Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Jarvis Simbeye, vazi la kufanyia usafi kwa vikundi vya usafi cha Mtaa wa Ngoto uliopo katika Kata ya SabaSaba baada ya kushinda tuzo ya Kimkoa kwa masuala ya usafi na uwekaji wa kumbukumbu na takwimu.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa,( wapili kutoka kushoto) akifungua karatasi ili kuona aina ya zawadi waliozawadiwa ya Lap top aina ya Toshiba kwa Wilaya hiyo baada ya kushinda ushindi wa jumla katika umpangilio wa kitakiwmu za afya na kumbukumbu mbalimbali za afya na usafi ,( wakwanza kushoto) ni Kaimu RAS Mkoa wa Morogoro, Esther Lauwo na ( wakwanza kutoka kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Francis Miti.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Frida Mokiti ( aliyesimama ) akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, (watatu walioketi kutoka kushoto) na ( wakwanza kushoto ) ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu ,akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Evaarist Ndikilo, pamoja na wadau wengine wa afya wa Mkoa huo wakati wa kikao cha pamoja cha nusu mwaka kati ya sekretarieti ya Mkoa , timu ya uendeshaji wa huduma za afya kwenye Halmashauri juu ya kutathimini utoaji wa huduma za Afya Mkoani Morogoro.
Wadau wa afya wa Wilaya ya Mvomero wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Frida Mokiti ( hayupo pichani) wakati wa kikao cha pamoja cha nusu mwaka kati ya sekretarieti ya Mkoa , timu ya uendeshaji wa huduma za afya kwenye Halmashauri juu ya kutathimini utoaji wa huduma za Afya Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, (wanne walioketi kutoka kushoto) akiwa pamoja na wadau wa afya wa Mkoa huo mara baada ya kufungua kikao cha pamoja cha nusu mwaka kati ya sekretarieti ya Mkoa , timu ya uendeshaji wa huduma za afya kwenye Halmashauri juu ya kutathimini utoaji wa huduma za Afya Mkoani Morogoro.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii-Morogoro.
Habari kwa Hisani Ya Michuzi Blog
Habari kwa Hisani Ya Michuzi Blog