Tuesday, August 30, 2011

HOT NEWS ...LUDEWA WAANDAMANA KWA MBUNGE KUILALAMIKIA BENKI YA NMB


Na Francis Godwin
Wananchi wa jimbo la Ludewa ambao ni wateja wa benki ya NMB tawi la Ludewa wametinga nyumba kwa mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe wakitaka awasaidie kuishtaki benki hiyo kwa madai ya upotevu wa fedha zao katika mazingira tata.
Agnesi Mapunda ni mtumishi wa Halmashauri ya Ludewa idara ya ardhi ambaye ni mteja wa benki hiyo mwenye akanti namba 6012400990 NMB tawi la Ludewa ambaye alidai kuwa akaunti yake ilikuwa na fedha zaidi ya shilingi milioni 1 ila mwezi wa sita alikuta akaunti hiyo ikiwa na salio la shilingi 144,000 pekee na baada ya kuuliza aliambiwa fedha zake zimetolewa kwa huduma ya pesa fasta na NMB Mobel huduma ambayo kwa upande wake hajawahi kuitumia toka awe mteja wa benki hiyo.
Hata hivyo alisema baada ya kuhoji sana ndipo benki hiyo ilipoamua kuchunguza suala hilo na kubaini majina ya watu waliohamisha fedha hizo na kuwa hadi sasa suala hilo lipo polisi linafanyiwa kazi.
Huku baadhi ya wateja wakienda benki hapo na polisi kutaka kufunga akanti zao na kuhama uteja na benki hiyo .
Mbunge wa jimbo hilo Filikunjombe amekili kupokea malalamiko hayo na kuwa tayari amewasiliana na meneja wa kanda na meneja wa benki hiyo ili kutolea ufafanuzi suala hilo.





No comments: