Mkazi wa Pongwe Tanga, Zainabu Hamza (kulia) akipewa ushauri nasaha kuhusu ugonjwa wa ukimwi mara baada ya kupima damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS
iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayetoa ushauri ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Elizabeth Lawuo. Anayeangalia ni mtoto wa Selina, Amina Adamu.
iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayetoa ushauri ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Elizabeth Lawuo. Anayeangalia ni mtoto wa Selina, Amina Adamu.
Mkazi wa Pongwe Tanga, Hadija Rashidi (kulia) akipima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga.
Mkazi wa Pongwe Tanga, Selina Anthony (kulia) akipima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga na mtoto aliyebebwa ba Selina ni mjukuu wake, Gerald Rashidi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Saruji Tanga, David Lee (kulia) akitolewa damu kupima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wakazi wa mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga.
NA MWANDISHI WETU
Pongwe Tanga.
KAMPUNI ya Saruji Tangaimezindua kampueni ya siku nne kuhusu masuala ya ufahamu juu ya ugonjwa waHIV/AIDS na upimaji wa virusi vya ugonjwa huo katika kata ya Pongwe mkoaniTanga jana ikiwa ni sehemu ya sera za kampuni hiyo katika kuisaidia jamii (CSI).
Akizungumza wakati wauzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement, David Lee alisema TangaCement imeona kuna umuhimu mkubwa wa kufanya kampeni hiyo kwani maendeleo yaTaifa lolote yanatokana na kuwa na watu wenye afya bora.
“Tanga Cement inajengaTanzania, hivyo tunaamini kuwa huwezi kujenga Taifa kama wananchi wengiwatakuwa hawana afya hususani vijana ambao ndio nguvu kazi kubwa katika uchumiwan chi hii”, akasema.
Mkurugenzi huyo alisemakampeni kama hiyo ilianzia kwanza kwa wafanyakazi wao pamoja na familia zaokatika mkakati huo huo kwamba ugonjwa wa ukimwi unazorotesha afya hivyo kampunihaitaweza kutimiza malengo yake endapo idadi kubwa ya wafanyakazi watakuwa niwaathirika.
“kama ilivyo kauli mbiuyetu katika kampeni hii kuwa ’Okoa Maisha Pima Afya yako’ hivyo tunaaminiukijua hali yako ukiwa umeathirika au hujaathirika itakusaidia kujiokoa wewe,familia yako na wale wanaokuzunguuka”, akaongeza.
Akizungumziautekelezaji wa zoezi hilo, Ofisa Mawasiliano wa TCCL, Bi. Mtanga Noor alisemawanatarajia kuhudumia zaidi ya wakazi 600 katika eneo hilo la Pongwe na kijijicha Kichangani vyote vikilizunguuka eneo ya kiwanda na makazi ya wafanyakazi wakampuni hiyo.
“Hawa majirani zetuhivyo afya zao ni muhimu pia na ndio sababu moja ya vipengele tunavyoangaliakatika mpango wetu wa kuisaidia jamii (CSI) ni afya, na ukimwi unaingia katikakipengele hiki”, akasema.
Bi. Mtanga akasemakatika kampeni hiyo ya siku nne wananchi hao watapata ushauri nasihi kuhusuugonjwa huo, kuchunguzwa afya zao ambapo zaidi ya shs milioni 17 zitatumikakufanikisha zoezi hilo.
Awali akizungumzia haliya ugonjwa huo Mratibu Ukimwa mkoani humo, Moses Kisibo aliishukuru Tanga Cementkwa kufanikisha zoezi hilo litakalosaidia kupunguza kasi ya maambukizi katika Mkoa wa Tanga akisema kuwakwa sasa ipo zaidi ya aslimia 8.7
Mratibu huyo alitajamoja ya sababu inayochangia kuongezeka kwa kasi ua ugonjwa huo kuwa ni uelewamdogo kuhusu HIV/AIDS kwa wakazi wa mkoa huo ambapo zaidi ya asilimia 75 yawatu wanaojijihusisha na masuala ya ngono wanafanya ngono za gizani.
“Kondomu hazitumikiwatu wanafanya ngono ‘gizani’ na hata hao wanaozitumia hawazitumiii jinsiinavyotakiwa kwa kufuata hatua zinazoshauriwa na wataalamu hii inachangia kasiya ugonjwa huu kuwa kubwa”, akaongeza.
Mmoja wa wakaziwaliojitokeza kupima virusi vya ukimwi yeye na mtoto wake, Zainabu Hamza namwanaye, Amina Adamu alisema anafuraha sana baada ya kujitambua afya yake kwanihiyo ilikuwa mara yake ya tatu hivyo hiyo itamsaidia kuweza kuishi akichukujatahadhari zote ili asipate maambukizi.