Thursday, July 28, 2011

LATEST NEWS: MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA WANORWAY WALIOLIPULIWA NA BOMU

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Mdogo wa Norway nchini Tanzania, Svein Baera, baada ya kuwasili kwenye ofisi za ubalozi huo zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutia saini Kitabu cha Maombolezo, kufuatia tukio la kuripuliwa kwa bomu kulikofanyika nchini Norway wiki hii na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70. Katikati ni Balozi Mdogo wa ubalozi huo anayehusika na masuala ya Utawala, Tom Elversather.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, nje ya Ofisi ya Ubalozi wa Norway, wakati alipofika kwa ajili ya kutia saini Kitabu cha Maombolezo ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa Bomu uliotokea wiki  hii nchini Norway na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70. Katikati ni Balozi Mdogo wa Norway nchini Tanzania Svein Baera.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo katika ofisi za Ubalozi wa Norway nchini, kufuatia vifo vya watu zaidi ya 70 waliofariki kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea wiki hii nchini humo. Katikati ni Balozi Mdogo wa Norway nchini, Svein Baera (kulia) ni Balozi Mdogo anayehusika na masuala ya Utawala, Tom Elvesather
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: