Thursday, August 11, 2011

CHADEMA Wapiga mkutano Arusha Leo



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hii leo kimefanya mkutano mkubwa jijini Arusha ambapo kimetoa ufafanuzi juu ya maamuzi yake kuwavua uanachama waliokuwa Madiwani wa chama hicho.
Picha kutoka Jamii Forums 
=====

Wakazi wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha, wakimsikiliza mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chadema, Godbless Lema alipohutubia mkutano wa hadhara kulaani kuadimika kwa mafuta ya petroli na mgao wa umeme unaondelea nchini, mkutano ulioambatana na ufunguaji wa matawi ya Chama hicho. Picha na Silvan Kiwale
--
SHUGHULI mbalimbali zikiwamo za kiuchumi na kijamii katika baadhi ya mitaa ya jiji la Arusha, jana zilisimama kwa muda wakati misafara mirefu iliyojaa mbwembwe za kila aina ya magari, pikipiki, baiskeli na mikokoteni iliyofungwa bendera za Chadema, ilipopita kwenye kata nne ambazo zilikuwa zikiongozwa na madiwani kiliowatimua uanachama hivi karibuni.

Ziara hiyo ya kwanza ya viongozi wa juu wa Chadema imekuja siku chache baada ya Kamati Kuu (CC) ya chama iliyokutana Mjini Dodoma kati ya Agosti 5 na 6, kuamua kuwafukuza uanachama madiwani wake watano kutokana na madai ya kuingia muafaka na CCM na TLP katika nafasi ya umeya wa jiji hilo Juni 20, mwaka huu bila ridhaa ya uongozi wa taifa.Kwa habari zaidi bofya na Endelea....>>>>>

No comments: