Wachezaji wa Yanga kutoka (kushoto) Julius Mlope, Rashid Gumbo na Nurdin Bakar. |
Viingilio katika mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya mabingwa watetezi Yanga na Makamu Bingwa Simba itachezwa kesho katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ambapo viingilio vitakuwa ni kama ifuatavyo:-
Viti vya bluu sh. 5,000, Viti vya kijani sh. 7,000, Viti vya rangi ya chungwa sh. 10,000, VIP C sh. 20,000, VIP B sh. 25,000 na VIP A sh. 50,000.
Tiketi zimeanza kuuzwa leo mchana (Agosti 15 mwaka huu) kwenye vituo vyote vya mafuta vya Big Bon jijini Dar es Salaam. Pia zinauzwa katika baadhi ya vituo vya Oilcom na TSN.
LIGI DARAJA LA KWANZA
Ligi ya Taifa ngazi ya Fainali imemalizika jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga. Timu zilizofanikiwa kupanda daraja la kwanza kwa kuongoza makundi yao ni Polisi Central ya Dar es Salaam, Mlale JKT ya Ruvuma na Mgambo Shooting ya Tanga. Timu zilizopanda kama washindwa bora ni Samaria ya Singida na Small Kids ya Rukwa.
Usajili kwa ajili ya timu za daraja la kwanza utafanyika kuanzia Agosti 15 mwaka huu hadi Septemba 15 mwaka huu. Jumla ya timu 18 zitashiriki ligi inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa Septemba mwaka huu. Taarifa rasmi ya tarehe ya kuanza ligi hiyo itatolewa baadaye.
Timu nyingine za Daraja la Kwanza ni Temeke United ya Temeke, Polisi (Iringa), Burkina Faso (Morogoro), Polisi (Morogoro), Rhino Rangers (Tabora), Polisi (Tabora), 94 KJ (Green Warriors) ya Kinondoni, Tanzania Prisons (Mbeya), Morani (Manyara), Transit Camp (Temeke), Rhino FC (Mbeya), Majimaji (Songea) na AFC (Arusha).
Manyema Rangers ya Ilala, Nyerere FC ya Kilimanjaro na Mwanza United ya Mwanza ndizo zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Taifa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Kumbukumbu ya mchezo wa watani hao wa Jadi uliopita. |
Kikosi cha Simba. |
Amir Maftah wa Simba (kulia) akichuana na Taita wa Yanga, katika mchezo uliopita, Je kesho nani kuibuka kidedeA??? Libeneke kwa Hisani ya Sufiani Mafoto |
No comments:
Post a Comment