Saturday, August 20, 2011

TAASISI YA USTAWI WA JAMII YAAJIRI WAHADHIRI WAPYA 18, CHUO KUFUNGULIWA JUMATATU



Siku
kadhaa baada ya Wahadhiri wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii jijini Dar es
Salaam kusitishiwa ajira zao kwa sababu ya kusababisha mgomo usio halali
ili kuushinikiza uongozi kutekeleza madai yao mbalimbali ikiwemo
kuwaongezea mishahara, uongozi wa chuo hicho kupitia Bodi ya Magavana
umeajiri wahadhiri wapya 18 ili kufidia pengo hilo.

Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo Bw
MWANDE MADIHI amethibitisha suala hilo na kuongeza kwamba wahadhiri hao
wapya wataanza kazi rasmi baada ya chuo hicho kufunguliwa Agosti 22
mwaka huu.

Katika hatua nyingine uongozi huo
pia umewaomba wanafunzi wa chuo hicho kutoa ushirikiano kwa wahadhiri
hao wapya na kuwaahidi kutojirudia kwa mgogoro uliojitokeza ili kuleta
maendeleo kwa taasisi na taifa kwa ujumla.


No comments: