
na Watumishi wengineo wa Mahakam za Tanzania Bara.
Wajumbe wa Tume hiyo watakuwa hawa wafuatao:-
(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa Mwenyekiti;
(b) Mwanasheria Mkuu;
(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania
ambaye atateuliwa kwa ajili hiyo na Rais baada ya
kushauriana na Jaji Mkuu
(d) Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu;
(e) Wajumbe wawili ambao watateuliwa na Rais.
(2) Mtu hataweza kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume kwa
mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
81
ikiwa mtu huyo ni Mbunge au ni mtu mwenye madaraka ya aina
nyingine yoyote iliyotajwa kwa ajili hiyo na sheria iliyotungwa na
Bunge.
Madaraka ya
kuajiri
Mahakimu na
watumishi
wengine wa
Mahakama
Sheria ya
1979 Na.14
Ib.7
Sheria ya
1985 Na.15
ib.22
Sheria ya
1985 Na.24
ib….
113.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria yoyote iliyotungwa
na Bunge inayohusika na suala la kuajiri Mahakimu na Watumishi
wengineo wa Mahakama mgawanyo wa madaraka kwa ajili ya
suala hilo utakuwa ifuatavyo:
(a) madaraka ya kuwaajiri watu wa kushika madaraka ya
aina zilizotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii
(pamoja na madaraka ya kuwathibitisha watu hao
kazini na kuwapandisha vyeo) yatakuwa mikononi mwa
Rais;
(b) madaraka ya kudhibiti nidhamu ya watu hao na
madaraka ya kuwaondoa kazini yatakuwa mikononi
mwa Tume ya Kuajiri iliyotajwa katika ibara ya 112 ya
Katiba hii.
(2) Madaraka yanayohusika na masharti ya ibara hii ni
madaraka ya Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na
Naibu wa Msajili huyo wa daraja lolote, madaraka ya Msajili wa
Mahakama Kuu na Naibu wa Msajili huyo wa daraja lolote,
madaraka ya Hakimu Mkazi na Hakimu wa aina nyingine yoyote,
na madaraka ya aina nyingine yoyote yanayohusika na
Mahakama yoyote (isipokuwa Mahakama ya Kijeshi) itakayotajwa
na Sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya Katiba
hii.
Uanachama
katika Vyama
vy a Siasa
Sheria ya
1994 Na.34
ib.19
113A. Itakuwa ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani,
Jaji wa Mahakama Kuu, Hakimu wa ngazi yoyote kujiunga na
chama chochote cha Siasa, isipokuwa tu kwamba atakuwa na
haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
SEHEMU YA NNE
MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR
Mahakama
Kuu
ya Zanzibar
Sheria ya
1985 Na.15
ib.22
114. Kwa madhaumuni ya ufafanuzi wa Sura hii ya Katiba hii,
ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika sura hii hayazuii
kuendelea kuwapo au kuanzishwa, kwa mujibu wa Sheria
zinazotumika Zanzibar kwa Mahakama Kuu ya Zanzibar au
Mahakama zilizo chini ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
82
Mamlaka ya
Mahakama
Kuu
ya Zanzibar
Sheria ya
1985 Na.15
ib.22
na 25
115.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 83 na 116 ya
Katiba hii, mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar yatakuwa
kama itakavyoelezwa katika Sheria zinazotumika Zanzibar.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine
yoyote iliyotungwa na Bunge, iwapo sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge inayotumika Tanzania Bara na vile vile Tanzania Visiwani
imekabidhi madaraka yoyote kwa Mahakama Kuu, basi
Mahakama Kuu ya Zanzibar yaweza kutekeleza madaraka hayo
kwa kiasi kile kile inavyoweza kutekeleza Mahakama Kuu ya
Jamhuri ya Muungano.
SEHEMU YA TANO
MAHAKAMA YA RUFANI YA
JAMHURI YA MUUNGANO
Tafsiri
Sheria ya
1984 Na.15
ib.25 na 26
116.-(1) Katika Sehemu hii ya Tano ya Sura hii ya Tano ya
Katiba hii na katika sehemu nyingine za Katiba hii, ila iwapo
maelezo yahitaji vinginevyo:
"Idara ya Mahakama" maana yake ni Mahakama ya Rufani ya
Jamhuri ya Muungano iliyotajwa katika ibara ya 117 ya Katiba hii
(au kwa kifupi "Mahakama ya Rufani"), Mahakama Kuu ya
Jamhuri ya Muungano iliyotajwa katika ibara ya 108 ya Katiba hii
(ambayo itajulikana kwa kifupi kama "Mahakama Kuu) pamoja na
Mahakama nyingine zozote za ngazi zilizo chini ya Mahakama
Kuu;
"Jaji Mkuu" maana yake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani na
ni pamoja na Kaimu Jaji Mkuu au Jaji wa Rufani anayeshikilia au
kutekeleza madaraka ya Jaji Mkuu;
"Jaji wa Rufani" maana yake ni Jaji yoyote wa Mahakama ya
Rufani.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (3), Jaji Mkuu
hatakuwa na madaraka juu ya jambo lolote linalohusu muundo na
uendeshaji wa shughuli za siku hadi siku za Mahakama
zilizoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar au sheria yoyote
ya Tanzania Zanzibar.
(3) Jaji Mkuu atashauriana mara kwa mara na Jaji Mkuu wa
Zanzibar kuhusu uendeshaji wa shughuli za Mahakama ya Rufani
kwa jumla, na pia kuhusu uteuzi wa Majaji wa Rufani.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
83
Mhakama ya
Rufani ya
Jamhuri ya
Muungano na
mamlaka yake
sheria
za 1979 Na.14
ib.8 na
Sheria ya
1984
Na.15 ib.27
117.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya
Muungano (itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama ya
Rufani") ambayo mamlaka yake yatakuwa kama ilivyoelezwa
katika Katiba hii au katika Sheria nyingine yoyote.
(2) Mahakama ya Rufani haitakuwa na mamlaka yoyote
kuhusu usuluhishi wa suala lolote litakaloshughulikiwa kwa mujibu
wa masharti ya ibara ya 126 ya Katiba hii ambayo inahusu ubishi
kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar.
(3) Kazi ya Mahakama ya Rufani itakuwa ni kusikiliza na kutoa
uamuzi juu ya kila rufaa inayoletwa mbele ya Mahakama ya
Rufani kutokana na hukumu au uamuzi wa namna nyingine yoyote
wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Hakimu.
(4) Sheria iliyotungwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na
Bunge au na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar yaweza kuweka
masharti yatakayoeleza utaratibu wa kupeleka rufaa mbele ya
Mahakama ya Rufani, nyakati na sababu za kukata rufaa na
namna ya kushughulikia rufaa hizo.
Majaji wa
Mahakama ya
Rufani na
uteuzi wao
Sheria za
1979 Na.14
ib.8 na
Sheria ya
1984
Na.15 ib.28
118.-(1) Kutakuwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani
(ambaye katika ibara zifuatazo kwenye Katiba hii atatajwa tu kwa
kifupi kama "Jaji Mkuu" na Majaji wengine wa Mahakama ya
Rufani wasiopungua wawili, isipokuwa kwamba kikao maalum cha
Mahakama nzima kitakuwa kamili kikiwa na Majaji wa Rufani
wasiopungua watano.
(2) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais na atakuwa ndiye Kiongozi
wa Mahakama ya Rufani na pia Mkuu wa Idara ya Mahakama
kama ilivyofafanuliwa katika ibara ya 116 ya Katiba hii.
(3) Majaji wengineo wa Mahakama ya Rufani watateuliwa na
Rais, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa
watu ambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu
ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyoelezwa katika ibara ya 109
ya Katiba hii au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa
kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa
Sheria zinazotumika Zanzibar.
(4) Iwapo itatokea kwamba:-
(a) Kiti cha Jaji Mkuu kitakuwa wazi; au
(b) Jaji Mkuu hayupo Tanzania; au
(c) Jaji Mkuu atashindwa kutekeleza kazi yake kwa
sababu yoyote na Rais akiona kuwa kwa muda wa
tukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua Kaimu
Jaji Mkuu, basi Rais aweza kumteua Kaimu Jaji Mkuu
kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kustahili
kuteuliwa kuwa Majaji wa Mhakama ya Rufani, na huyo
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
84
Kaimu Jaji Mkuu atatekeleza kazi za Jaji Mkuu mpaka
atakapoteuliwa Jaji Mkuu au mpaka Jaji Mkuu
mwingine ambaye alikuwa hayupo Tanzania au alikuwa
hamudu kazi zake atakaporejea kazini.
(5) Ikitokea kwamba kiti cha Jaji yeyote wa Mahakama ya
Rufani kitakuw wazi au ikiwa Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani
atateuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu au kama atashindwa kutekeleza
kazi zake kwa sababu yoyote, au Jaji Mkuu atamshauri Rais kuwa
kazi za Mahakama kama ya Rufani ilivyo wakati huo zahitaji
ateuliwe Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani, basi Rais aweza,
baada ya kushauriana na Jaji Mkuu kama kawaida, kumteua
Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoka miongoni mwa watu
ambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani
kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii.
(6) Mtu yeyote atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama
ya Rufani kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara
hii, ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya
Rufani kwa muda wowote utakaotajwa wakati wa kuteuliwa kwake,
au, kama muda haukutajwa, mpaka uteuzi wake utakapofutwa na
Rais, lakini bila ya kujali kwamba muda wake wa kazi umemalizika
au kwamba uteuzi wake umefutwa, mtu huyo aweza kuendelea
kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani mpaka
amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe
shughuli nyingine yoyote inayohusika na rufaa au mashauri
mengine yoyote ambayo alikwisha anza kuyasikiliza kabla muda
wake wa kazi haujamalizika au kabla ya uteuzi wake haujafutwa.
(7) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi wa
masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 118 ya Katiba hii
(inayotaja idadi ya Majaji wa kudumu wa Mahakama ya Rufani) na
masharti ya ibara ya 119 ya Katiba hii (inayoeleza mamlaka ya
Majaji wa Mahakama ya Rufani), inatamkwa rasmi hapa kwamba
Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyeteuliwa kwa mujibu wa
masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara hii, atakuwa na mamlaka
kamili ya Jaji wa Mahakama ya Rufani na kwamb atatekeleza kazi
zake kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani bila ya kujali kuwa
kuteuliwa kwake kutakiuka idadi ya Majaji wa kudumu wa
Mahakama ya Rufani iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara
118 ya Katiba hii, lakini masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila
ya kuathiri masharti ya ibara ya 122 ya Katiba hii kuhusu kiwango
cha vikao vya Mahakama ya Rufani.
(8) Kazi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani haitafutwa wakati
yupo mtu aliyeshika madaraka ya kiti cha Jaji wa Mahakama ya
Rufani.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
85
Mamlaka ya
Majaji
Mahakama ya
Rufani Sheria
za 1979 Na.14
ib.8 na 1984
Na.14 ib.29
119. Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani hatakuwa na
mamlaka ya kusikiliza shauri lolote katika Mahakama Kuu au
katika Mahakama ya Hakimu ya ngazi yoyote:
Isipokuwa kwamba iwapo Jaji yeyote wa Mahakama Kuu
atateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, basi hata baada ya
kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji huyo
aweza kuendelea kufanya kazi zake katika Mahakama Kuu mpaka
amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka akamilishe
shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo
alikwisha anza kuyasikiliza kabla hajateuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani, na kwa ajili hiyo itakuwa halali kwake kutoa
hukumu au uamuzi mwingine wowote unaohusika kwa kwa
kutumia na kutaja madaraka aliyoshika kabla ya kuteuliwa kuwa
Jaji wa Mahakama ya Rufani, lakini endapo hatimaye hukumu hiyo
au uamuzi huo mwingine utapangwa kwa njia ya rufaa
itakayofikishwa mbele ya Mahakama ya Rufani, basi katika hali
hiyo Jaji huyo wa Mahakama ya Rufani, hatakuwa na mamlaka ya
kusikiliza rufaa hiyo.
Muda wa
Majaji
wa Mahakama
ya Rufani
kushika
Madaraka
sheria
za 1979 Na.14
ib.8 na
Sheria ya
1984
Na.15 ib.30
120.-(1) Kila Jaji wa Mahakama ya Rufani atalazimika kuacha
kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini na tano, lakini
masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila kuathiri masharti
yafuatayo katika ibara hii.
(2) Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani aweza kujiuzulu kazi
katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wakati
wowote baada ya kutimiza umri wa miaka sitini, isipokuwa kama
Rais ataagiza kwamba asijiuzulu, na iwapo Rais ataagiza hivyo,
basi huyo Jaji wa Mahakama ya Rufani atakayehusika na maagizo
hayo ya Rais hatakuwa na haki ya kujiuzulu mpaka upite kwanza
muda wowote utakaotajwa na Rais kwa ajili hiyo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
86
(3) Iwapo Rais ataona kuwa kwa ajili ya manufaa ya Umma
inafaa Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyetimiza umri wa miaka
sitini na tano aendelee kufanya kazi, na huyo Jaji mwenyewe wa
Mahakama ya Rufani anakubali kwa maandishi kuendelea
kufanya kazi; basi Rais aweza kuagiza kuwa Jaji huyo wa
Mahakama ya Rufani aendelee kufanya kazi kwa muda wowote
utakaotajwa na Rais.
(4) Bila ya kujali kwamba Jaji wa Mahakama ya Rufani
ametimiza umri ambao analazimika kuacha kazi kwa mujibu wa
masharti ya ibara hii, mtu anayefanya kazi ya Jaji wa Mahakama
ya Rufani aweza kuendelea kufanya kazi baada ya kutimiza umri
huo mpaka amalize kutayarisha na kutoa hukumu au mpaka
akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri
ambayo alikwisha anza kuyasikiliza kabla hajatimiza umri huo wa
kuacha kazi.
(5) Jaji wa Mahakama ya Rufani aweza tu kuondolewa katika
madaraka ya kazi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sababu ya
kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au
sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, na
hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya
utaratibu unaofanana na ule uliowekwa kwa ajili ya kumwondoa
kazini Jaji wa Mahakama Kuu kama ilivyoelezwa katika ibara
ndogo ya (6) na ya (7) ya ibara ya 110 ya Katiba hii, na kwa ajili
hiyo masharti ya ibara ndogo ya (8) ya ibara hiyo ya 110
yatatumika kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa namna ile ile
yanavyotumika kwa Jaji wa Mahakama Kuu.
(6) Masharti ya ibara hii yatatumika bila ya kuathiri masharti ya
ibara ndogo ya (5) ya ibara ya 118 ya Katiba hii.
Kiapo cha
Majaji
wa Mahakama
ya Rufani
Sheria za
1979 Na.14
ib.8 na
Sheria ya
1984
Na.15 ib.31
121. Jaji wa Mahakama ya Rufani hatashika madaraka yake
ila mpaka awe ameapishwa kiapo cha uaminifu na kiapo kingine
chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa
mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
87
Kiwango cha
vikao vya
Mahakama ya
Rufani
Sheria za
1979 Na.14
ib.8 na
Sheria ya
1984
Na.15 ib.32
122.-(1) Kiwango cha kila kikao cha Mahakama ya Rufani ni
Majaji wa Mahakama ya Rufani wasiopungua watatu.
(2) Katika kila rufaa suala linalohitaji uamuzi wa Mahakama ya
Rufani litaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji
wa Mahakama ya Rufani waliosikiliza rufaa.
Mashauri
yanayoweza
kuamuliwa na
Jaji mmoja wa
Mahakama ya
Rufaa
Sheria za
1979 Na.14
ib.8 na
Sheria ya
1984
Na.15 ib.33
123. Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani aweza kutekeleza
madaraka yoyote ya Mahakama ya Rufani ambayo hayahusiki na
kutoa uamuzi juu ya Rufaa:
Isipokuwa kwamba:
(a) Katika mashauri ya jinai, iwapo Jaji wa Mahakama ya
Rufani aliyeombwa kutekeleza madaraka hayo atatoa
uamuzi ambao mwombaji haridhiki nao, basi mwombaji
atakuwa na haki kutaka maombi yake yaamuliwe na
Mahakama ya rufani;
(b) Katika mashauri ya madai, Mahakama ya Rufani
yaweza kubatilisha au kubadilisha amri, agizo au
uamuzi wa namna nyingine wowote uliotolewa na Jaji
mmoja wa Mahakama ya Rufani kwa mujibu wa
masharti ya ibara hii.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
88
SEHEMU YA SITA
UTARATIBU WA KUPELEKA HATI
NA KUTEKELEZA MAAGIZO
YALIYOMO KATIKA HATI
ZILIZOTOLEWA NA MAHAKAMA
Utekelezaji wa
maagizo ya
Mahakama
utafanywa
nchini Tanzania
kote Sheria ya
1984 Na.15
ib.34
124.-(1) Hati zenye maagizo yaliyotolewa na Mahakama za
Tanzania Bara na Mahakama za Tanzania Zanzibar katika
mashauri ya madai ya aina zote na mashauri ya jinai ya aina zote
(pamoja na hati za kuamuru kukamata watu) zaweza kupelekwa
mahali popote nchini Tanzania na maagizo hayo yaweza
kutekelezwa mahali popote nchini Tanzania kwa kufuata
masharti yafuatayo:-
(a) iwapo mahakama imetoa hati zenye maagizo
yatakayotekelezwa mahali ambako mahakama hiyo
haina mamlaka, basi hati hiyo itapelekwa huko na
maagizo yaliyomo katika hati hiyo yatatekelezwa kwa
mujibu wa utaratibu unaotumika huko kwa ajili ya
kupeleka hati au kutekeleza maagizo yaliyomo katika
hati iliyotolewa na mahakama yenye mamlaka huko
ilikopelekwa hati; na
(b) iwapo sheria inayotumika huko ilikopelekwa hati
imeweka masharti kwamba hati zilizotolewa na
mahakama ya mahali pengine ni lazima ithibitishwe
kwanza na Mahakama yenye mamlaka mahali hapo
inapotumika sheria hiyo, basi kila hati iliyotolewa na
mahakama ya mahali pengine itabidi ithibitishwe
kwanza kwa mujibu wa sheria hiyo kabla maagizo
yaliyomo katika hati hiyo hayajatekelezwa.
(2) Iwapo mtu amekamatwa mahali popote nchini Tanzania
kwa mujibu wa hati ya kuamuru kukamatwa kwake iliyotolewa na
mahakama ambayo haina mamlaka mahali hapo alipokamatwa
mtu huyo, basi mtu huyo atahesabiwa kuwa yuko chini ya ulinzi
halali na aweza kufikishwa mbele ya mahakama iliyotoa hati hiyo,
lakini masharti haya yaliyomo katika ibara hii ndogo itabidi
yatumiwe bila kuathiri masharti ya sheria inayotumika hapo
mahali alipokamatwa mtu huyo.
(3) Masharti yaliyomo katika ibara hii hayatazuia sheria
kuweka utaratibu kwa ajili ya kupeleka nje ya Tanzania hati
zilizotolewa na Mahakama za Tanzania Bara au mahakama za
Tanzania Visiwani.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
89
SEHEMU YA SABA
MAHAKAMA MAALUM YA KATIBA
YA JAMHURI YA MUUNGANO
Mahakama
Maalum ya
Katiba ya
Jamhuri ya
Muungano
Sheria
ya 1984 Na.15
ib.35
125. Kutakuwa na Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano ambayo Mamlaka yake, muundo wake na utaratibu
wa shughuli zake ni kama ilivyoelezwa katika ibara ya 126, 127
na 128 ya Katiba hii.
Mamlaka ya
Mahakama
Maalum ya
Katiba Sheria
ya 1979 Na.14
ib.9
na Sheria ya
1984 Na.15
ib.36
126.-(1) Kazi pekee ya Mahakama Maalum ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano ni kusikiliza shauri lililotolewa mbele yake,
kutoa uamuzi wa usuluhishi, juu ya suala lolote linalohusika na
tafsiri ya Katiba hii iwapo tafsiri hiyo au utekelezaji wake
unabishaniwa kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
(2) Katika kutekeleza kazi yake kwa mujibu wa masharti ya
ibara hii, Mahakama Maalum ya Katiba haitakuwa na mamlaka
ya kuchunguza au kubadilisha uamuzi wa Mahakama Kuu au
uamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa kwa mujibu wa
masharti ya ibara ya 83 ya Katiba hii au uamuzi wa Mahakama
ya Rufani uliotolewa kwa mujibu wa ibara ya 117 ya Katiba hii.
(3) Kila uamuzi wa usuluhishi utakaotolewa na Mahakama
Maalum ya Katiba kwa mujibu wa ibara hii utakuwa ndio wa
mwisho, hakutakuwa na haki ya kukata rufaa popote.
Muundo wa
Mahakama
Maalum ya
Katiba Sheria
ya 1984 Na.15
ib.37
127.-(1) Mahakama Maalum ya Katiba itakuwa na
wajumbe ambao nusu ya jumla ya wajumbe wote watateuliwa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na nusu nyingine ya jumla hiyo
watateuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
(2) Mtu anayeweza kuteuliwa kuwa Mjumbe wa
Mahakama Maalum ya Katiba ni yule tu ambaye ni jaji au
aliyepata kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama
Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar,
au mtu mwenye uwezo na ujuzi wa kazi ya Jaji na anayestahili
kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji kwa mujibu wa Sheria
inayotumika Tanzania Bara na sheria inayotumika Tanzania
Zanzibar, kadri hali itakavyokuwa.
(3) Mtu aweza kuteuliwa kuwa mjumbe wa Mahakama
Maalum ya Katiba ama kwa ajili ya kusikiliza shauri moja tu au
mashauri mawili au zaidi kama yatatokea. Mjumbe ataendelea
kutekeleza madaraka ya kazi yake kama Mjumbe wa Mahakama
Maalum ya Katiba mpaka shauri analohusika nalo litakapokwisha
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
90
au mpaka uteuzi wake utakapofutwa au mpaka atakaposhindwa
kutekeleza kazi yake kama Mjumbe kwa sababu ya maradhi au
sababu nyingine yoyote.
Utaratibu katika
vikao vya
Mahakama
Maalum ya
Katiba
Sheria ya 1984
Na.15 ib.37
128.-(1) Mahakama Maalum ya Katiba itafanya vikao vyake
wakati ule tu kunapokuwa na shauri la kusikiliza, na itafanya
vikao vyake mahali popote patakapoamuliwa kwa utaratibu
utakaotumika kwa ajili ya mashauri yatakayosikilizwa na
Mahakama Maalum ya Katiba.
(2) Kiwango cha kila kikao cha Mahakama Maalum ya
Katiba ni wajumbe wote, na iwapo mjumbe yeyote atakuwa
hayupo au ikiwa kiti cha mjumbe yoyote kitakuwa wazi basi
Serikali iliyomteua mjumbe huyo ambaye hayupo au ambaye kiti
chake ki wazi itamteua mjumbe mwingine wa kushika mahali
pake. Mjumbe wa muda aliyeteuliwa kwa mujibu wa ibara hii
ndogo ataendelea kutekeleza kazi katika Mahakama Maalum ya
Katiba mpaka mjumbe wa kawaida atakaporejea kazini au mpaka
mtu atakapoteuliwa kujaza nafasi iliyo wazi au mpaka shauri
litakapokwisha, kutegemea ni lipi kati ya mambo hayo litakalo
tokea mapema zaidi.
(3) Kila suala linalohitaji uamuzi wa Mahakama Maalum ya
Katiba litaamuliwa kwa kufuata kauli ya theluthi mbili ya wajumeb
kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutoka
Tanzania Zanzibar.
(4) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka
masharti kuhusu utaratibu wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa
Mahakama Maalum ya Katiba, utartibu wa kupeleka shauri mbele
ya Mahakama hiyo, utaratibu wa kuendesha shauri katika
Mahakama na utaratibu wa kuwasilisha Serikalini uamuzi wa
Mahakama Maalum ya Katiba:
Isipokuwa kwamba iwapo shauri lolote litafikishwa mbele ya
Mahakama Maalum ya Katiba wakati hakuna sheria yoyote ya
aina iliyoelezwa katika ibara hii ndogo, basi shauri litasikilizwa na
kuamuliwa kwa kufuata utaratibu utakaowekwa na Mahakama
yenyewe kabla ya kuanza kusikiliza shauri, au iwapo Wajumbe
wa Mahakama watashindwa kukubaliana juu ya utaratibu huo,
basi shauri litasikilizwa na kuamuliwa kwa kufuata utaratibu
utakaoamuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa
kushirikiana na Serikali ya Zanzibar.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
91
SURA YA SITA
SEHEMU YA KWANZA
TUME YA HAKI ZA BINADAMU
NA UTAWALA BORA
Tume ya Haki
za Binadamu na
Utawala Bora
Sheria ya 2000
Na.3 ib.17
129.-(1) Kutakuwa na Tume itakayoitwa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, ambayo majukumu yake yatakuwa
kama ilivyoelezwa katika ibara ya 130 ya Katiba hii.
(2) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora itakuwa na
Makamishna wafuatao:
(a) Mwenyekiti, ambaye atakuwa ni mtu mwenye sifa ya
kuweza kuteuliwa kuwa Jaji;
(b) Makamu Mwenyekiti, ambaye atateuliwa kwa
kuzingatia kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu
anayetoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano,
yeye atakuwa ni mtu wa kutoka upande mwingine wa
Jamhuri ya Muungano;
(c) Makamishna wengine wasiozidi watano
watakaoteuliwa kutoka miongoni mwa watu wenye
ujuzi, uzoefu na upeo mkubwa katika mambo ya haki
za binadamu, sheria, utawala, siasa au mambo ya
jamii;
(d) Makamishna Wasaidizi.
(3) Makamishna na Makamishna Wasaidizi wote watateuliwa
na Rais baada ya kushauriana na Kamati ya Uteuzi.
(4) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi kwa madhumuni ya ibara
hii ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani;
(b) Spika wa Bunge;
(c) Jaji Mkuu wa Zanzibar;
(d) Spika wa Baraza la Wawakilishi; na
(e) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye
atakuwa ndiye Katibu wa Kamati hii.
(5) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna
wengine wote kila mmoja atashika madaraka yake kwa kipindi
cha miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine
kimoja tu cha miaka mitatu.
(6) Kwa madhumuni ya kuwakinga Makamishna kutokana na
migongano ya kimasilahi, mtu yeyote akiteuliwa kuwa Kamishna
wa Tume atalazimika kuacha mara moja madaraka yoyote katika
chama chochote cha siasa au madaraka ya aina nyingine yoyote
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
92
itakayotajwa kwa ajili hiyo na sheria iliyotungwa na Bunge.
(7) Kamishna au Kamishna Msaidizi wa Tume aweza tu
kuondolewa katika madaraka ya kazi yake katika Tume kwa
sababu ya kushindwa kutekeleza kazi yake, ama kutokana na
maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabia
mbaya inayoathiri maadili ya kazi ya Kamishna.
(8) Tume yaweza kutekeleza shughuli zake bila ya kujali
kwamba kuna nafasi iliyo wazi miongoni mwa viti vya wajumbe
au kwamba mjumbe mmojawapo hayupo.
Majukumu ya
Tume na
taratibu
za utekelezaji
Sheria ya 2000
Na.3 ib.17
130.-(1) Tume ya Haki na Utawala Bora itatekeleza
majukumu yafuatayo:
(a) kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu na
wajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba na Sheria za
nchi;
(b) kufanya shughuli za kupokea malalamiko ya uvunjaji
wa haki za binadamu kwa jumla;
(c) kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu
uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi
ya utawala bora.
(d) kufanya utafiti, kutoa na kueneza nchini elimu kwa
umma kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
(e) kama ikibidi, kufungua mashauri mahakamani ili
kuzuia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu au
kurekebisha haki inayotokana na uvunjwaji huo wa
haki za binadamu, au ukiukwaji wa misingi ya utawala
bora;
(f) kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika
au taasisi yoyote inayohusika na masharti ya ibara hii
katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi
au majukumu yake au utekelezaji unaokiuka
madaraka hayo;
(g) kutoa ushauri kwa Serikali na vyomno vingine vya
umma na vya sekta ya binafsi kuhusu haki za
binadamu na utawala bora;
(h) kuchukua hatua zipasazo kwa ajili ya kukuza na
kuendeleza usuluhishi na suluhu miongoni mwa watu
na taasisi mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbele
ya Tume.
(2) Tume itakuwa ni idara inayojitegemea, na bila ya kuathiri
masharti meingine ya ibara hii, katika kutekeleza madaraka yake
kwa mujibu wa Katiba hii, Tume haitalazimika kufuata maagizo
au amri ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali au maoni ya
chama chochote cha siasa au ya taasisi nyingine yoyote ya
umma au ya sekta ya binafsi.
(3) Masharti ya ibara ndogo ya (2) yasihesabiwe kuwa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
93
yanamzuia Rais kutoa maagizo au amri kwa Tume, wala hayatoi
Haki kwa Tume kutofuata maagizo au amri, endapo Rais ataona
kuwa, kuhusiana na jambo lolote au hali yoyote, masilahi ya taifa
yahitajia hivyo.
(4) Tume itafanya uchunguzi kwa kufuata masharti ya ibara
hii na masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, na
itafanya uchunguzi juu ya mtu yeyote anayehusika au taasisi
yoyote inayohusika kila itakapoagizwa na Rais kufanya
uchunguzi; vilevile, isipokuwa kama Rais ameagiza Tume
isifanye uchunguzi, Tume yaweza kufanya uchunguzi wakati
wowote inapoona infaa kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote
anayehusika, au taasisi yoyote inayohusika, na masharti ya ibara
hii anayetuhumiwa au inayotuhumiwa kwa kukiuka madaraka ya
kazi yake, kutumia vibaya madaraka ya kazi yake au majukumu
ya taasisi hiyo au kwa uvunjaji wa haki za binadamu au misingi
ya utawala bora.
(5) Tume haitakuwa na mamlaka yoyote, ama kwa mujibu wa
masharti ya ibara hii au masharti ya sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge kwa madhumuni ya sura hii ya Katiba hii ya kuchunguza
uamuzi wa Jaji yeyote, Hakimu yeyote au wa Mahakama iwapo
uamuzi huo ameutoa katika kutekeleza madaraka ya kazi yake;
vile vile Tume haitakuwa na mamlaka ya kuchunguza uamuzi
wowote uliotolewa na chombo chochote chenye asili ya
Mahakama kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria iwapo uamuzi
huo umetolewa katika kutekeleza mamlaka yake.
(6) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watumishi wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na wale wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, watumishi na viongozi wa vyama vya
siasa wanaoshughulikia mambo ya umma, wajumbe na
watumishi wa Tume zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
za Serikali hizo, mashirika ya umma na vyombo vingine vya
umma au vya binafsi, kama ni kampuni, jumuiya, ushirika,
wadhamini au muundo mwingine wowote, kadri itakavyoelezwa
katika sheria iliyotungwa na Bunge; lakini masharti haya
hayatatumika kwa Rais wala kwa Kiongozi wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar isipokuwa tu kwa kuzingatia masharti ya
ibara ya 46 ya Katiba hii au ibara ya 36 ya Katiba ya Zanzibar, ya
1984.
Mamlaka ya
Tume na
utaratibu wa
shughuli zake
Sheria ya 2000
Na.3 ib.17
131.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii,
Bunge laweza kutunga sheria kwa mujibu wa masharti ya Sura
hii ya Katiba hii kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu mamlaka ya
Tume, utaratibu wa kuendesha shughuli zake na kuhusu kinga za
kisheria watakazokuwa nazo Makamishna na watumishi wa
Tume kwa makusudi ya kuwawezesha kutekeleza kazi zao bila
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
94
ya matatizo ya kisheria.
(2) Tume haitachunguza mambo yafuatayo, kwa madhumuni
ya kutekeleza majukumu yake, yaani:
(a) jambo lolote ambalo liko mbele ya Mahakama au
chombo kinginecho cha kimahakama;
(b) jambo lolote linalohusu uhusiano au mashirikiano kati
ya Serikali na Serikali ya nchi yoyote ya nje au Shirika
la Kimataifa;
(c) jambo linalohusu madaraka ya Rais kutoa msamaha;
(d) jambo jingine lolote lililotajwa na sheria yoyote.
(3) Kila mwaka wa fedha Tume itatayarisha na kuwasilisha
kwa Waziri anayesimamia haki za binadamu taarifa kuhusu-
(a) shughuli za Tume katika mwaka uliotangulia;
(b) hali ya utekelezaji wa hifadhi ya haki za binadamu
katika Jamhuri ya Muungano,
Na Waziri atawasilisha mbele ya Bunge kila taarifa
iliyowasilishwa kwake na Tume mapema iwezekanavyo baada ya
kuipokea.
(4) Masharti ya ibara ndogo ya (3) hayatahesabiwa kuwa
yanaizuia Tume kuwasilisha taarifa nyingine yoyote kwa mtu
mwingine au mamlaka nyingine yoyote.
SEHEMU YA PILI
SEKRETARIETI YA MAADILI YA
VIONGOZI WA UMMA
Sekretarieti ya
Maadili
Sheria ya 1995
Na.12 ib.18
132.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma ambayo itakuwa na mamlaka ya kuchunguza tabia na
mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya
kuhakikisha kwamba masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi
wa Umma yanazingatiwa ipasavyo.
(2) Kwa madhumuni ya ibara hii, maana ya kiongozi wa
umma na masharti ya maadili ya viongozi wa umma itabidi
ifahamike kwa mujibu wa masharti ya sheria ya Maadili ya
Viongozi wa Umma au masharti ya sheria nyingine yoyote
iliyotungwa na Bunge kwa kadri masharti hayo yanavyohusika
na suala la uongozi na ufafanuzi wake.
(3) Sekretarieti ya Maadili itakuwa na Kamishna wa Maadili
na wafanya kazi wengine ambao idadi yao itatajwa na sheria
iliyotungwa na Bunge.
(4) Bunge litatunga Sheria itakayoainisha misingi ya Maadili
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
95
ya Viongozi wa Umma itakayozingatiwa na watu wote
wanaoshika nafasi za madaraka zitakazotajwa na Bunge.
(5) Misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma:
(a) itafafanua nafasi za madaraka ambazo watu wenye
kushika nafasi hizo watahusika nayo;
(b) itawataka watu wanaoshika nafasi fulani za
madaraka kutoa mara kwa mara maelezo rasmi
kuhusu mapato, rasilimali na madeni yao;
(c) itapiga marufuku mienendo na tabia inayopelekea
kiongozi kuonekana hana uaminifu, anapendelea au
si muadilifu au inaelekea kukuza au kuchochea
rushwa katika shughuli za umma au inahatarisha
maslahi au ustawi wa jamii;
(d) itafafanua adhabu zinazoweza kutolewa kwa kuvunja
misingi ya maadili;
(e) itaelekeza taratibu, madaraka na desturi
zitakazofuatwa ili kuhakikisha utekelezaji wa maadili;
(f) itaweka masharti mengine yoyote yanayofaa au
ambayo ni muhimu kwa madhumuni ya kukuza na
kudumisha uaminifu, uwazi, kutopendelea na uadilifu
katika shughuli za umma na kwa ajili ya kulinda
fedha na mali nyinginezo za umma.
(6) Bunge laweza kwa sheria kuweka masharti ya mtu
kufukuzwa au kuondolewa kazini kutokana na kuvunja maadili
ya viongozi, bila ya kujali kama kazi hiyo ni ya kuchaguliwa na
kuteuliwa.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
96
SURA YA SABA
MASHARTI KUHUSU FEDHA ZA
JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
MCHANGO NA MGAWANYO WA MAPATO
YA JAMHURI YA MUUNGANO
Akaunti ya Fedha
ya pamoja
Sheria ya 1984
Na.15 ib.42
133. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itatunza akauti
maalum itakayoitwa "Akaunti ya Fedha ya Pamoja" na ambayo
itakuwa ni sehehmu ya Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano, ambamo kutawekwa fedha yote
itakayochangwa na Serikali mbili kwa kiasi kitakachoamuliwa na
Tume ya pamoja ya Fedha kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge, kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuri ya Muungano
kwa Mambo ya Muungano.
Tume ya pamoja
ya Fedha
Sheria ya 1984
Na.15 ib.42
134.-(1) Kutakuwa na Tume ya pamoja ya Fedha yenye
wajumbe wasiozidi saba ambao watateuliwa na Rais kwa
mujibu wa ibara hii na masharti ya sheria iliyotungw na Bunge.
(2) Majukumu ya Tume yatakuwa ni:
(a) kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na,
au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Muungano,
na kutoa mapendekezo kwa Serikali mbili kuhusu
mchango na mgawo wa kila mojawapo ya Serikali
hizo;
(b) kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za
fedha wa Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano
katika mambo ya kifedha kati ya Serikali mbili;
(c) kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais
ataipatia Tume au kama Rais atakavyoagiza, na kwa
mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
97
SEHEMU YA PILI
MFUKO MKUU WA HAZINA NA FEDHA
ZA JAMHURI YA MUUNGANO
Mfuko Mkuu wa
Hazina ya
Serikali ya
Jamhuri ya
Muungano
Sheria ya 1984
Na.15 ib.
135.-(1) Fedha zote zitakazopatikana kwa njia mbalimbali
kwa ajili ya matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
isipokuwa fedha za aina iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya
ibara hii, zitawekwa katika mfuko mmoja maalum ambao utaitwa
Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.
(2) Fedha ambazo hazitawekwa kwenye Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na Sheria
kwamba zitumike kwa shughuli maalum au ziwekwe katika
mfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum.
Masharti ya
kutoa fedha za
matumizi kutoka
mfuko
Mkuu wa Hazina
ya Serikali
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
136.-(1) Fedha hazitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina
ya Serikali kwa ajili ya matumizi ila kwa mujibu wa masharti
yafuatayo:-
(a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo
yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika
Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na idhini hiyo iwe
imetolewa na Katiba hii au sheria nyingine yoyote;
(b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo
yameidhinishwa ama na sheria ya Matumizi ya
Serikali iliyotungwa mahsusi na Bunge au sheria
iliyotungwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 140
ya Katiba hii.
(2) Fedha zilizomo katika mfuko maalum wowote wa serikali,
ukiachilia mbali Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, hazitatolewa
kutoka mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi
hayo yawe yameidhinishwa na sheria.
(3) Fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali
hazitatolewa kutoka Mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka
matumizi hayo yawe yameidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali na pia kwa sharti kwamba fedha
hizo ziwe zimetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa ajili
hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
98
Utaratibu wa
kuidhinisha
matumizi ya
fedha zilizomo
katika Mfuko
Mkuu wa Hazina
ya Serikali Sheria
ya 1984 Na.15
ib.43
137.-(1) Rais atatoa maagizo kwa watu wanaohusika
kwamba watengeneze na kuwasilisha kwenye Bunge katika kila
mwaka wa fedha wa Serikali, makadirio ya mapato na matumizi
ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kipindi cha
mwaka wa fedha unaofuata.
(2) Baada ya Bunge kuyakubali makadirio ya matumizi
(mbali na matumizi ambayo yameidhinishwa ama na Katiba hii
au sheria nyingine yoyote kuwa yatokane na fedha zilizomo
katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali) kutawasilishwa
kwenye Bunge Muswada ambao utaitwa Muswada wa Sheria ya
Matumizi ya fedha za Serikali, kwa ajili ya kuidhinisha matumizi
ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, na fedha
hizo zitatolewa kulipa gharama za shughuli mbalimbali za
Serikali zinazohusika na makadirio hayo.
(3) Ikiwa katika mwaka wa fedha wowote inaonekana
kwamba:
Fedha za matumizi zilizoidhinishwa na sheria ya
matumizi ya Fedha za Serikali kwa ajili ya shughuli fulani
hazitoshi au kwamba imekuwa lazima kulipa gharama za
shughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibu
wa sheria; au
Kuna fedha ambazo zimetumiwa kwa ajili ya shughuli
fulani kwa kiasi kinachozidi kiwango cha matumizi
yaliyoidhinishwa na sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali
kuhusu shughuli hiyo au kwamba fedha zimetumiwa kulipia
gharama za shughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizi
kwa mujibu wa Sheria, kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio
ya matumizi ya nyongeza au, kadri itakavyokuwa, maelezo ya
matumizi ya ziada, na baada ya Bunge kuyakubali hayo
Makadirio ya matumizi ya nyongeza au maelezo ya matumizi ya
ziada, kutawasilishwa kwenye Bunge Muswada wa Sheria ya
Matumizi ya fedha za Serikali kwa ajili ya kuidhinisha matumizi
ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na fedha
hizo zitatumiwa kulipia gharama za shughuli zinazohusika na
hayo makadirio au maelezo.
Masharti ya
kutoza kodi
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
138.-(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa
kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wa
utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu kisheria na
sheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
99
(2) Masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (1) ya ibara hii
hayatalizuia Baraza la Mapinduzi la Zanzibar kutumia mamlaka
yake ya kutoza kodi ya aina yoyote kwa mujibu wa madaraka ya
Baraza hilo.
Utaratibu wa
kuidhinisha
matumizi ya
fedha kabla ya
Sheria za
Matumizi kuanza
kutumika
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
139.-(1) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka
masharti ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu
wa Hazina ya Serikali kwa kufuata utaratibu ulioelezwa katika
ibara ndogo ya (2) ya ibara hii.
(2) Iwapo mwaka wa fedha wa Serikali umeanza na Sheria ya
Matumizi ya Fedha za Serikali inayohusika na mwaka huo
haijaanza kutumika basi Rais aweza kuidhinisha fedha itolewe
kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa ajili ya kulipia
gharama za lazima za shughuli za Serikali, na fedha hizo
zitatumiwa mpaka ipite miezi minne tangu mwanzo wa mwaka
wa fedha mpaka Sheria ya matumizi ya Fedha za Serikali
itakapoanza kutumika, kutegemea ni lipi kati ya mambo hayo
litakalotokea mapema zaidi.
Mfuko wa
matumizi ya
dharura
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
140.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka
masharti kuhusu mambo yafuatayo:
(a) kuanzisha mfuko wa matumizi ya dharura na
kumwezesha Rais au Waziri aliyeteuliwa na Rais
kwa ajili hiyo kuazima fedha kutoka mfuko huo
kulipia gharama za jambo la haraka na la dharura
ambalo halikutazamiwa kutokea na ambalo
halikupangiwa fedha zozote za matumizi; na
(b) kumwezesha Rais au Waziri aliyeteuliwa na Rais
kwa ajili hiyo kutumia fedha zilizotengwa mahsusi
kwa ajili ya shughuli fulani kulipia gharama za jambo
la haraka na la dharura kama ilivyoele zwa katika aya
ya (a) ya ibara hii ndogo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
100
(2) Iwapo fedha zimeazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi ya
dharura au fedha zilitengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli fulani
zimetumiwa kulipia gharama za jambo la haraka na la dharura,
basi kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio ya matumizi ya
nyongeza, na baada ya Bunge kuyakubali makadirio hayo
Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali
utakaowasilishwa kwenye Bunge kwa ajili ya kuidhinisha
Matumizi hayo ya nyongeza utahakikisha kwamba fedha zozote
zilizoazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi ya dharura
zitarudishwa kwenye Mfuko huo kutokana na fedha za matumizi
yatakayoidhinishwa na Muswada huo.
Deni la Taifa
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
141.-(1) Deni la Taifa litadhaminiwa na Mufko Mkuu wa
Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa ibara hii deni la Taifa
maana yake ni deni lenyewe na pia faida inayolipwa juu ya deni
hilo, fedha zinazowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni pole pole
na gharama zote zinazoambatana na usimamizi wa deni hilo.
Mishahara ya
watumishi fulani
wa Serikali
kudhaminiwa na
Mfuko Mkuu wa
Hazina ya
Serikali Sheria ya
1984 Na.15 ib.43
142.-(1) Watumishi wa Serikali wanaohusika na masharti ya
ibara hii watalipwa mishahara na posho kama itakavyoelezwa
na sheria iliyotungwa na Bunge.
(2) Fedha za malipo ya mishahara na posho za watumishi
wa Serikali wanaohusika na masharti ya ibara hii pamoja na
fedha za malipo ya uzeeni na kiinua mgongo kwa wale
wanaostahili malipo hayo miongoni mwa watumishi hao
zitatolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.
(3) Mshahara anaolipwa mtumishi wa Serikali anayehusika
na masharti ya ibara hii pamoja na masharti yake ya kazi
havitabadilishwa, baada ya mtumishi huyo kuteuliwa, kwa jinsi
ambayo itapunguza masilahi ya mtumishi huyo, lakini maelezo
haya hayahusiki na posho anayolipwa mtumishi huyo.
(4) Iwapo mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya
ibara hii ana hiari ya kuchagua kima cha mshahara au aina ya
masharti ya kazi, basi kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti
ya ibara ndogo ya (3) ya ibara hii, mshahara wa kima hicho
atakachochagua na aina hiyo ya masharti ya kazi
atakayochagua vitahesabiwa kuwa vina masilahi zaidi kwake
kuliko kima cha mshahara kingine chochote angalichoweza
kuchagua au aina ya masharti ya kazi nyingine yoyote
angaliyoweza kuchagua.
(5) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa Jaji wa Mahakama
ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano,
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
101
Mwenyekiti na kila Mjumbe wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi
na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri
ya Muungano.
Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za
Serikali wa
Jamhuri ya
Muungano
Sheria za 1979
Na.14 ib.11
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
143.-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na
jukumu juu ya mambo yafuatayo:
(a) kuhakikisha kwamba fedha zozote
zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali matumizi yake yameidhinishwa
na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 136 ya Katiba hii, na iwapo atatosheka
kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo,
basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe;
(b) kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi
yake yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo
katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au fedha
ambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheria
iliyotungwa na Bunge, na ambazo zimetumika,
zimetumiwa kwa ajili ya shughuli zilizo husika na
matumizi ya fedha hizo na kwamba matumizi hayo
yamefanywa kwa kufuata idhini iliyotolewa kuhusu
matumizi hayo; na
(c) angalau mara moja kila mwaka kufanya ukaguzi
na kutoa taarifa juu ya ukaguzi wa hesabu za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano, hesabu
zinazosimamiwa na watumishi wote wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na hesabu za Mahakama
zote za Jamhuri ya Muungano na hesabu
zinazosimamiwa na Katibu wa Bunge.
(3) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu na kila mtumishi
wa Serikali aliyeruhusiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu atakuwa na haki ya kuchunguza vitabu, kumbukumbu,
hati nyinginezo zote zinazohusika na hesabu za aina yoyote
iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii.
(4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwa
Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara
ndogo ya (2) ya ibara hii. Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais
atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye
kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais
kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho
kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho.
Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa
Spika wa Bunge (au Naibu wa Spika ikiwa kiti cha Spika ki wazi
wakati huo au ikiwa kwa sababu yoyote Spika hawezi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
102
kutekeleza shughuli za kazi yake) ambaye atawasilisha taarifa
hiyo kwenye Bunge.
(5) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa pia na
jukumu la kutekeleza kazi na shughuli nyingine, na atakuwa na
madaraka mengine ya namna mbalimbali, kama itakavyoelezwa
na sheria kuhusu hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano
au hesabu za vyombo vya Umma au hesabu za Mashirika.
(6) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa
masharti ya ibara ndogo ya (2), (3) na (4) ya ibara hii, Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au
maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali,
lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama
nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza madaraka
yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.
Kumwondoa
kazini Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.43
Sheria ya 1995
Na.12 ib.19
144.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika
ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Jamhuri ya
Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa
miaka sitini au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria
iliyotungwa na Bunge.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu
kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya
kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au
sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au
kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa
masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii.
(3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti
ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo
yatakuwa ifuatavyo:
(a) Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na
Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua
wawili. Huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya
wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu
ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa
Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi
yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;
(b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa
taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na
itamshauri Rais kama huyo Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa mujibu wa
masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
103
kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu
nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.
(4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara
ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa
kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote
au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini.
(5) Ikiwa suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya
uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, Rais aweza
kumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa
kumsimamisha kazi, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika
ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini.
(6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au
aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi
kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine
yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(7) Mashartiya ibara hii hayatatumika kwa mtu yoyote
aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.
SURA YA NANE
MADARAKA YA UMMA
Serikali za Mitaa
Sheria ya 1984
Na.15 ib.50
145.-(1) Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katika
kila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano,
ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.
(2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa,
litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo
vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato
na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.
Kazi za Serikali
za Mitaa Sheria
ya 1984 Na.15
ib.20
146.-(1) Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni
kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za
Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikisha
wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa
maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.
(2) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara
ndogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwa
kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
104
shughuli zifuatazo -
(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo
lake;
(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa
wananchi; na
(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia
demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.
SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI
Marufuku kuunda
majeshi ya Ulinzi
yasiyo majeshi
ya ulinzi ya
Umma Sheria ya
1984 Na.15 ib.49
Sheria ya 1992
Na.4 ib.36
147.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au
kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au
kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu
wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina
mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi
wa Tanzania.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki
ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake
ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu
katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi
la Kujenga Taifa.
Madaraka ya
Amiri Jeshi Mkuu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.49
148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
(2) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge, madaraka juu ya mambo yafuatayo
yatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani-
(a) madaraka ya kuwateua viongozi katika majeshi ya
ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(b) madaraka ya kuwateua watu watakaojiunga na
majeshi ya ulinzi na madaraka ya kuwaondoa jeshini
wanajeshi;
(c) madaraka ya kuwateua wanajeshi watakaoongoza
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
105
vikosi mbali mbali vya majeshi ya ulinzi; na
(d) madaraka ya kumwamuru mwanajeshi yeyote
asitumie madaraka yoyote aliyokabidhiwa na
ambayo yanaambatana na kuwa kwake mwanajeshi.
(3) Jambo lolote atakalotenda mwanajeshi yoyote kinyume
cha amri iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa
masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2) ya ibara hii litakuwa
batilifu.
SURA YA KUMI NA MOJA
MENGINEYO
Maelezo ya
mambo
yanayohusika na
madaraka ya
Kazi mbalimbali
zilizoanzishwa na
Katiba hii
Sheria za 1980
Na.1 ib.16; na
Sheria ya 1984
Na.15 ib.52
Sheria ya 1992
Na.4 ib.37
149.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote
iliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, Naibu
Waziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwa
mujibu wa madaraka ya kazi yake, aweza kujiuzulu kwa kutoa
taarifa iliyoandikwa na kutiliwa sahihi kwa mkono wake, kwa
kufuata masharti yafuatayo:
(a) iwapo mtu huyo aliteuliwa au alichaguliwa na mtu
mmoja, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu atawasilisha
kwa mtu huyo aliyemteua au aliyemchagua, au
iwapo aliteuliwa au alichaguliwa na kikao cha watu,
basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye
kikao hicho;
(b) iwapo mtu huyo ni Rais, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu
ataiwasilisha kwa Spika;
(c) iwapo mtu huyo ni Spika au Naibu wa Spika wa
Bunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha
kwenye Bunge; na
(d) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya
kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika.
(2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa masharti
ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, atahesabiwa kuwa amejiuzulu
tangu siku ile ambayo taarifa yake ya kujiuzulu itakapopokelewa
na mtu anayehusika au kikao kinachohusika na
itakapopokelewa na mtu yeyote aliyeruhusiwa kuipokea taarifa
hiyo na mtu anayehusika au kikao kinachohusika, lakini kama
taarifa hiyo ya kujiuzulu imeeleza kwamba mtu huyo atajiuzulu
tangu siku nyingine baada ya taarifa hiyo kupokelewa na mtu
anayehusika au kikao kinachohusika, basi mtu huyo
atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku hiyo nyingine ya
baadaye.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
106
(3) Iwapo mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote
iliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, Naibu
Waziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwa
mujibu wa madaraka ya kazi yake) amejiuzulu, basi ikiwa anazo
sifa zote zinazohitajika na kwa kila hali anastahili, aweza
kuteuliwa au kuchaguliwa tena kushika madaraka ya kazi hiyo
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(4) Masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (3) ya ibara hii
hayatamzuia mtu ambaye ni Rais kuchaguliwa tena kuwa Rais
wakati bado ameshika madaraka ya kazi ya Rais.
Maelezo kuhusu
utaratibu wa
kukabidhi
madaraka ya kazi
katika utumishi
wa Serikali
Sheria ya 1979
Na.14 ib.12
Sheria ya 1980
Na.1 ib.16 na
Sheria ya 1984
Na.15 ib.52
150.-(1) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya
Katiba hii kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka ya kazi
katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ifahamike
kuwa mtu yeyote mwenye mamlaka, kwa mujibu wa Katiba hii,
ya kumteua au kumchagua mtu mwingine kushika madaraka ya
kazi fulani anao pia uwezo wa kumteua au kumchagua kaimu
au mtu ambaye atashikilia kwa muda na kutekeleza madaraka
ya kazi hiyo:
Isipokuwa kwamba maelezo hayo hayatatumika kwa
madaraka ya kazi ya Waziri, Naibu Waziri, Jaji wa Mahakama
ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu, Mjumbe wa Tume ya
Kudumu ya Uchunguzi au Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
(2) Kanuni zifuatazo zitatumika pia kwa madhumuni ya
ufafanuzi wa masharti ya Katiba hii kuhusu utaratibu wa
kukabidhiana madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano, yaani:
(a) iwapo kuna mtu mwenye madaraka ya kazi fulani
aliyokabidhiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii
na mtu huyo yupo likizoni na wakati huo huo
anangojea kuacha kazi hiyo, basi anaweza kuteuliwa
mtu mwingine na kukabidhiwa madaraka ya kazi
hiyo, bila ya kujali kuwapo kwa yule mtu
anayengojea kuacha kazi hiyo;
(b) iwapo kuna watu wawili au zaidi ambao kwa wakati
mmoja wote wanashika madaraka ya kazi fulani
kutokana na uteuzi wao uliofanywa kwa mujibu wa
Kanuni iliyoelezwa katika
aya ya (a) ya ibara hii ndogo, basi katika hali hiyo
kukitokea haja ya kutekeleza shughuli yoyote
inayohusika na madaraka ya kazi hiyo yule mtu wa
mwisho kuteuliwa ndiye atakayehesabiwa kuwa mtu
pekee mwenye dhamana ya kazi hiyo;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
107
(c) iwapo mtu ameteuliwa, kwa mujibu wa masharti ya
Katiba hii, kuwa kaimu au kushikilia madaraka ya
kazi fulani wakati mtu maalum aliyeteuliwa kushika
madaraka ya kazi hiyo anashindwa kutekeleza
shughuli zinazohusika na kazi hiyo, basi
haitaruhusiwa kufanya uchunguzi wowote au kutoa
hoja yoyote juu ya uteuzi wa huyo kaimu eti kwa
sababu kwamba huyo mtu maalum aliyeteuliwa
kushika madaraka ya kazi hiyo anashindwa
kutelekeza shughuli zinazohusika na kazi hiyo.
Ufafanuzi Sheria
ya 1984 Na.15
ib.52 na 53
Sheria ya 1992
Na.4 ib.38
Sheria ya 2000
Na.3 ib.19
151.-(1) Katika Katiba hii, ila iwapo maelezo yahitaji
vinginevyo: "amri ya Jeshi" maana yake ni sheria au amri
iliyotolewa kwa mujibu wa sheria, ya kusimamia nidhamu katika
jeshi;
"askari" likitumika kuhusiana na jeshi lolote, maana yake ni
pamoja na askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri ya
jeshi hilo ni mtu anayewajibika kinidhamu;
"Baraza la Wawakilishi" maana yake ni Baraza la Wawakilishi,
la Zanzibar lililotajwa katika ibara ya 106 ya Katiba hii na
linalotekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii
na Katiba ya Zanzibar 1984;
"Bunge" maana yake ni bunge la Jamhuri ya Muungano
lililotajwa katika ibara ya 62 ya Katiba hii;
Sheria Na.5 ya
Mwaka 1992
"Chama cha Siasa" maana yake ni chama cha Siasa
kilichoandikishwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria ya
Vyama vya Siasa, ya Mwaka 1992;
"Idara ya Mahakama" maana yake ni kama ilivyofafanuliwa
katika ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 116 ya Katiba hii;
"Idara ya Mahakama ya Zanzibar" maana yake ni Idara ya
Mahakama inayojumlisha mahakama zote ambazo ziko katika
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
"Jaji Mkuu" maana yake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani
aliyetajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 115 ya
Katiba hii ambaye ameteuliwa kwa mujibu wa masharti
ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hiyo ya 118 au iwapo Jaji
Mkuu hayupo au anashindwa kutekeleza kazi zake kwa
sababu yoyote, Kaimu Jaji Mkuu aliyeteuliwa kwa mujibu
wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hiyo ya 118
ya Katiba hii, na kama Kaimu Jaji Mkuu naye hayupo au
anashindwa kutekeleza kazi za Jaji Mkuu, Jaji wa
Mahakama ya Rufani iliyepo kazini kwa wakati huo na
ambaye yuko kwenye daraja la juu zaidi la madaraka
kupita majaji wote wa Rufani waliopo;
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
108
"Jaji Mkuu wa Zanzibar" maana yake ni Jaji Mkuu wa
Mahakama Kuu ya Zanzibar ambaye, kwa mujibu wa
Katiba ya Zanzibar 1984, ndiye Mkuu wa Idara ya
Mahakama ya Zanzibar;
"Jeshi" maana yake ni lolote kati ya majeshi ya ulinzi na ni
pamoja na jeshi lolote jingine lililoundwa na Katiba hii au
kwa mujibu wa sheria na linalotawaliwa kwa amri ya
jeshi;
Sura 512;
"Jumuiya ya Madola" maana yake ni jumuiya ambayo
wanachama wake ni Jamhuri ya Muungano na kila nchi
ambayo inahusika na masharti ya ibara ya 7 ya Sheria ya
Uraia, ya mwaka 1961;
"kiapo" maana yake itabidi ifahamike kwa maana ya kawaida ya
neno hilo na ni pamoja na tamko rasmi la namna yoyote
linaloruhusiwa kisheria kutumiwa badala ya kiapo;
"kiapo cha uaminifu" maana yake ni kiapo cha kuwa mwaminifu
kwa nchi na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
"Maadili ya Kazi ya Jaji" maana yake ni masharti ya kimaadili
yanayoongoza mwenendo wa watu wafanyao kazi ya Jaji
au ya Hakimu;
"madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano" maana yake itabidi ifahamike kwa mujibu wa
maana ya kawaida ya maneno hayo na ni pamoja na
utumishi katika Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya
Muungano na katika Jeshi la Polisi au jeshi linginelo
lililoundwa kwa mujibu wa Sheria;
"mahakama" maana yake ni mahakama yoyote yenye mamlaka
katika Jamhuri ya Muungano isipokuwa mahakama
iliyoundwa kwa amri ya jeshi; lakini kwa ajili ya ibara ya
13, ya 14 na ya 15 za Katiba hii, itakuwa ni pamoja na
mahakama iliyoundwa kwa amri ya jeshi.
"Mahakama Kuu" maana yake ni Mahakama Kuu ya Jamhuri ya
Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar;
"Mambo ya Muungano" maana yake ni mambo yote ya umma
ambayo yametajwa na ibara ya 4 ya Katiba hii kuwa ni
Mambo ya Muungano;
"Mamlaka ya Nchi" ni pamoja na Serikali na Bunge la Jamhuri
ya Muungano, pamoja na Serikali na Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar;
"Mwanasheria Mkuu" maaana yake ni Mwanasheria mkuu wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano aliyetajwa katika ibara
ya 59;
"Serikali" maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au
Halmashauri ya Wilaya au ya Mji, na pia mtu yeyote
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
109
anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba
ya Serikali au Halmashauri;
"Serikali za Mitaa" maana yake ni vyombo vya kiserikali
vilvyoundwa kwa mujibu wa ibara ya 145 ya Katiba hii
kwa madhumuni ya kutekeleza madaraka ya umma;
"Tanzania Bara" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya
Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya
Tanganyika;
"Tanzania Zanzibar" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya
Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya
watu wa Zanzibar na ambalo kabla ya Sheria hii
kutungwa liliitwa Tanzania Visiwani;
"Uchaguzi Mkuu" au "uchaguzi unaofanywa na wananchi"
maana yake ni uchaguzi wa Rais na uchaguzi wa
Wabunge wanaowakilisha wilaya za uchaguzi
unaaofanywa baada ya Bunge kuvunjwa;
"Ujamaa" au "Ujamaa na Kujitegemea" maana yake ni misingi
ya maisha ya jamii ya kujenga Taifa linalozingatia
demokrasia, kujitegemea, uhuru, haki, usawam udugu na
umoja wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano;
"Waziri" maana yake ni Mbunge aliyekabidhiwa madaraka ya
kazi ya Waziri, isipokuwa Naibu Waziri, na maana hiyo
itatumika pia kwa Makamu wote wa Rais;
"Zanzibar" maana yake ni sawa na maana ya Tanzania
Zanzibar.
(2) Kanuni zifuatazo zitatumika kwa madhumuni ya
ufafanuzi wa masharti ya Katiba, yaani -
(a) kila yanapotajwa madaraka ya Rais, ifahamike kuwa
mdaraka yanayohusika ni pamoja na mamlaka ya
kutekeleza shughuli za kazi mbalimbali na vile vile
wajibu wa kutekeleza shughuli na kazi mbali mali
kama Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na
pia mamlaka mengine kama hayo au wajibu
mwingine kama huo ikiwa imeelezwa katika Katiba
hii au katika sheria nyingine yoyote kwamba
mamlaka hayo mengine ni ya Rais au kwamba
wajibu huo mwingine ni wa Rais;
(b) kila yanapotajwa madaraka ya kazi katika utumishi
wa Serikali, ifahamike kuwa kazi inayohusika ni kazi
katika Utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Mungano
isipokuwa kama imeelezwa vingine, na kila
inapotajwa Idara ya Serikali ifahamike kuwa idara
inayohusika ni idara ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, isipokuwa kama imeelezwa vingine;
(c) iwapo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii kuna
jambo lolote linalotakiwa litekelezwe au
lishughulikiwe na chama chochote cha siasa, basi,
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
110
lishughulikiwe na chama chochote cha siasa, basi,
jambo hilo litatekelezwa au litashughulikiwa na
chama hicho kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na
chama hicho kwa ajili hiyo, na pia kwa kuzingatia
masharti ya Katiba hii au Sheria yoyote iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo;
(d) kwa madhumuni ya Katiba hii, mtu hatahesabiwa
kuwa ana madaraka ya kazi katika utumishi wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa sababu tu
kwamba anapokea malipo ya uzeeni au malipo
mengine ya aina hiyo kwa ajili ya utumishi wake wa
zamani katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano au
katika Serikali yoyote ya zamani ya Tanzania Bara
au katika Jeshi la Ulinzi au la Polisi la Serikali ya
Jamhuri ya Muungano au Serikali ya zamani ya
Tanzania Bara au ya Zanzibar;
(e) katika Katiba hii, ila iwapo maelezo yahitaji vingine,
kila anapotajwa mtu mwenye dhamana ya kazi fulani
kwa kutaja madaraka ya kazi yake, ifahamike kuwa
mtu anayehusika ni pamoja na mtu yeyote ambaye ni
Kaimu au aliyeteuliwa kwa njia ya halali kushikilia
dhamana ya kazi hiyo;
(f) katika Katiba hii, kila yalipotajwa mamlaka ya
kumwondoa mtu katika madaraka ya kazi katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
ifahamike kuwa mamlaka yanayohusika ni pamoja na
mamlaka yaliyotolewa kwa mujibu wa masharti ya
Sheria yoyote yanayomtaka mtu huyo au
yanayomruhusu mtu huyo kustaafu:
Isipokuwa kwamba maelezo ya Kanuni hii
yasifahamike kuwa yanampa mtu yeyote mamlaka ya
kumtaka Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa
Mahakama Kuu au Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
astaafu;
(g) katika Katiba hii, kila ilipotajwa sheria ambayo
inabadilisha au kufuta sheria nyingine, ifahamike
kuwa sheria inayohusika ni pamoja na sheria
ambayo inarekebisha sheria hiyo nyingine au
ambayo inaendeleza kutumika kwa hiyo sheria
nyingine, ama bila mabadiliko au baada ya
kubadilishwa au kurekebishwa; au sheria ambayo
inaweka masharti mapya katika sheria nyingine.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
111
Jina kamili la
Katiba tarehe ya
kuanza kutumika
na matumizi ya
Katiba hii.
Sheria ya 1985
Na.15 ib.52
152.-(1) Jina kamili la Katiba ya Jamhuri ya Muugano wa
Tanzania, ya mwaka 1977.
(2) Katiba hii itaanza kutumika tarehe 26 Aprili, 1977.
(3) Katiba hii itatumika Tanzania Bara na vile vile
Tanzania Visiwani.
_________
NYONGEZA YA KWANZA
_________
(Imetajwa katika ibara ya 4)
Mambo ya Muungano
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
12. Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13. Leseni ya viwanda na takwimu.
14. Elimu ya juu.
15. Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16. Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17. Usafiri na usafirishaji wa anga.
18. Utafiti.
19. Utafiti wa hali ya hewa.
20. Takwimu.
21. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22. Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
yanayohusiana navyo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
112
__________
NYONGEZA YA PILI
___________
ORODHA YA KWANZA
(Imetajwa katika ibara ya 98 (1)(a))
(Sheria ambazo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na
heluthi mbili ya Wabunge wote).
Sura ya 500,
Sheria ya
kluthibitisha
Tanganyika
kuwa Jamhuri
ya mwaka 1962
Ibara ya 3, 17,18, 23 na 26
Sura ya 508,
Sheria ya
Utumishi katika
Idara ya
Mahakama ya
mwaka 1962
Ibara ya 22, 23, na 24
Sura ya 509,
Sheria ya
Utumishi
Serikalini ya
mwaka 1962
Ibara ya 22, 23, na 24.
Sura ya 512,
Sheria ya Uraia,
ya mwaka 1961
Sheria yote
Sura ya 557,
Sheria ya
Kuthibitisha
Mapatano ya
Muungano wa
Tanganyika na
Zanzibar ya
mwaka 1964
Sheria yote.
ORODHA YA PILI
(Imetajwa katika ibara 98 (1) (b))
Mambo ambayo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na
theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi
mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Visiwani.
1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.
2. Kuwapo kwa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.
3. Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
4. Kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
5. Madaraka ya Serikali ya Zanzibar.
6. Mahakama Kuu ya Zanzibar.
7. Orodha ya Mambo ya Muungano.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
113
8. Idadi ya Wabunge kutoka Zanzibar.
_____________