Tuesday, July 12, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA KIGODA CHA KUMBUKUMBU YA MWL NYERERE JANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kumbukumbu ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere kinachohusika na masuala ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi, kilichozinduliwa leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutangazwa kwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda hicho, Prof. Pius Yanda.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rwekaza Mukanda (kulia) akimvisha kofia na Joho, Prof. Pius Yanda, baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu yerere, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kigoda hicho kilichozinduliwa kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Makenya Maboko.
Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Pius Yanda, akiwa ameketi kwenye Kigoda hicho baada ya kutangazwa rasmi wakati wa uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, kilichozinduliwa leo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Prof. Pius Yanda, baada ya kutangazwa na kuvishwa Joho la kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa na Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua maonyesho ya vitabu vya kumbukumbu nje ya ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kuzinduz Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo mchana.
Mkurugenzi na Kiongozi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto, akiigiza kusafiri na Ngamia wake, wakati akitoa burudani ya kuimba mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere kilichozinduliwa leo Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam baada ya uzinduzi huo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: