Picha ya mfano wa Maharusi. |
Na Francis Godwin, Iringa
Bwana harusi mmoja mkazi wa Makete mkoani Iringa jina na (picha za harusi yake vimehifadhiwa) ametoa kali ya mwaka baada ya kufunga ndoa na mwenzi wake na kisha kugoma kata kata kuingia ukumbini kumalizia sherehe ya ndoa yao, kwa madai kuwa Bibi harusi aliyefunga naye ndoa si chaguo lake na kuwa hajazoea kutazamwa na watu wengi kiasi hicho. Bwana harusi huyo ambaye ni mmoja kati ya wafanyabiashara maarufu katika mikoa ya kusini mwa Tanzania, alitoa kali hiyo baada ya 'MC' wa sherehe hiyo kuwaingiza ukumbini wasimamizi wa harusi hiyo 'Maflowers' na wacheza shoo na ilipofika zamu ya maharusi kuingia ukumbini.
Bwana harusi huyo aligoma kata kata kuingia ukumbini jambo lililosababisha mabaunsa waliokuwa katika kamati ya harusi hiyo kuingilia kati na kutaka kumpa kichapo bwana harusi huyo na kujaribu kutaka kumuingiza kwa nguvu ukumbini kwa kuivuruga sherehe hiyo. Hata hivyo muda wote bibi harusi na ndugu wa maharusi hao ambao walikuwa wameingia ukumbini muda wote machozi yalikuwa yakiwatoka kutokana na hatua ya bwana harusi kugoma kuingia ukumbini . Kutokana na vuta nikuvute kati ya MC, mabaunsa na bwana harusi, Bwana harusi huyo ambaye alikuwa chakali kwa kilevi cha pombe alitoa masharti na sharti la kwanza kati ya aliyoyatoa Bwana harusi huyo, alitaka taa zote zilizomo ukumbini humo zizimwe ndipo aweze kuingia ukumbini.
Baada ya kutekelezwa kwa sharti hilo, harusi hiyo iliendelea kama kawa japo Bwana harusi hakuacha kutoa vituko kila alipotakiwa kufanya jambo ukumbini humo.
No comments:
Post a Comment