Tuesday, July 12, 2011

Lowasa Akutana Na Mufti Simba; Ammwagia Mamilioni

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akimkabidhi fuba la sh. milioni 13, Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa Shaaban bin Simba, kwa ajili ya kusaidia shule ya sekondari la Edward Lowassa iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Mufti ambaye ni mlezi wa shule hiyo, Shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi mwakani kwa kuanzia na wanafunzi 200 wa kidato cha kwanza, na kwamba fedha hizo zitatumika kukamilisha baadhi ya mambo ya shule hiyo ikiwemo kujenga bweni la watoto 30, choo cha shule, kisima cha maji na shule itajihusisha zaidi kusomesha yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Kulia ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo.

Wakiagana baada ya shughuli hiyo.Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog