Saturday, August 20, 2011

JAMII JIJINI MBEYA YATAKIWA KUTAMBUA KUWA MAJI YATOKAYO KATIKA MAMBOMBA MAPYA SI SALAMA


Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mbeya imehitadharisha jamii juu ya matumizi ya maji yanayotoka kwenye mabomba mapya yaliyowekwa hivi karibuni na kwamba maji hayo si salama kwa matumizi ya binadamu.



Afisa uhusiano wa maji safi na maji taka jijini Mbeya Marry Sayula amesema licha ya tatizo la maji safi jijini hapa jamii haitakiwi kutumia maji hayo kwa matumizi ya nyumbani

Wakati huohuo amesema uhaba wa maji jijini Mbeya unachingiwa kwa kiasi kikubwa titizo la mgao wa umeme kwenye mitambo ya kusukuma maji.

Hivi karibuni baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji safi ikiwa ni pamoja na kutumia maji kutoka kwenye mito ambayo si salama kwa matumizi ya binadamu na kwamba inashauriwa kuwa unapotumia maji hayo unatakiwa kuyachemsha.

No comments: