Monday, July 25, 2011

Bright Secondary School: Kwa Mpango Huu hapa Je tutafika kielimu?.. Ni swali kwa wadau wote

 Hili ni moja la Darasa ambalo wanafunzi wanatumia kufundishiwa... Tulipo ingia ndani kulikua ni mawe na vumbi tuu na wanafunzi walikua wakiendelea na shule.. Kwa jinsi palivyo na kama panavyo onekana hapo je kuna uwezekano wa wanafunzi kupona vifua vyao? kwa maana humo ndani kumejaa Vumbi
Hapa ni moja ya kibao Kikionesha madarasa wanayo fundisha
Kibao hiki kinasomeka kama kilivyo hapo sasa Swali ni kwamba kama kuandika kwa  Kimombo tuu hawajui je wanafunzi inakuaje?
Hili ndilo eneo lenyewe la shule .. kwa jinsi palivyo pembeni kuna kiwanda cha Mbao kinapiga kelele masaa yote, pia pembeni kidogo Kuna kiwanda cha kutengenezea chakula cha kuku, na cha ajabu zaidi shule hiyo imezungukwa na Genge na Vibanda vinavyo uzwa pombe za kienyeji.. Sasa swali tena linawaludia wadau hapa kuna kusoma kweli?
Hiki ni kiwanda ambacho kipo Pembeni tuu na shule hiyo na kinatengeneza chakula cha kuku


JE HAWA WAHUSIKA WA SECTA HII YA ELIMU WAKO WAPI MPAKA KUFIKIA KILA MTU AFUNGUE SHULE ANAVYO JITAKIA?



No comments: