Naibu Spika Job Ndugai akiwaamuru wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema kutoka ndani ya Bunge leo mara baada ya wabunge hao kuvunja kanuni ya Bunge ya kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha akisoma bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma leo kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Godbless Lema ambaye ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kuhusu wizara ya mambo ya ndani ya Nchi akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Askari Polisi wa Bunge wakiwasindikiza wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu (kulia) Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Godbless Lema (wa pili kushoto) ili waondoke nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai (hayupo pichani) kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika. Wa pili kulia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwasindikiza wabunge wenzake.
Askari Polisi wa Bunge wakiwasindikiza wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu (kulia) Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Godbless Lema (katikati) ili waondoke nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai (hayupo pichani) kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika.
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Godbless Lema akiingia ndani ya gari huku Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) akisubiri kuingia mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni ya Bunge ya kuongea bila ruhusa kupata ruhusa ya Naibu Spika.
Askari Polisi wa Bunge wakihakikisha kuwa gari lililowabeba wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema linaondoka nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
1 comment:
ni masikitiko namna demokrasia inavyoendelea kubakwa hapa tanzania, huu ni udhalilishaji wa hali ya juu,
wabunge wa ccm wanaruhusiwa kuzomea, kupiga kelele kwa mambo ya kipuuzi lakini wabunge wa chadema wanazibwa midomo wasiongee, tuliona zitto kabwe,akiitwa mwongo mwaka 2007 lakini wabunge haohao wa ccm aibu ziliwajaa baadae
haya jana wenje alitaka kuzungumza juu ya samaki wa sumu, mwenyekiti akakurupuka kumfukuza, leo tena!!!??
ni aibu, hawa wabunge wa ccm na viongozi wa bunge wanaligeuza bunge letu liwe sehemu ya vituko, sasa naamini kwa nini lema aliwahi kusema milango ifungwe watu wazichape
Post a Comment