Thursday, January 31, 2013

JK- Tunajua biashara ya dini inalipa, lakini msiivuruge Tanzania


RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa mtindo wa kufanya fujo na kusababisha uvunjifu wa amani kwa visingizio vya dini nchini ni biashara inayolipa na ndiyo maana wakereketwa wa kufanya hivyo hawaishi.
Hata hivyo, akaonya kwamba Serikali katu haitawavumilia wanaotaka kuwavuruga Watanzania kwa kutumia dini zao.
Kikwete aliyasema hayo wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mchakato wa Nchi za Afrika Kujitathmini zenyewe katika nyanja za Demokrasia, Utawala Bora na Uchumi (APRM) nchini Ethiopia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema ni jambo la kushangaza kuona kuwa wadau wanatumia dini kuiyumbisha nchi kwa vigezo kuwa ni miongoni mwa nchi zilizodumisha amani kwa muda mrefu.
Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali yake haitayumba wala kusita kupambana ipasavyo na wafanya fujo hao ikiwa ni pamoja na kutumia njia za busara wakati wa kutoa uamuzi na hatua za kisheria.
“Kuna baadhi ya watu wanatumia vigezo vya kidini kwa ajili ya kufanya vurugu za kuhatarisha amani, Serikali haitaweza kuwavumilia, badala yake tutatumia njia mbalimbali ili kushughulikia matatizo hayo ikiwa ni pamoja na kutumia busara na hatua za kisheria,” alisema Kikwete.
Alisema mapendekezo yaliyotolewa na APRM ya kusimamia kwa uangalifu tofauti za kidini nchini ameyachukua kwa mikono miwili.
Alisema kitendo cha Tanzania kuwa na amani na utulivu kwa muda mrefu ni bahati iliyotokana na kutokuwapo kwa ugomvi wa kikabila, kidini ama yale ya kutokana na rangi za watu. Alisema hali hii inatokana na ukweli kuwa sera iliyopo haina ubaguzi kwa wananchi kwa misingi ya kabila, dini, rangi ama sehemu anakotoka Mtanzania, ni sera nzuri na wanaidumisha.
Kwa mujibu wa Kikwete, uzuri kuhusu dini katika Tanzania ni kwamba kila mmoja ana uhuru wa kuabudu na kwamba Serikali haina dini.
“Tunajua fika kuhusu hatari zinazoweza kusababishwa na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wenye malengo ya kuchochea fujo za kidini, hatuwezi kuyumba wala kusita kupambana ipasavyo na watu wa namna hiyo,” alibainisha.
Alisema ikiwa wataona uchochezi wa kidini unafikia kiwango cha kuhatarisha amani ya nchi ama uvunjifu wa amani na sheria na dola itachukua mkondo wake ili haki iweze kutendeka.

Mwananchi

Monday, October 22, 2012

UTARATIBU WA SHEREHE ZA EID EL ADH-HA LEICESTER UK


Assalaamu Alaykum Wapendwa katika Imani,

Kama mjuavyo, Inshaallah Eid El Adh-ha itasherehekewa Siku ya IJUMAA 26-10-2012
Ufuatao ni utaratibu wa Sherehe zetu hapa katika mji wa Leicester, Uingereza:

Inshaallah Sala ya Eid itasaliwa katika ukumbi wa Taylor Road School na kufuatiwa na Kifungua kinywa kwa utaratibu huu:
TAKBEER: Zitaanza Saa Mbili na Nusu asubuhi (8.30am)
SALA YA EID: Itasaliwa Saa Tatu Kamili asubuhi (9.00am)
PAHALA: Taylor Road School, Taylor Road, Leicester, LE1 2JP
KIFUNGUA KINYWA: Baada ya Sala Waumini watjumuika kama kawaida yetu kupata kifungua kinywa

PAHALA: 1st Floor, Kocha House, Malabar Road, Leicester, LE1 2PD

AN NOOR COMMUNITY LEICESTER
yakutakieni nyote
 MUBAARAK!!!

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi:
Mohammed Omar 07903978481, Abdul Dau 07792104495, Khamis Sahal 07982124581, Omar Hussein 07565512058

TANZANIA KUONDOKA KATIKA KUNDI LA NCHI MASKINI IFIKAPO 2015

Naibu Katibu Mkuu Mtendaji Ofisi ya Rais Kamisheni ya Tume ya Mipango, Bw. Clinfford K. Tandari, akifuatilia majadiliano yaliyohusu Utekelezaji wa Mpango wa Istanmbuli kwa nchi maskini maarufu kama LDGs. Mkutano huo ulifanyika nchini ya Kamati ya Pili ya Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa.

 Alipopata nafasi ya kuchangia utekelezaji wa Mpango huo ( Istambul Plan of Action) Bw. Tandari pamoja na mambo mengine, alisema Tanzania imekwisha kuuingiza mpango huo katika Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo wa Kila Miaka Mitano , lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania inaondoka katika kundi la nchi maskini na kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati ( Middle Income Countries), ikifikapo mwaka 2015.

Akabainisha kwamba ili kufikia hatua hiyo, Serikali imejiwekee vipaumbele kadhaa ambavyo vimeainishwa katika Mpango huo wa Miaka mitano. Akavitaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni Kilimo na Usalama wa Chakula, uboreshaji wa huduma za Elimu, Afya na huduma za maji na usafi wa mazingira, maendeleo ya miundombinu ikiwamo ya barabara, reli, bandari na huduma za nishati. 

Akavitaja vipaumbele vingine kuwa ni usawa wa kijinsia na uwezeshashi pamoja na kujenga mazingira bora ya biashara na ushindaji wa kibiashara. Katika hatua nyingine Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Rais Kimisheni ya Mipango alieleza kwamba Tanzania ingeweza kufikia lengo lake la kutoka katika kundi la nchi maskini na kuwa kundi la nchi ambazo uchumi wake ni wakati kabla hata ya mwaka 2015 ikiwa tu washirika wa maendeleo ya kichumi watatekeleza ahadi zao za kuisaidia Tanzania zikiwamo zile walizotoa miaka mingi ya nyuma na ambazo hazijatekelezwa hadi sasa. 

Hata hivyo akasema Tanzania imejidhatiti katika kuhakikisha kwamba inaboresha makufanso ya mapato yake ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa kodi na kuibua vyazo vipya vya mapato ili kuziba pengo litokanalo wa wadau wa maendeleo kushindwa kutekeleza ahadi zao. 

Wednesday, August 29, 2012

BENKI YA KCB TANZANIA IMETOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI TANO (5M) KCMC...!!!


Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya makabidiano ya hundi yenye thamani ya shilingi 5m/- kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa  vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC. Kulia ni na Kaimu mkurugenzi wa hospitali  Profesa Raimos Olomi na kushoto ni mkurugenzi wa utawala wa hospitali hiyo Stanley Mmbaga

Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau akimkabidi mfano wa hundi ya shilingi 5m/- kwa Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC {kulia} Profesa Raimos Olomi kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa  vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC.
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (kushoto)  akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 5m/- mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga. Fedha zilizotolewa zinalenga kusaidia ununuzi wa  vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali. Katika kati ni  Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC Profesa Raimos Olomi
Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC rofesa Raimos Olomi akiifurahia hundi ya shilingi 5m/-iliyotolewa na Benki ya KCB kusaidia ununuzi wa  vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC. Kushoto ni Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau
Mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga akitoa maelezo kwa Emmanuel Grayson ambaye ni mkuu wa masuala ya kijamii wa Benki ya KCB tawi la moshi juu ya wodi iliyokarabatiwa na benki hiyo mwaka jana mara baada ya kutoa msaada wa wa 5m/- kusaidia ununuzi wa  vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo. 
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza na Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC {kushoto} Profesa Raimos Olomi na Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya akina mama Dkt  Gileard Masenga (kulia) mara baada ya kutoa msaada wa 5m/- kusaidia ununuzi wa  vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo. 

---
Na Mwandishi Wetu
Benki ya ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa shilingi milioni tano (5m) kusadia ununuzi wa vifaa katika wodi ya akina mama katika hospitali ya rufaa KCMC ikiwa ni jitihada za kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika kwa akina mama wajawazito.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya fedha hizo uliofanyika hospitali hapo jana, Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau alisema kuwa msaada huo ulikuwa ni muendelezo wa msaada ambao benki hiyo iliutoa mwaka jana.

Mwaka jana tulikarabati chumba cha akina mama wagonjwa hatuti kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni kumi na moja. Nilipofamishwa kuwa chumba kilikuwa tayari lakini hakuna vifaa niliona kuna umuhimu kutoa msaada wa kununulia vifaa ili pesa iliyotolewa kwanza isiwe imepotea bure,” alieleza.

Meneja huyo wa tawi alisema kuwa Benki yake imeamua kutoa msaada huo kwa kutambua umuhimu wa kusaidia serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuhakikisha kuwa malengo ya millennia ya kuhakikisha kuwa vifo vya akina mama na mtoto vinakwisha kufikia mwaka 2015.

Akipokea msaada huo, Kaimu mkurunzi wa hospital ya KCMC Profesa Raimos Olomi alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto katika hospitali hiyo kutokana.

Vifo vya akina mama na watoto hapa nchini bado ni vingi. Jitihada kubwa zinahitajika kuvipunguza. Kupitia misaada ya wadau mbalimbali kama huu wa Benki ya KCB lengo linaweza kufikiwa. Tunaishukuru sana Benki ya KCB kwa msaada huu muhimu.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake hospitalini hapo Dr Gileard Masenga alisema kuwa hospitali hiyo haikuwa na wodi ya akina mama mahututi na kuongeza kuwa msaada huo utasadia kuokoa maisha ya akina mama na watoto.

Mwanzoni tulikuwa tunalazimika kuwapeleka akina mama kwenye hodi za wagonjwa hahututi ambazo wagonjwa wote wanatibiwa. Tunaamini msaada huo utasaidia kuboresha hali na hivyo kuokoa wakina mama wengi zaidi. Tunaishukuru Benki ya KCB kwa kuwekeza katika afya ya mama na mtoto,” alifafanua  
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------




By Staff reporter
KCB Bank Tanzania, has donated 5m/-to Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) in Moshi to facilitate the procurement of equipments for women Intensive Care Unit (ICU)
Speaking during the cheque handing over ceremony held at the hospital yesterday, KCB Bank branch manager for Moshi Lomnyaki Saitabau said, the donation was continuation of donation that the bank issued to the hospital last year.

“Last year we donated over 11m/- to facilitate the renovation of women ICU room. When I asked and informed that the room was ready but it was not in as there was no required equipments I felt that there was a need to provide support again so that the first donation to be meaningful,” he elaborated.

The branch manager noted that, KCB decided to support maternal health at the hospital to complement the government efforts to reduce maternal death that can be prevented and the realization of Millennium Development Goal (MDG) number 4 to reduce maternal death by 2015.

This donation is not very big but I believe it can make a significant difference by saving the needy women who die because of lack of enough facilities to save their lives and that of their new born,” he said.

KCMC acting director Professor Raimos Olomi said, the donation was a big push to the hospital adding that it would help to save lives of women and their new born who die as a result of pregnancy complications.

“There still a lot of maternal death incidences here in Tanzania. In order scale down the deaths, a lot is to be done if the death rate is to be done and this requires support from different stakeholders. Today, KCB has once again shown its true commitment to save the women and children. We are grateful to this important support,” he said.

On his side, the head of Obstetric and Gynecology Dr Gileard Masenga said, the hospital had no special ICU room dedicate for women with pregnancy complications stressing that the donation would make a difference.

“At the beginning women with pregnancy complications had to use the general ICU room. We believe this donation would facilitate to procure some of the required equipments and thus assist to save lives of women and their new born. We are grateful to KCB Bank for investing in women health,” he said.

Wednesday, July 25, 2012

BREAKING NUUUUUUUZ: AJALI MBAYA IMETOKEA MUDA MCHACHE ULIO PITA INASEMEKANA ASKARI KAMA WANNE WAFARIKI PAPO HAPO


Hii ni ajali ya gari dogo la police ilikua imebeba maabusu imepata ajali mbele tu kidogo ya chalinze, kama nusu saa iliyopita na askari kam 4 hivi wamefariki hapo hapo,,.nawengine wapo hoi saana!!..Mungu azipumzishe roho za marehem, pema peponi..AMEEN

“ JAMAN MADEREVA MWENDOKASI HATARI JAMANI MTATUUA“
Chanzo: Blog ya Malecela


Wednesday, May 30, 2012

Tanzania ni Salama kwa Watalii

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALI


TAARIFA KWA UMMA

Kufuatia vitendo vya vurugu zilizozuka hivi karibuni katika maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar baada ya mitandao ya kimataifa imekuwa ikiripoti taarifa za kuwepo kwa hali ya wasiwasi kwa watalii wanaotaka kuja kutembelea Visiwa hivyo.

Kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Utalii, ningependa kuwahakikishia wageni, ambao tayari wako nchini, na wale ambao wanajiandaa kuja, kuwa vurugu hizo ambazo zimeshadhibitiwa na Serikali hazikuathiri utalii. Mjini Zanzibar pamoja na maeneo ya vivutio vya utalii kote nchini.

Hadi hivi leo napotoa taarifa hii, amani imetawala Mji Mkongwe Zanzibar na hakuna taarifa yoyote ya uharibifu wa maeneo ya vivutio vya utalii vya Zanzibar wala kuchomwa kwa hoteli ama kudhulika kwa raia yeyote wa kigeni. Hivyo nasisitiza kuwa Zanzibar nisehemu salama kwa watalii. 

Vilevile, Siku chache kabla ya tukio la Zanzibar, kulikuwa na matukio manne ya watalii kuporwa katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Uporaji huo ulitendwa na watu waliokuwa kwenye magari au pikipiki ambao waliwapora watembea kwa miguu.

Serikali inawahakikishia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya pekee na ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya pekee na ya kupita na hatua zimechukuliwa na Jeshi la Polisi kuongoza usalam kwa wakazi na watalii.

Nachukua fursa hii kuwahakikishia wageni kwamba kila juhudi zimechukuliwa kuhakikisha kuwa usalama wa watalii unadumishwa pamoja na faraja wakati watakapotembelea Tanzania.

Daima tukumbuke kuwa, Tanzania ni kisiwa cha amani na nchi imenuia kudumisha sifa hiyo nzuri. 

Karibu Tanzania.

Mhe. Lazaro Nyalandu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
30 Mei, 2012

Tuesday, May 29, 2012

MEDIA BRIEFING NOTE FOR THE GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP DIALOGUE TO BE HELD IN DAR ES SALAAM, TANZANIA – 24TH TO 28TH MAY, 2013



Tanzania
will host the next Smart Partnership Dialogue that is scheduled to take
place from 24th to 28th May, 2013 in Dar es Salaam. President Jakaya
Mrisho Kikwete, is  expected  to officiate the  National launch at noon
 today Tuesday May 29, 2012 at the Karimjee Hall grounds in Dar es
salaam.
President
Kikwete had agreed to host the event  during the last dialogue that
took place in Putrajaya, Malaysia in June, 2011  -  branded the Langkawi
International Dialogue.
The
Smart Partnership Dialogues are a brainchild of the Commonwealth
Partnership for Technology Management. The CPTM which is the social and
scientific interlinkage arm of the Commonwealth, has since 1995
undertaken in collaboration with willing national partners to provide a
forum that cuts across the east-west, have, have not’s and the developed
and developing dichotomy for the discussion of topical subjects in a
conducive inclusive, open dialogue. Inspired by the increasing need to
ensure a win-win interrelationship between actors, the CPTM, in
collaboration with the host country undertake to provide an ambient
setting where individuals from all walks of life and professions can
meet and hold serious discourse on selected subjects every two years.
To ensure that these dialogues are successful, a two pronged approach is utilized. The first is
when the host country convenes a National Dialogue. This involves the
gathering together of different sectors of the host community and coming
up with a topical issue that is not just locally relevant, but which
resonates internationally and merits a grander discourse and focus. The second is
when the Host country in collaboration with the CPTM plan for, invite
participants and hold an international open dialogue on the selected
topic, in essence, host aSMART DIALOGUE.
As
hosts, the kicking off of the National Dialogue is very crucial. It is a
means for creating National and International awareness of the next
host of the Dialogue and avails the opportunity to announce the dialogue
venue, topic and dates.
The Launch of the National Campaign for the Dialogue in Tanzania will take place on the 29th May, 2012 at the Karimjee Hall Grounds from 10:00 am to 11:00 am. The
Host and Patron Advisor for the 2013 |Smart Partnership Dialogue, H.E.
Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania will
officially launch preparations for the 2013 Dialogue and introduce the
Theme for the Dialogue (Leveraging Technology for Africa’s Socio-Economic Transformation) announce the date for the Dialogue (24th to 28th May, 2013) and the venue (Dar es Salaam) issue
a holistic invitation to both the citizens of Tanzania as well as the
International Community at large, and share his vision for the Dialogue.
The Dialogue has been branded the GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP DIALOGUE in
anticipation of interest the chosen theme is likely to raise.
Technology is a global phenomenon, a global concern, a global topical
issue. It is therefore more than likely that a Dialogue on Technology
for development shall merit global attention and have a global
audience/participation.
The
Execution of the preparation will be undertaken under the guidance of
the Chief Secretary who is the Convener of the Dialogue. The Chief
Secretary will be supported by a National Steering Committee that
comprises of Permanent Secretaries from All Ministries as well as
Representatives of Keyline Sectors both on Mainland Tanzania and
Zanzibar.
A
Focal Point Team from the Ministry of Foreign Affairs will spearhead
the logistical and liaising activities necessary for the successful
execution of the Dialogue. The Team will over time incorporate Members
from different Links
A
Resource Group with an Advisory role comprising of key members of the
Academia, Business and Corporate Community, Youth, Labour, Culture,
Industry and Media has been set up under the leadership of Professor
Samuel Wangwe.
Following
the National Launch, the next step is scheduled to be contact with
different Links within Tanzania who will in turn be linked with
counterparts interested in participating in the Dialogue in 2013. A
National Dialogue to discuss the theme will follow thereafter.
Other
African countries that have hosted the Smart Partnership Dialogues
include Botswana, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Mozambique, Swaziland,
Lesotho and Uganda that has hosted it twice. Other countries include
Barbados, and Malaysis that has hosted the dialogue nine times.
 Issued by
THE FOCAL POINT TEAM, GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP DIALOGUE,  MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION

Monday, May 28, 2012

Neno La Leo: Jambo La Zanzibar Ni Letu Bara, Lakini....



Ndugu zangu,

MFALME Suleiman aliambiwa ndotoni aombe kitu chochote kwa Mola wake, naye akajibu; “ Ewe Mola wangu, nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili ili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya, maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?” Hivyo basi, Mfalme Suleiman aliichagua hekima. Maana, ni Mfalme Suleiman huyo anayekaririwa na vitabu vya dini akitamka, kuwa; “ Watu wangu wanaangamia kwa kukosa hekima”.

Naam, hekima ndilo jambo lililo bora kabisa kwa mwanadamu kuwa nalo. Mwanadamu aliyepunguwa hekima ana hasara kubwa maishani. Hekima ni tunu na kipaji ambacho Mwenyezi Mungu amewajalia waja wake, ili nao waweze kupambanua na kuamua kati ya yalo mema na maovu. Duniani hakuna shule ya hekima.

Zimetufika habari; Zanzibar kuna moto unawaka. Si moto wa kuupuza. Hekima inatuongoza katika kutambua, kuwa ukiupuuzia moto unaowaka kwenye nyumba ya jirani yako, basi, nyumba yako pia imo hatarini kuungua . Naam, ndio sababu ya kusema; Jambo la Zanzibar ni letu.

Ndio, ni letu hata sie tulio bara. msiba wa Unguja ni msiba wetu. Hivyo, kadhia hii ya Zanzibar ni kadhia yetu. Ni wakati sasa wa kutanguliza busara na hekima katika kutanzua kadhia hii. Hoja ya msingi inasemwa kuwa ni suala la Muungano. Mengine ni makandokando yanayotokana na hoja ya msingi. Basi, tuujadili Muungano, kisha tuone kama kuna lingine. Maana, hata bila Muungano wa Serikali moja, sisi bado ni ndugu na majirani wa daima na milele. Tujadili basi aina iliyo bora ya Muungano ili tuendelee kushirikiana kama ndugu.

Binafsi nilifika Zanzibar kwa mara ya kwanza mwaka 1988 ( pichani). Nilikuwa kijana mdogo sana. Zanzibar ndio kisiwa cha kwanza kupata kukitembelea. Tangu hapo niliipenda Zanzibar, nimefika Zanzibar mara kadhaa. Wenyeji ni wakarimu sana. Lakini, ukweli ni huu, tangu safari yangu ya kwanza Unguja miaka hiyo, wenyeji walinikumbusha, tena kwa kutamka kwa vinywa, kuwa mimi ni ' Mtanganyika'- mtu wa mlima. Hivyo, kwangu mimi, hoja ya Muungano nimeionja kwa karibu tangu mwaka 1988 nikiwa Zanzibar.

Si jambo jema wala la kistaarabu kwa watu wachache kule Zanzibar kuchoma moto makanisa, baa na biashara za watu wa kutoka upande wa pili wa Muungano, lakini, vitendo hivi viovu vinavyopaswa kukemewa kwa nguvu zote haviwezi kumalizwa kwa nguvu za kipolisi au kijeshi, bali kwa kuzikutanisha pande zinazotofautiana kwenye meza ya mazungumzo.

Kwa hatua iliyopo sasa, bado Wazanzibari wenyewe wanaweza kukaa chini na kujadiliana kwa uwazi namna ya kwenda mbele. Lililo muhimu ni kuhifadhi amani na utulivu uliokuwepo.

Tayari kinachotokea Zanzibar kimeshakuwa na athari mbaya kiuchumi na kijamii. Kijamii, kuna mbegu za chuki zinapandwa. Ni jambo la hatari. Siku zote , chuki huzaa chuki, silaha huzaa silaha na hatimaye kupelekea uvunjivu wa amani wa muda mrefu.

Katika dunia ya sasa ya teknolojia ya upashanaji habari, habari za uvunjivu wa amani Zanzibar zimeshasambaa duniani kote kama moshi wa kifuu. Watalii wa dunia wanataadharishwa sasa kutokwenda Zanzibar. Tunajua , baada ya kushuka kwa soko la karafuu, asilimia kubwa ya uchumi wa Zanzibar inatokana na mapato kwenye sekta ya utalii. Kadhia hii itapelekea kushuka kwa biashara ya utalii Zanzibar na hivyo kushuka kwa mapato.

Na mfano rahisi wa jinsi Mzanzibar wa kawaida atakavyoathirika, ni pale atakapoambiwa na wenye mahoteli asisitishe kupeleka samaki wake kwa vile wageni watalii wamehadimika. Na kuna vijana wengi wa Zanzibar ambao kipato chao kinategemea sana shughuli za utalii. Nao watakosa cha kufanya, na mapato pia. Mazingira hayo huchangia kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu. Na hasira pia ya wananchi, naam, midomo yenye njaa ni midomo yenye hasira.

Kadhia ya Zanzibar inaweza pia kuathiri uchumi wa Bara hasa kwenye eneo hilo la utalii ukiachilia maeneo mengine. Mfano, kuna watalii wanaokuja Bara wakiwa na mipango ya kuunganisha safari zao hadi Zanzibar. Kama Zanzibar hakuendeki na bara hakutaendeka pia. Hivyo, hata mapato ya bara yanayotokana na biashara ya utalii yatapungua.

Naam, huu si wakati tena wa kutanguliza propapanda. Ndio, propaganda iwekwe kando na diplomasia ichukue nafasi yake; mazungumzo, mazungumzo, mazungumzo. Ndicho kinachohitajika sasa. Pande mbili zinazokinzana ziwe kwenye mazungumzo hadi zifikie muafaka ulio na maslahi kwa jamii pana.

Huu si wakati wa kutafuta mshindi, maana, hata tulipofikia sote tumeshashindwa. Ni wakati wa kutanguliza busara na hekima. Na maamuzi mengine tunayotakiwa kuyafanya sasa yasitokane na mazoea ya siku nyuma bali uzoefu mpya tunaoupata sasa.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,
Iringa.

0788 111 765
http://mjengwablog.com

Sentensi 6 za Zitto Kabwe juu ya vurugu za Zanzibar





 1.Vurugu za Zanzibar ni ‘unwanted distractions’ katika mchakato wa kuandika katiba mpya.

2. Hakuna namna vitendo hivyo vinaweza kuhalalishwa na kutetewa lakini ni matokeo ya muda mrefu ya ‘superficial attempts at dealing against group  with ulterior motives.

3. Rais Ali MohamedShein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti vurugu hizo,na kuanza mzungumzo na pande zote.Hiki sio kitendo cha kudharau kabisa.

4. Muungano wetu ni sacred na tumetoka mbali kushindwa sasa kuulinda, ‘not when we are so close at having an everlasting formula’.

5. Waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara moja. Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache kutuingiza katika vurugu za kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa.

6. Zanzibar Political leaders and public opinion makers must engage the Zanzibaris into a serious and objective dialogue about the future of Zanzibar within or outside the Union.

Wakili maarufu afariki Dunia



MKURUGENZI Msaidizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo (44) ‘Jembe’ amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi alilithibishia Tanzania Daima jana asubuhi kutokea kwa kifo hicho ambapo alisema bado ofisi yake na taifa limepata pigo kubwa lakuondokewa na gwiji hilo la uendeshaji wa mashitaka hususani ya jinai hapa nchini na kwamba mchango wake mzuri katika uendeshaji wa kesi hususani za jinai hautasaulika na utaenziwa. 

Dk.Feleshi alikuwa akizungumza na gazeti hili kwa uzuni alisema Jumamosi jioni Boniface ambaye pia alikuwa Msimamizi wa Uendeshaji wa Kesi zenye maslahi kwa umma, aliingia Dar es Salaam, akitokea Moshi kwaajili ya kutoa mafunzo ya jinsi ya uendeshaji wa mashitaka kwa maofisa wa Idara ya Uhamiaji akiwa mwenye afya njema na alirejea nyumbani kwake Kinondoni lakini ilipofika usiku wa siku hiyo hali yake ilibadilika ghafla na kukimbizwa katika Hospitali ya Regency kwaajili ya matibabu. “Baada ya kufikishwa hospitalini hapo alifariki dunia ila mimi kama kiongozi wake wa kazi kwa sasa siwezi kusema chanzo cha kifo hicho hadi pale tutakapopata taarifa rasmi za madaktari na msiba upo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mtaa wa Sinza Load Kitalu Na.4 na hadi kufikia leo utaratibu shughuli za msiba zitakuwa zimefahamika na tutawajulisha”alisema Dk.Feleshi. 

Dk.Feleshi alimuelezea Boniface kuwa ni miongoni mwa mawakili wa serikali waliokuwa wakijitoa kwa moyo wao wote katika kuitumikia serikali yao katika uendeshaji wa kesi bila woga na katika kuthibitisha hilo ni katika kesi za mauji yaliyoibuika miaka ya nyumba mkoani Mbeya ambapo watu walikuwa wakiwachunya binadamu wenzao ngozi, kesi za wizi wa fedha za EPA, matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuongeza kuwa marehemu alikuwa akitumia taaluma yake kwa kuwapatia watu wengine waliokuwa wakiitaji. 

Miongoni mwa kesi kubwa ambazo mwandishi wa habari hizi amekuwa akimshuhudia akiziendesha kwa zaidi ya miaka mitano katika mahakama mbalimbali hapa nchini sasa ni kesi ya wizi wa shilingi bilioni 1.8 katika EPA, iliyokuwa ikimkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 23 mwaka jana, iliwahukumu kwenda jela miaka mitano, kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la TBC, Jerry Murro na wenzake ambapo Murro alishinda kesi hiyo mwaka jana, kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabishara Jayankumar Patel “Jeetu Patel’ na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na Reginal Mengi iliyokuwa akitaka afutiwe kesi zake nne za EPA zilizopo katika mahakama ya Kisutu kwasababu Mengi alimuhukumu kabla ya hajahukumiwa na mahakama kwa sababu alimuita ni Fisadi Papa, ambapo Boniface alimwakilisha AG na DPP na aliibuka mshindi katika kesi hiyo.

Kesi nyingine kubwa ambayo marehemu alikuwa akiziendesha ambazo bado hadi umauti unamkuta hazijatolewa hukumu ni ile ya mauji ya Ubungo Mataa ambayo inaendelewa kusikilizwa na Jaji Projestus Rugazia, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomwona mfanyabiashara Naeem Gile ambayo inasikilizwa mbele ya Jaji Laurence Kaduri ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya kufua umeme ya Richmond LCC, kuwa hana kesi ya kujibu, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu iliyomuona Jerry Murro hana hatia na kesi ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 inayomkabili waliokuwa mawaziri wa Fedha na Nishati, Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja. 

Boniface alizaliwa Februali 21 mwaka 1968 ameacha mke na watoto watatu, aliitimu shahaha ya kwanza ya Sheria mwaka 1995 na shahada ya pili ya sheria alimaliza mwaka 2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Julai Mosi mwaka 1995 aliajiriwa rasmi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kama Wakili wa Serikali, ilipofika Oktoba Mosi mwaka 2006 alipandishwa cheo na kuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi.Oktoba Mosi mwaka 2007 alipandishwa cheo tena na kuwa Wakili Kiongozi wa Serikali.

Nyadhifa ambazo Boniface aliwahi kuzishika enzi za uhai wake ni kati ya mwaka 2003-2007 alikuwa ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Mbeya.Kati ya Mei 2007 na Oktoba 2010 alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Mwanza.Novemba 2009 hadi Novemba 2010 alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa Serikali mkoani Dar es Salaam. Kutokana na utendaji kazi wake mzuri ilipofika Desemba 2010 hadi mauti yanamkuta aliteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia awaka Msimamizi wa uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake liimidiwe. 

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatatu, Mei 28 mwaka 2012.

Friday, May 25, 2012

DKT.BILAL AMWAKILISHA RAIS KATIKA MKUTANO WA MAENDELEO ENDELEVU AFRIKA JIJINI GABORONE, BOTSWANA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akihutubia kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo Endelevu katika Bara la Afrika mjini Gaborone.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Rais wa Liberia Bibi Ellen Johnson Sirleaf kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo Endelevu Barani Afrika mjini Gaborone.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi pamoja na wawakilishi  kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa Maendeleo Endelevu katika Bara la Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dkt. Mohammed Gharib Bilal amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Maendeleo Endelevu Afrika unaolenga katika kujumuisha thamani ya Rasilimali Asilia katika kupima maendeleo ya kiuchumi katika nchi za Afrika.
Katika mkutano huo, Tanzania imeunga mkono kuanzishwa kwa mfumo wa kujumuisha thamani ya raslimali asilia ambao utahusishwa kwenye tathmini ya pato la taifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na  vijavyo.
Makamu wa Rais alisema wakati akihutubia mkutano huo leo Alhamis Mei 24, 2012 kuwa, mchango wa rasilimali asilia zina nafasi kubwa katika kuchangia katika pato la taifa lakini ili mchango wake utambulike, nchi zinahitajika kuwa na utaratibu wa kuzifanyia tathmini hasa kuhusu matumizi yake na faida zake katika uchumi huku pia athari zake zikitazamwa hasa zile zinazotokana na kupoteza uhalisia wa mazingira ama kuharibu mazingira ya nchi.
“Ni imani ya serikali ya Tanzania kuwa mpango huu utasaidia kutoa nafasi ya nchi kujikagua hasa kwa kuzingatia rasilimali zinazotumika na faida inayopatikana. Tena mpango huu utatoa nafasi kwa nchi kujiuliza kama matumizi ya rasilimali zake yanalenga kutambua faida ya sasa na siku zijazo ili kuhakikisha kuwa mazingira yanabakia kuwa salama kwa ajili ya vizazi vijavyo,” anasema Mheshimiwa Makamu wa Rais Katika hotuba yake.
Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, dhana ya kutathmini mazingira na kujumisha raslimali asilia kwenye hesabu za pato la taifa, kunaweza kusaidia nchi kufikia maamuzi ambayo yataliwezesha taifa kupata maendeleo endelevu hali ambayo itachangia jitihada za kupunguza umaskini na kukuza uchumi.
“Tathmini ya hesabu kuhusu maendeleo, ukijumuisha na hesabu za raslimali asilia, zinaweza zikatupa takwimu za kina kwa ajili ya kusimamia vizuri uchumi,” anaeleza Makamu wa Rais na kuongeza:
“Tena kwa upande mwingine, hesabu za mapato katika sekta za maji, nishati na nyinginezo, udhibiti wa uchafu wa mazingira na hali kadhalika matumizi makubwa ya raslimali zinahitajika ili kukuza uchumi na wakati huo huo zikitakiwa kufanyiwa tathmini ya faida zake na hasara kwa mazingira na hali ya nchi katika miaka ijayo.”
Katika mkutano huo, pia kumejadiliwa suala la umuhimu wa serikali za nchi za Afrika kutazama  upya sera na mikakati ya nchi hizo na kuweka  mikakati inayolenga katika kutunza mazingira ambayo itawezesha kupata maamuzi ya busara  yatakayohakikisha upatikanaji wa maendeleo endelevu.
Dkt. Bilal anaueleza mkutano huo kuwa, Tanzania iliona umuhimu wa raslimali asilia tangu nchi ilipopata uhuru mwaka 1961 ambapo iliweza kutenga asilimia 30 ya eneo la nchi kwa ajili ya wanyama na viumbe hai. Tena ziliwekwa sera nzuri zilizolinda uvunaji wa raslimali hizo kwa manufaa ya taifa.
“Dunia hivi leo inakabiliwa na matumizi yasiyo endelevu ya raslimali asilia. Tumemaliza benki ya raslimali asilia kwa kuwa matumizi yamekuwa makubwa zaidi kwenye uvuaji wa samaki, uvunaji wa misitu, hewa iliyopo na vingine vingi vilivyobaki. Mbaya zaidi, tumekuwa tukitumia vibaya raslimali hizo wakati zaidi ya watu bilioni moja wanaishi katika umaskini uliokithiri, “ anasema
Makamu wa Rais ameueleza mkutano huo pia kuwa, nchi nyingi za Afrika zinategemea kilimo kama njia kuu ya uchumi na sekta hii bado inategemea mvua huku ikihusisha wakulima wadogo wadogo hali ambayo inaonesha ma mazingira yataharibiwa ni wazi maisha ya wengi yataathirika. Anasisitiza kuhusu kuwepo kwa mfumo mpya wa kilimo unazingatia kutoharibu rasilimali asilia na wakati huo huo kuhakikisha kuwa mazingira yanabaki kama yalivyo ili yasaidie jamii zijazo.
Akifungua mkutano huo, Rais Seretse Khama Ian Khama wa Botswana alisema nchi yake imeandaa mkutano huo kwa lengo la kutaka kuzungumzia masuala ya Afrika kwa pamoja juu ya maendeleo endelevu na kuangalia namna nchi hizo zinavyoweza kutumia utajiri wa raslimali za asili katika kukuza maendeleo ya nchi zao.
Katika mkutano huo, Tanzania na Botswana zimepongezwa kwa uhifadhi wa maliasili na mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadaye.
Mkutano huo wa pia unahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nchi zipatazo 11 wakiwemo Marais Hifikupenye Pohamba wa Namibia, Bibi Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Waziri Mkuu wa Msumbiji na nchi .
Mkutano huu ni maandalizi ya mkutano wa Mazingira wa Rio +20 unaotarajiwa kufanyika nchini Brazil mwezi ujao katika jiji la Rio de Janeiro. Maazimio ya mkutano huu yanalenga nchi za Afrika kushiriki mkutano huo zikiwa na sauti moja kuhusu utunzaji wa mazingira na pia kukabiliana na tabia ya uharibifu mkubwa wa mazingira hasa unaofanywa na nchi tajiri duniani.
 Imetolewa na:  Kitengo cha Habari
                 Ofisi ya Makamu wa Rais
              Alhamisi – 24/5/2012   

Taswira Zaidi Za Marais Wastaafu Nane wa Nchi za Afrika Wanaokutana nchini Afrika Kusini Kwa Siku Tatu

Pichani shoto ni   Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akichangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,mapema leo jioni,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya kumbi ya   chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini.Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na mwisho ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo.
 Pichani kulia ni Rais mstaafu wa Benin,Nicéphore Dieudonné Soglo akifafanua jambo kwa makini wakati wa mchakato wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ulipokuwa umepamba moto jioni ya leo,katika mkutano uliofanyika kweny moja ya kumbi ya   chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo mchana,Pichani kati ni Rais mstaafu Pedro Pires wa Cape Verde na   Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamini Mkapa
Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,ambaye pia ni Mratibu mkuu wa mkutano akifafanua jambo kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Mkutano huo mapema leo mchana.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
Baadhi ya Marais Wastaafu kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa kwenye mkutano wa kujadili   maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
 Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
Pichani juu na chini Mkutano wa kujadili   maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika ukiendelea ndani ya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo mchana.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Tanzania,Mh Benjamini Mkapa akijadiliana jambo na Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin walipokuwa wakiwasili kwenye viunga vya vya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika
 Pichani  mbele ni Marais Wastaafu wa Tanzania,Ally Hassan Mwinyi na  Benjamin Mkapa sambamba  na  Marais wengine wakiwasili katika viwanja vya chuo  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.
 Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakijadiliana jambo nje ya ukumbi,kabla ya kuanza kwa Mkutano huo,Shoto ni Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications),Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper), Muondosha Mfanga (The Guardian).
 Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kutoka nchini Tanzania,wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa  kikuu cha  Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini mapema leo kwa ajili ya kuripoti mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.Shoto ni Yvonne Msemembo (ITV) ,Joseph Kulangwa (Tanzania Standard News Paper),Nestor Mapunda,Absolom Kibanda (Free Media),Mzee Theophili Makunga (Mwananchi Communications), Muondosha Mfanga (The Guardian) pamoja na Deus Mjatta (ITV).
Baadhi ya wanafunzi kutoka vyo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,ambao umewashirikisha Marais Wastaafu nane wa Afrika.Picha Zote na Ahmed Michuzi-Johannesburg
---
Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wamekutana jana jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kufanya mkutano wa siku tatu ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.



Marais wastaafu hao waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania, Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin, Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania, Rais Joaquim Chissano wa Msumbiji, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Rais Rupiah Banda wa Zambia.



Aidha - mbali ya Marais hao waliohudhuria mkutano huo, pia ulihudhuriwa na  Wataalam mbalimbali wa nishati, viongozi wa umma na sekta binafsi na wanafunzi na kitivo kutoka vyuo vikuu 9 vya kimataifa kikiwemo chuo kikuuu mwenyeji cha Witwatersrand a.k.a Wits. Tanzania iliwakilishwa na wanafunzi watano na walimu wawili kutoka chuo kikuu cha Dar-es-Salaam.



Mratibu mkuu wa mkutano huo - Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadiliana juu ya ufumbuzi wa mageuzi ya nishati katika nchi za Kiafrika, na kuhakikisha nchi za Afrika zinajiwakilisha vyema katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala zima la Nishati. Balozi Stith alisema kuwa mkutano huo utaleta mshikamano wa pamoja kwa viongozi wa sekta ya nishati na wafadhili mbalimbali wa miradi mbalimbali, ili kuhakikisha nishati hiyo inatosheleza mahitaji ya Afrika kwa ujumla. Mkutano huo wa siku 3 utafikia tamati Mei 25.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII:SHERIA HAIRUHUSU VIBALI KUUZWA KWENYE SHAMBA LA SAO HILL

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
--
 SHERIA HAIRUHUSU VIBALI KUUZWA KWENYE SHAMBA LA SAO HILL
Wizara ya Maliasili na Utalii inafafanua kuwa uvunaji wa Miti katika Shamba la Sao Hill unafuata utaratibu uliowekwa kisheria.
Sheria ya Misitu haimzuii mwananchi yeyote kuvuna mazao ya misitu kutoka kwenye misitu ya asili au ya kupandwa mradi awe amefuata sheria na taratibu zilizopo katika nyaraka husika, na hakuna nyaraka yoyote inayoagiza kwamba vibali vya uvunaji vigawiwe kwa viongozi ama watumishi wa serikali ili waviuze.


Ufafanuzi huu unatolewa kufuatia habari zilizoandikwa na gazeti moja kuwa vigogo wa Maliasili ndiyo wanaochukua vibali na kuviuza kwa wateja. Habari hiyo haina msingi maana utaratibu unaotumika unatekelezwa kwa uwazi na unajulikana kwa wateja wa mazao ya misitu.
Shughuli za uvunaji wa mazao ya misitu hufanywa kwa kufuata ‘Mwongozo wa Uvunaji Endelevu na Biashara ya Mazao ya Misitu’ wa mwaka 2007, ambao unaonyesha taratibu muhimu za kufuatwa katika shughuli za uvunaji na biashara ya mazao ya misitu.


Mwongozo huo unatokana na Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 na Sheria ya Misitu Namba 14 ya mwaka 2002, pamoja na Matangazo ya Serikali (Government Notices) Namba 69 na 70 ya mwaka 2006.


Shughuli za ugawaji wa mazao ya kuvuna katika kila shamba la Serikali hufanywa na Kamati ya Ugawaji Mazao ya Misitu ya sehemu husika.


Utaratibu uliopo ni kuwa mwananchi anayehitaji mazao kutoka katika misitu ya mbao laini, kama ile ya Sao Hill, hupeleka maombi yake kwa Meneja wa shamba linalohusika, kuanzia Januari 1 hadi tarehe 30 Aprili kila mwaka. Maombi hayo yanatakiwa yapokelewe mapema maana Kamati ya Ugawaji hufanya kikao chake mwezi Juni kila mwaka.
Aidha mwongozo wa uvunaji unaotumika hivi sasa unatanabaisha kuwa kipaumbele kitatolewa kwa mwombaji mwenye kiwanda lakini sio lazima awe na kiwanda.


Hata hivyo, taratibu hizo za uvunaji zimefanyiwa marekebisho yatakayoanza kutumika mwaka ujao wa fedha ambapo mwombaji sasa atalazimika kuwa na kiwanda ili aweze kupata kibali. Utaratibu huu ulitangazwa kwenye vyombo vya habari na tovuti ya Wizara www.mnrt.go.tz.


Katika utaratibu huo mpya Wizara itandaa utaratibu maalumu wa kuhakikisha wanavijiji wanaopakana na misitu ya serikali inayovunwa wananufaika na misitu hiyo kwa kuwa wanachangia kuilinda.


George Matiko
MSEMAJI WA WIZARA
Tarehe 24 Mei 2012
Simu - 0784 468047