CHAMA cha demokrasia na maendeleo (chadema) wilaya ya Iringa mjini kimetangaza rasmi zoezi la uchukuaji fomu ambalo limeanza Agosti 17 mwaka huu hadi agosti 20 huku kikitamba kuchukua kata hizo mbili zilizoachwa wazi na madiwani wa CCM waliofariki dunia.
Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima alisema hayo wakati akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusiana na maandalizi ya chama hicho katika mchakato wa kuwania udiwani kwenye kata hizo za Miyomboni na Gangilonga.
Alisema kuwa zoezi la utoaji fomu kwa wagombea limeanza toka Agosti 17 mwaka huu na siku ya jumamosi Agosti 20 itakuwa ni siku ya mwisho kwa wanachama waliochukua fomu kurejesha fomu zao ofisi za chadema kata husika.
Hata hivyo alisema wote wenye sifa ya kuwania udiwani wanaomba kujitokeza kuchukua fomu hizo zinazotolewa kwa shilingi 10,000 pekee kwa kila fomu na kuwa baada ya wanachama kurudisha fomu hizo vikao husika vya mchujo kwa wagombea vitakaa na kuchuja waghombea wake.
Katibu huyo alitamba kuwa pamoja na kata hizo kabla ya kuachwa wazi zilikuwa zikiongozwa na madiwani wa CCM Abubakar Mtamike kwa kata ya Gangilonga na Mariamu Nyangiywa kwa kata ya Miyomboni ambao wote walifariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu ,alisema kuwa lazima Chadema wapokee urithi huo kwa CCM.

Habari na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment