JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALI
TAARIFA KWA UMMA
Kufuatia vitendo vya vurugu zilizozuka hivi karibuni katika maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar baada ya mitandao ya kimataifa imekuwa ikiripoti taarifa za kuwepo kwa hali ya wasiwasi kwa watalii wanaotaka kuja kutembelea Visiwa hivyo.
Kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Utalii, ningependa kuwahakikishia wageni, ambao tayari wako nchini, na wale ambao wanajiandaa kuja, kuwa vurugu hizo ambazo zimeshadhibitiwa na Serikali hazikuathiri utalii. Mjini Zanzibar pamoja na maeneo ya vivutio vya utalii kote nchini.
Hadi hivi leo napotoa taarifa hii, amani imetawala Mji Mkongwe Zanzibar na hakuna taarifa yoyote ya uharibifu wa maeneo ya vivutio vya utalii vya Zanzibar wala kuchomwa kwa hoteli ama kudhulika kwa raia yeyote wa kigeni. Hivyo nasisitiza kuwa Zanzibar nisehemu salama kwa watalii.
Vilevile, Siku chache kabla ya tukio la Zanzibar, kulikuwa na matukio manne ya watalii kuporwa katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Uporaji huo ulitendwa na watu waliokuwa kwenye magari au pikipiki ambao waliwapora watembea kwa miguu.
Serikali inawahakikishia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya pekee na ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya pekee na ya kupita na hatua zimechukuliwa na Jeshi la Polisi kuongoza usalam kwa wakazi na watalii.
Nachukua fursa hii kuwahakikishia wageni kwamba kila juhudi zimechukuliwa kuhakikisha kuwa usalama wa watalii unadumishwa pamoja na faraja wakati watakapotembelea Tanzania.
Daima tukumbuke kuwa, Tanzania ni kisiwa cha amani na nchi imenuia kudumisha sifa hiyo nzuri.
Karibu Tanzania.
Mhe. Lazaro Nyalandu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
30 Mei, 2012
No comments:
Post a Comment