Marehemu Ditopile Mzuzuri.
Na Mwandishi wetu.
KATIBU Mkuu wa klabu ya Ashanti United ya jijini Dar es salaam Haji Bechina kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo wamepanga kuwaombea duwa marehemu wote waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo itakayofanyika katika shule ya msingi Boma Ilala jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Bechina aliwataja watakaosomewa duwa hiyo kuwa ni pamoja aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyekuwa Mlezi wao Rajabu Mgodo, Athumani Nobi waliokuwa makatibu katika vipindi tofauti na Mzee Mwalimu Kinyogori ambaye alikuwa mwenyekiti.
Bechina alisema kuwa klabu zote za mpira wa miguu zilizopo jijini Dar es salaam pamoja na wadau wa mchezo wa soka wamepewa mialiko kwa kushiliki duwa hiyo itakayofanyika jumapili hii ya julai 17.
Aidha klabu hiyo imepanga kuisuka upya timu ya soka ya Ashanti United baada ya kupoteza mwelekeo miaka ya hivi karibuni Mbali na soka Ashanti pia hujishughulisha na uinuaji wa vipaji vya mchezo wa ngumi kupitia kocha Rajabu Mhamila Super D.
Bechina aliongeza kuwa wanajivunia timu hiyo ya ngumi ambapo mchezaji wake wengi wamendelea kufanya vizuri katika mchezo uho ambapo jumapili ya julai 17 inaingia ulingoni kushindana na Klabu za Amana'Matimbwa'Bigrayt na Midizini