SERIKALI Iringa yaingilia kati sakata la ufisadi wa mkataba feki wa uwindaji katika mradi wa wa Hifadhi ya Mali Hai (Mbomipa) unaoundwa na vijiji 22 vya Tarafa za Idodi na Pawaga, vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, wilayani Iringa kwa kuivunja Halmashauri kuu ya Mbomipa baada ya kudaiwa kuhusika na ufisadi wa shilingi milioni 50 katika maradi huo.
Taarifa za ndani ya Mbomipa zinadai kuwa serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Iringa kepten mstaafu Aser Msangi katika kikao chake cha pamoja na bodi na Halmashauri kuu ya Mbomipa kilichokiti wiki iliyopita katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo ilibaini kuwepo kwa ufisadi huo wa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 ambazo hazikuingizwa katika akaunti ya Mbomipa huku viongozi wa Halmashauri ya Mbomipa wakidaiwa kuizunguka bodi ya wadhamini na kusaini mkakata na mwekezaji kinyume na katiba ya Mbomipa.
Mmoja kati ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya Mbomipa ambaye hakupenda kutaja jina lake alidai kuwa viongozi wa Halmashauri hiyo ambao wameondolewa madarakani ili kupisha uchaguzi mpya ulipangwa kjufanyika ndani ya wiki mbili kuanzia sasa ,kuwa viongozi hao walikuwa wakiendesha mradi huo kwa maslahi yao na kuwatumia wajumbe wa vijiji vya Pawaga ambavyo ni miongoni mwa vijiji jirani vya maradi huo vinavhyonufaika na mradi ili kujiwekea uhalali wa kuungwa mkono kama njia ya kuendeleza ufisadi ndani ya mradi huo.
Hata hivyo alisema kuwa katibu wa Halmashauri kuu ya Mbomipa Josephat Kisangage na makamu mwenyekiti wake Mashauri Msavi walisafiri kwa ndege kwenda Arusha kwa mwekezaji kwa ajili ya kusaini mkataba feki ,mkataba uliopaswa kusainiwa na bodi bila hata wajumbe wa Halmashauri kuu ya Mbomipa kujulishwa zaidi ya kupewa taarifa baada ya kurejea kuwa wameingia mkakaba na mwekezaji wa kampuni ya Marera.
Mjumbe huyo kutoka Idodi anadai kuwa wajumbe kutoka Pawaga ndio ambao walikuwa wakiiunga mkono mkataba huo feki pamoja na viongozi hao ambao katika kikao cha Halmashauri kuu kilichofanyika Nzihi viongozi hao walipania kuivunja bodi ya wadhamini kwa baada ya kuibua ufisadi wa shilingi milioni 50.
Alisema kuwa njama za viongozi wa Halmashauri kuu kutaka kuvunja bodi hiyo ziligonga mwamba baada ya mwanasheria wa wilaya kuingilia kati na kupinga uamuzi huo kwa madai kuwa mwenye haki ya kuvunja bodi ni msajili wa serikali kwa mujibu wa katiba na si vinginevyo.
Pia alisema kuwa mbali ya hatua iliyofikiwa na mkuu wa wilaya ya kuivunja Halmashauri hiyo bado wizara ya maliasili iliifutia kibali kampuni ya Marera kuendelea kufanya kazi ya uwindaji katika mradi huo wa Mbomipa.
Aidha alisema katika kikao hicho kilichohudhuliwa na madiwani wa kata ya Mlowa ,Itunundu, Mlenge na Ilolompya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri ,mkuu wa wilaya aliweza kutoa maamuzi hayo kama njia ya kuepusha mwanya wa ufisadi kuendelea ndani ya Mbomipa.
Hata hivyo katibu bodi ya Wadhamini wa Mbomipa, Michael Filiakosi alikili kuvunjwa kwa Halmashauri hiyo na kudai kuwa uwindaji haramu unaofanywa katika eneo la Mkupula ambalo lilikuwa chini ya kampuni ya Marera ndio umepelekea hata wanyama katika eneo hilo kupungua huku viongozi wa Halmashauri kuu wakiendelea kusaini mikataba feki.
Filiakosi alisema mradi huo ambao upo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za utalii , upigaji wa picha wa wanyama waliomo kwenye hifadhi hiyo na uwindaji umeendelea kupoteza mwelekeo wake
Alisema baadhi ya watu waliokuwa wamenunua vitalu katika hifadhi hiyo, wamevitumia vibaya baada hasa kwa vitendo vya kuwaua wanyama kiholela na kusababisha idadi yao kupungua.
Katibu huyo wa Mbomipa, vitendo hivyo vimesababisha kupungua kwa idadi ya watalii waliokuwa wakitembelea hifadhi hiyo kubwa nchini .
Alisema wanyama kama Nyati ,simba, tembo na swala sasa wamepungua kwa kiwango kikubwa katika hifadhi ya Ruaha na hii imesababishwa na uwindaji haramu unaotetewa na Halmashauri kuu ya Mbomipa.
Alisema kuwa mbali ya uwindaji haramu ila bado hata malengo ya Mradi huo ulianzishwa kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa vijiji 22 vya mradi huo ,bado yametoweka na badala yake kuwa mradi wenye kuwanufaisha zaidi viongozi wachache wa Halmashauri kuu ya Mbomipa
Hata hivyo alipongeza hatua ya serikali ya wilaya ya Iringa chini ya mkuu wa wilaya kwa kuivunja Halmashauri hiyo na kuwa bila uamuzi huo mradi huo ungeweza kufa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stevin Mhapa alisema kuwa hatua ya mkuu wa wilaya imelenga kujenga mradi huo na kuendelea kunufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa na kuwa kwa sasa wanasubiri kuundwa kwa Halmashauri mpya itakayofanya kazi kwa misingi iliyowekwa.
........................Itaendelea ...........................
Habari kwa hisani ya Francis Godwin
No comments:
Post a Comment