Katibu wa CCM mkoa wa kilimanjaro,Steven Kazidi,akimpa pole Bi.Esimend Parimina ambaye amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya KCMC baada ya kujeruhiwa jicho lake la kulia katika ajali ya basi la Lim Safari iliyotokea juzi jioni eneo la kibosho road nje kidogo ya Manispa ya Moshi,watu 11 walipoteza maisha yao na wengine 26 kujeruhiwa vibaya.Picha na Mdau Bashir Nkromo.
CHAMA cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Kilimanjaro,kimetoa pole kwa majeruhi wa ajali ya Basi iliyotokea juzi jioni katika bara bara ya kibosho road nje kidogo yaManispaa ya Moshi.
Katika ajali hiyo iliyohusisha basi la Lim Safari lenye namba za usajili T489BJR na roli la mizigo aina ya Bitisubishi Fuso lenye namba za usajili T884BFJ likiendeshwa na dereva wake Sifael Kaaya,watu 11 walifariki papo hapo wakiwamo madereva wote wa magari hayo mawili. Wote waliofariki ukiondoa madereva hao,ni vibarua waliokuwa wakirejea makwao
huko machame wilaya ya Hai wakitoka kuvuna kahawa katika shamba la kahawa laKilimanjaro Plantretion Ltd ambalo lipo eneo la Kibosho wilaya ya Moshi Vijijini.
Mashuda wa ajli hiyo walisema dereva wa basi hilo,alikuwa amelewa na hakuweza kusikia kilio cha abiria wake waliomtaka apunguze mwendo.
Akitoa pole jana katika Hosiptal ya rufaa ya KCMC baada ya kutembelea majeruhi
wa ajli hiyo,katibu wa CCm mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi,alisema ajali hiyoinatoa funzo kwa mamlaka husika kuwajibika katika kusimamia sheria za usalama barabarani.
Katibu huyo alisema kuwa,aajli nyingi zinatokea kutokana na uzembe wa madereva na kutaka jitihada zifanywe na vyombo husika kutoa adhabu kali kwa madereva wanaosababisha ajali.Alisema Chama cha Mapindizi CCM kimeguswa na ajali hiyo na katika kuonesha kwavitendo,CCM ilitoa msaada wa sh,600,000 na kati ya hizo sh,300,000 zilitolewa na Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Manispaa ya moshi .
Msaada huo aliutoa kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya uuguzi katika Hospital hiyo ya KCMC Redempta Mamseri aliyepokea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospital hiyo,Moshi Ntabae.
Kazidi ambaye alitembelea Idara ya upasuaji katika hospital hiyo na kuzungumza na baadhi ya majeruhi ,alifuatana na katibu wake msaidizi,Habas Mwijuki, Kamanda ya UVCCM Manispaa ya Moshi Agrrey Marealle na Katibu wa CCM Manispaa ya
Moshi,Amos Shimba.
Kwa upande wake kamanda wa UVCCM Manispaa ya Moshi,Agrrey Marealle ,alitioa wito kwa serikali kuona umhimu wa ajali za barabarani kuongezwa katika orodha ya majanga ya kitaifa pamoja na kuweka sheria kali za kudhibiti uzembe kwamadereva.
Aidha Marealle alishauri serikali kuboresha elimu ya madereva kwa kutoa elimu juu ya sheria za usalama barabarani,kudhibiti mianya ya rushwa ikiwamo biashara ya leseni bandia na pia kuwa na utaratibu wa madereva kurudia majaribia ya udereva(driving test) mara kwa mara .
Alishauri pia kuweka mkazo katika kuwadhibiti madereva wanaoendesha vyombo vya moto huku wakiwa wamelewa,kupunguza safari za usiku pamoja na kutoa muda wa kupumzika kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo bila hivyo taifa litaendelea kupoteza nguvu kazi hasa vijana.
'Bila hivyo tutaendelea kupoteza watu hususani vijana ambao ndiyo raslimali kuu ya nchi,kampeni hii inahitaji ushirikiano kati ya polisi na serikali,vyama vya siasa,vyombo vya habari,madhehebu ya dini na jamii kwa ujumla'alisema Marealle. |
No comments:
Post a Comment