Mama Salma Kikwete kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Utawala
wa Africa Diana White na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya Kimarekani
wanaofanya kazi Tanzania kwenye masuala ya afya na lishe, baada ya mkutano
wa pamoja tarehe 18-05-2012.
Mkuu wa Utawala wa Africare Bi. Diana White akitoa taarifa ya
utekelezaji wa shughuli za Africare nchini Tanzania kuanzia mwaka 1994
walipofungua ofisi zao nchini Tanzania kwenye Mkutano na Mama Salma
Kikwete alipotembelea ofisi hizo tarehe 18-05-2012.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi maelezo kuhusu WAMA Mkuu waUtawala wa Africare Bi. Diana White kama ishara ya kuanzisha ushirikiano
na taasisi hiyo ili kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji kuhusu masuala
ya lishe Tanzania.
Mama Salma Kikwete na ujumbe wake wakiangalia mfano wapicha za matunda za ukutani zinazoelezea umuhimu wa matunda na mboga kwa
afya ya mtoto.
Picha Juu na chini ni Profesa Jerome Paulsen, Daktari naMkurugenzi wa Children's Hospital Global Affairs akizungumza na ujumbe wa
Mama Salma Kikwete kuhusu mpango wa Hospitali hiyo ya kuwafundisha
madaktari kuhusu magonjwa ya watoto yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.
Dkt Hadija Mwamtemi, Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili akizungumzia umuhimu wa kushirikiana na Pediatric Association
of Tanzania ili kujenga uwezo wa madaktari wa watoto Tanzania ili
kuwakinga watoto na magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafuzi wa
mazingira.
Mama Salma Kikwete akimsikiliza Dkt Nasra Nirza, daktari
bingwa wa watoto wa Hospitali ya National Children kuhusu huduma wanayotoa
kwa watoto wanaolazwa kwenye hospitali hiyo. Pembeni ya Mama Salma ni Dkt.
Hadija Mwamtemi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili alieyeongozana na Mama
Kikwete kwenye ziara hiyo.
Picha juu na chini ni Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo alipokuwa kwenye mkutanona wenyeji wake wa Hospitali ya Watoto National Children baada ya
kutembelea maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
Juu na chini ni Mama Salma Kikwete akiwakabidhi wadau mbalimbali maelezokuhusu WAMA kama ishara ya kuanzisha ushirikiano na taasisi hiyo ili
kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji kuhusu masuala ya afya ya msingi kwa
watoto wa Tanzania.
Picha na Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC
No comments:
Post a Comment