Monday, October 22, 2012

TANZANIA KUONDOKA KATIKA KUNDI LA NCHI MASKINI IFIKAPO 2015

Naibu Katibu Mkuu Mtendaji Ofisi ya Rais Kamisheni ya Tume ya Mipango, Bw. Clinfford K. Tandari, akifuatilia majadiliano yaliyohusu Utekelezaji wa Mpango wa Istanmbuli kwa nchi maskini maarufu kama LDGs. Mkutano huo ulifanyika nchini ya Kamati ya Pili ya Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa.

 Alipopata nafasi ya kuchangia utekelezaji wa Mpango huo ( Istambul Plan of Action) Bw. Tandari pamoja na mambo mengine, alisema Tanzania imekwisha kuuingiza mpango huo katika Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo wa Kila Miaka Mitano , lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania inaondoka katika kundi la nchi maskini na kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati ( Middle Income Countries), ikifikapo mwaka 2015.

Akabainisha kwamba ili kufikia hatua hiyo, Serikali imejiwekee vipaumbele kadhaa ambavyo vimeainishwa katika Mpango huo wa Miaka mitano. Akavitaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni Kilimo na Usalama wa Chakula, uboreshaji wa huduma za Elimu, Afya na huduma za maji na usafi wa mazingira, maendeleo ya miundombinu ikiwamo ya barabara, reli, bandari na huduma za nishati. 

Akavitaja vipaumbele vingine kuwa ni usawa wa kijinsia na uwezeshashi pamoja na kujenga mazingira bora ya biashara na ushindaji wa kibiashara. Katika hatua nyingine Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Rais Kimisheni ya Mipango alieleza kwamba Tanzania ingeweza kufikia lengo lake la kutoka katika kundi la nchi maskini na kuwa kundi la nchi ambazo uchumi wake ni wakati kabla hata ya mwaka 2015 ikiwa tu washirika wa maendeleo ya kichumi watatekeleza ahadi zao za kuisaidia Tanzania zikiwamo zile walizotoa miaka mingi ya nyuma na ambazo hazijatekelezwa hadi sasa. 

Hata hivyo akasema Tanzania imejidhatiti katika kuhakikisha kwamba inaboresha makufanso ya mapato yake ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa kodi na kuibua vyazo vipya vya mapato ili kuziba pengo litokanalo wa wadau wa maendeleo kushindwa kutekeleza ahadi zao. 

No comments: