Thursday, July 28, 2011

NAIBU WAZIRI WA CHINA ATEMBELEA DODOMA LEO

 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni Anjela Ngovi akimvalisha kanga naibu waziri wa Utamaduni wa China Zhao Shaohua wakati naibu waziri huyo alipotembelea mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuonana na viongozi wa Serikali  huku waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Prof. Helmasi Mwansoko (kulia) wakishuhudia . Zhao pamoja na ujumbe wake  wako  nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
 Naibu waziri wa Utamaduni wa China Zhao Shaohua akiangalia ngoma ya kabila la kisukuma iliyokuwa inachezwa na kikundi cha ngoma cha Mwinamila cha mjini Dodoma wakati naibu waziri huyo alipowasili mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuonana na viongozi wa Serikali . Zhao pamoja na ujumbe wake  wako  nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
Naibu waziri wa Utamaduni wa China Zhao Shaohua akiangalia zawadi ya picha ya pundamilia aliyopewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinga wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodima. Zhao pamoja na ujumbe wake  wako  nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo Emmanuel Nchimbi (kulia) akisalimiana na Naibu waziri wa Utamaduni wa China Zhao Shaohua (katikati) katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma Zhao pamoja na ujumbe wake  wako  nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China. Kulia ni Zhao Haisheng aliyeapambana na ujumbe huo.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinga akiangalia  zawadi ya chombo cha kuwekea sukari aliyopewa na  Naibu waziri wa Utamaduni wa China Zhao Shaohua wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodima. Zhao pamoja na ujumbe wake  wako  nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo

No comments: