Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya makabidiano ya hundi yenye thamani ya shilingi 5m/- kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC. Kulia ni na Kaimu mkurugenzi wa hospitali Profesa Raimos Olomi na kushoto ni mkurugenzi wa utawala wa hospitali hiyo Stanley Mmbaga
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau akimkabidi mfano wa hundi ya shilingi 5m/- kwa Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC {kulia} Profesa Raimos Olomi kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC.
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 5m/- mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga. Fedha zilizotolewa zinalenga kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali. Katika kati ni Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC Profesa Raimos Olomi
Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC rofesa Raimos Olomi akiifurahia hundi ya shilingi 5m/-iliyotolewa na Benki ya KCB kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC. Kushoto ni Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau
Mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga akitoa maelezo kwa Emmanuel Grayson ambaye ni mkuu wa masuala ya kijamii wa Benki ya KCB tawi la moshi juu ya wodi iliyokarabatiwa na benki hiyo mwaka jana mara baada ya kutoa msaada wa wa 5m/- kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo.
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza na Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC {kushoto} Profesa Raimos Olomi na Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya akina mama Dkt Gileard Masenga (kulia) mara baada ya kutoa msaada wa 5m/- kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo.
---
---
Na Mwandishi Wetu
Benki ya ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa shilingi milioni tano (5m) kusadia ununuzi wa vifaa katika wodi ya akina mama katika hospitali ya rufaa KCMC ikiwa ni jitihada za kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika kwa akina mama wajawazito.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya fedha hizo uliofanyika hospitali hapo jana, Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau alisema kuwa msaada huo ulikuwa ni muendelezo wa msaada ambao benki hiyo iliutoa mwaka jana.
Mwaka jana tulikarabati chumba cha akina mama wagonjwa hatuti kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni kumi na moja. Nilipofamishwa kuwa chumba kilikuwa tayari lakini hakuna vifaa niliona kuna umuhimu kutoa msaada wa kununulia vifaa ili pesa iliyotolewa kwanza isiwe imepotea bure,” alieleza.
Meneja huyo wa tawi alisema kuwa Benki yake imeamua kutoa msaada huo kwa kutambua umuhimu wa kusaidia serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuhakikisha kuwa malengo ya millennia ya kuhakikisha kuwa vifo vya akina mama na mtoto vinakwisha kufikia mwaka 2015.
Akipokea msaada huo, Kaimu mkurunzi wa hospital ya KCMC Profesa Raimos Olomi alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto katika hospitali hiyo kutokana.
Vifo vya akina mama na watoto hapa nchini bado ni vingi. Jitihada kubwa zinahitajika kuvipunguza. Kupitia misaada ya wadau mbalimbali kama huu wa Benki ya KCB lengo linaweza kufikiwa. Tunaishukuru sana Benki ya KCB kwa msaada huu muhimu.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake hospitalini hapo Dr Gileard Masenga alisema kuwa hospitali hiyo haikuwa na wodi ya akina mama mahututi na kuongeza kuwa msaada huo utasadia kuokoa maisha ya akina mama na watoto.
Mwanzoni tulikuwa tunalazimika kuwapeleka akina mama kwenye hodi za wagonjwa hahututi ambazo wagonjwa wote wanatibiwa. Tunaamini msaada huo utasaidia kuboresha hali na hivyo kuokoa wakina mama wengi zaidi. Tunaishukuru Benki ya KCB kwa kuwekeza katika afya ya mama na mtoto,” alifafanua
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
By Staff reporter
KCB Bank Tanzania, has donated 5m/-to Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) in Moshi to facilitate the procurement of equipments for women Intensive Care Unit (ICU)
Speaking during the cheque handing over ceremony held at the hospital yesterday, KCB Bank branch manager for Moshi Lomnyaki Saitabau said, the donation was continuation of donation that the bank issued to the hospital last year.
“Last year we donated over 11m/- to facilitate the renovation of women ICU room. When I asked and informed that the room was ready but it was not in as there was no required equipments I felt that there was a need to provide support again so that the first donation to be meaningful,” he elaborated.
The branch manager noted that, KCB decided to support maternal health at the hospital to complement the government efforts to reduce maternal death that can be prevented and the realization of Millennium Development Goal (MDG) number 4 to reduce maternal death by 2015.
This donation is not very big but I believe it can make a significant difference by saving the needy women who die because of lack of enough facilities to save their lives and that of their new born,” he said.
KCMC acting director Professor Raimos Olomi said, the donation was a big push to the hospital adding that it would help to save lives of women and their new born who die as a result of pregnancy complications.
“There still a lot of maternal death incidences here in Tanzania. In order scale down the deaths, a lot is to be done if the death rate is to be done and this requires support from different stakeholders. Today, KCB has once again shown its true commitment to save the women and children. We are grateful to this important support,” he said.
On his side, the head of Obstetric and Gynecology Dr Gileard Masenga said, the hospital had no special ICU room dedicate for women with pregnancy complications stressing that the donation would make a difference.
“At the beginning women with pregnancy complications had to use the general ICU room. We believe this donation would facilitate to procure some of the required equipments and thus assist to save lives of women and their new born. We are grateful to KCB Bank for investing in women health,” he said.
No comments:
Post a Comment