Gari hii aina ya Nissan Blueburd yenye nambari za usajili T 788 APB imegongana na lori la kubeba mchanga aina ya Isuzu lenye nambari za usajili T 930 BNT maeneo ya Victoria,barabara ya Bagamoyo rodi jijini Dar usiku huu.kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,wanasema kwamba waliiona gari hii ndogo ikitokea upande wa mwenge na kueleke upande wa morocco huku ikiwa katika njia ya katikati iliopo katika barabara hiyo huku upande wa morocco kuelekea upande wa mwenge kulikuwa na hilo lori ambalo lilikuwa likielekea upande huo na baada ya kuiona gari hiyo ndogo ikizidi kuelekea wake ndipo dereva wa lori hilo akipojitahidi kuikwepa gari hiyo ndogo bila mafanikio na mpaka kupelekea kutokea kwa ajali hiyo.Dereva wa gari hii ndogo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja,alikimbizwa hospitali kwa matibabu kwani alikuwa kavunjika mkono wa kulia pamoja na mguu.
Baada ya muda kidogo ilikuja BreakDown na kuibeba gari hiyo ndogo ambayo imeumia vibaya sana.
Muonekano wa nyuma wa gari hiyo.
Hii ndio lori iliyogongana na gari hilo dogo usiku huu.
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog



