Kwa hili la Wizara ya nishati na Madini: Kamati zote za Kudumu za Bunge Zichunguzwe!
Kutokupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ni ushahidi kuwa kamati husika ya bunge kwa kujua au kutokujua hawakufanya kazi yao inavyopaswa kuhusu hiyo bajeti. Uchunguzi wa kina inabidi ufanyike kuangalia kama kweli kamati husika imepokea rushwa kutoka serikalini ili kukubaliana na bajeti hiyo.

Vyombo vya habari vimeripoti kuhusu Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda kuweka kando bajeti ya Nishati na Madini kwa wiki tatu baada ya mjadala mkali juu ya tatizo la umeme kutokea bungeni. Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, ameandika barua kwa mashirika na taasisi chini ya wizara yake ya kuwataka kuchangia Tsh milioni 50 kila mwaka ili kuwezesha kuwasilishwa laini ya bajeti ya Wizara yake
Hii inaonekana kama kitu cha kujirudia kama sehemu ya barua ilivyosema “...kama ilivyo kawaida wakati wa kuwasilisha hotuba ya bajeti bungeni Dodoma...”. ingawa sasa mambo yamebadilika na kuwa kama mtafaruko.
Wiki kadhaa zilizopita iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Kamati ya Kudumu ya bunge ya Wizara ya Nishati na Madini inawezekana ikawa imepewa rushwa ili kukubaliana na bajeti Dar es salaam. Hisia miongoni mwa wananchi ni kuwa kilichotokea kwenye Wizara ya Nishati na Madini inawezekana huwa kinatokea pia kwenye wizara nyingine.
Inavyoonekana, mwendo huu pia ulionekana kwa wizara nyinginekwa mfano kuandaliwa kwa semina kwa wabunge wa kamati kwa baadhi ya taasisi za umma kabla ya mjadala wa bajeti za wizara husika kufanyika. Semina hizi inawezekana zinafanyika ili kuwalipa wabunge wasiweze kuuliza juu ya matatizo yaliyopo kwenye bajeti zao.
Tanzania inakabiliwa na matatizo ya kudumu vikiwemo usimamizi duni wa serikali na Bunge. Baadhi ya matatizo hayo ni pamoja na mikataba ya kibiashara isiyo na faida, kashfa za rushwa kubwa, bajeti ya umma iliyojaa matumizi yasiyo ya lazima, usimamizi mbovu pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kwa kuwa bunge na serikali, wote wanahusishwa katika kashfa hii ya rushwa, chombo huru inabidi kipewe kazi ya kuunda kamati huru kuchunguza madai hayo ya serikali ya kuhonga bungeni. Hatua za marekebisho lazima zichukuliwe dhidi ya wale watakao gundulika kuhusika na sakata hili .
Imetolewa na
Mr Irenei Kiria
Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika P. O. Box 12183 Dar es Salaam,
Simu: +255 222 666355/57, Fax: 2668015, Email: info@sikika.or.tz, Tovuti: www.sikika.or.tz
Mr Irenei Kiria
Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika P. O. Box 12183 Dar es Salaam,
Simu: +255 222 666355/57, Fax: 2668015, Email: info@sikika.or.tz, Tovuti: www.sikika.or.tz
No comments:
Post a Comment