Tuesday, July 26, 2011

MKUTANO WA 57 WA CPA WAWAJADILI WAGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI CPA DUNIA

Mjumbe katika ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania katika Mkutano wa 57 wa Chama cha wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) unaofanyika London Uingereza, Mhe. Zito Kabwe akichangia hoja kuhusu msimamo wa Africa kwenye maandalizi ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama hicho. Wabunge wa Afrika katika Kikao chao hicho hawakufikia msimamo wa pamoja kuhusu Mgombea watakayempendekeza mpaka watakapo kutana tena kesho. Jumla ya wagombea watatu kutoka, Uingereza, Pakistani, na visiwa vya Samoa, wanawania kiti hicho.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 57 wa Chama cha wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) unaofanyika London Uingereza, wakifuatilia kwa makini hoja kutoka kwa wajumbe wanaowania uwenyekiti wa Dunia wa chama hicho. Kutoka Kushoto Ni Ndg. Emmanuel Mpanda, anayemwakilisha katibu wa Bunge, Naibu Spika Mhe. Job Ndugai, Mhe. Zungu, Mhe. Beatrice Shelukindo, Mhe. Zitto Kabwe na Mhe. Maua Daftari. Jumla ya wagombea watatu kutoka, Uingereza, Pakistani, na visiwa vya Samoa, wanawania kiti hicho. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
Mjumbe katika ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania katika Mkutano wa 57 wa Chama cha wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) unaofanyika London Uingereza, Mhe. Zito Kabwe akiteta jambo na Mbunge Mwenzie kutoka Kenya mara baada ya kikao cha kanda ya Afrika kumalizika. Kulia ni Spika wa Kenya Mhe. Keneth Marende (Mb). Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Picha Zote na Owen Mwandumbya -Bunge


No comments: