Na Pardon Mbwate, wa Jeshila Polisi Kigoma
Makachero wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma wamefanikiwa kuwatia nguvuni majambazi wanne sugu wawili kati yao wakitokea nchini Burundi wakiwa na silaha moja ya kivita aina ya SMG pamoja na risasi 85.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa majambazi hayo yalikamatwa jana kwa nyakati tofauti mkoani humo yakijipanga kuteka magari na kupora mali za abiria.
Kamanda Kashai amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Leonard Ntaoyima(47), na Omari Ngoloye(30), wote wafanyabiashara wa Kijiji cha Katumbi katika Tarafa ya Buhimbi wakiwa na silaha moja aina ya SMG yenye nambari 3315435 pamoja na risasi tatu katika magazine wote walikamatiwa katika kijiji hicho katika Wilaya ya Kigoma mjini.
Watuhumiwa wengine ambao ni Raia wa Burundi ni Sylivanus Zehimana(27) na mwenzake Ndiwayo Safari(19), wote kutoka katika Kijiji cha Kinyinya nchini humno wakiwa na risasi 82 za SMG ambao walikamatiwa katika Kijiji cha Nyankwi kilichopokatika Tarafa ya Kifura Wilayani Kibondo.
Amesema kuwa kukamatwa kwa majambazi hayo kunatokana na taarifa za siri za Raia wema walizozitoa Polisi za kuwepo kwa watu hao kabla ya kuwekewa mtego na Polisi na kutiwa mbaroni kabla ya kufanya uporaji.
Kamanda Kashai amesema kuwa silaha hiyo ambayo ilikuwa imetumbukizwa kwenye mfuko wa rambo ilikuwa ikitumika katika utekaji wa mabasi na uporaji wa mali za abiria katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Kamanda huyo amewashukuru wale wote waliosaidia kufanikiwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao na amezidi kutoa wito kwa wannchi kuendelea kutoa taariufa Polisi wanapobaini nyendo za watu wabaya ili wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.
Amesema kuwa mara nyingi watu kama hao wakiwemo wa kutoka nchi jirani wamekuwa wakishirikiana na Watanzania wachache kwa kufanya vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha ukiwemo wa utekaji wa magari na kupora mali za abiria.
1 comment:
Post a Comment