MPOKI NGOLOKE
MAELEZO-DAR ES SALAAM
WATU wawili wamekutwa wamefariki dunia , katika maeneo ya mtaa wa Kiziza kata ya Kibada Wilaya ya Temeke baada ya kudumbukia kwenye kisima cha maji na kukwama wakati wakitoa vifaa vyao vya kuchimbia walivyovisahau .
Tukio hilo limetokea Agosti 10, mwaka huu, majira saa 1:30 jioni katika mtaa wa Kiziza kata ya Kibada mkoani Temeke kati watu hao mmoja alitambuliwa kwa jina moja tu la Said na aliyekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 na mwingine aliyejulikana kwa jina la Frank Mnyaru ambaye umri wake haukuweza kufahamika mara moja .
Akielezea tukio hilo Kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Temeke, David Misime alisema Said alienda kwenye kisima kuchukua vifaa walivyokuwa navitumia kuchimbia kisima hicho kilichokuwa kinamilikiwa na Mohammed Juma(70),mmiliki huyo alipoona Said hatoki ndani kwa muda mrefu baada ya kuzidiwa na maji yaliyokuwamo ndani , aliomba msaada kwa mafundi wenzake waliojulikana kwa majina ya Zakayo Saimon(30) mkazi wa Mgindoni Mjimwema pamoja na Mnyaru.
Baada ya Mnyaru na Zakayo kuingia kisimani ili kumuokoa Said waliishiwa hewa ambapo Mnyaru alifariki dunia na Saimon alifanikiwa kuokolewa na kikosi cha zimamoto na askari polisi, ambao pia waliopoa miili ya marehemu hao.
Hatahivyo Saimon aliokolewa huku akiwa amepoteza fahamu na alipelekwa hospitalini.
Kamanda Misime ya marehemu hao wamehifadhiwa katika hospitali ya Vijibweni , iliyopo Kigamboni
No comments:
Post a Comment