Monday, July 18, 2011

KOMBAINI YA BENKI YAIBUKA KIDEDEA KATIKA BONANZA LILILOANDALIWA NA BENK YA POSTA TANZANIA KWA KUIFUNGA TIMU YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR .

MAKAMU wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba K Moshingi wakitoka kukagua timu wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba. K .Moshingi, alipowasili katika viwanja vya Mao Dzedung katika Tamasha la Bonaza la Mabenki Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Posta Tanzania.katikati Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Bihindi Hamad.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya Sira Mwamboya., akitabasamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba K.Moshingi.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba K Moshingi wakiwasalimia wachezaji wa timu ya Wawakilishi wakatik wa mapumziko wa mpambano huo ulioamuliwa kwa mikuju ya peneti.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi Kikombe cha Ubingwa wa kufuta kamba Nahodha wa timu ya Wawakilishi Hamza Hassan baada ya kuwashinda watunza mapesa wa mabenki.
Mjumbe wa Barazaa la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma akimkabidhi kikombe cha ubingwa wa Bonaza la Mabenki Nahodha wa timu ya Kombaini ya Benki Abdull Mshangama wa benki ya KCB.baada ya kuifunga timu ya Wawakilishi kwa peneti 5 - 6.mchezo uliofanyika uwanja wa Mao Dzedung.

MABINGWA wa Bonaza la Mabenki ya Zanzibar wakishangilia ubingwa wao baada ya kuifunga timu ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, katika bonaza lililoandaliwa na Benki ya Posta Tanzania kwa Wafanyakazi wa Benki zilioko Zanzibar.
Picha na Mdau Othman Maulid