Juu na Chini: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Ulinzi la Afrika ya Kusini wakati wa mwanzo wa Ziara yake Rasmi ya kitaifa nchini Afrika ya Kusini jana.
Mawaziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na Tanzania Bernard Membe na Bi. Maite Nkoana Mashabane wakibalishana mikataba ya kuanzishwa kwa Tume ya Ushirikiano(Bi-National Commission) kati ya nchi hizo mbili muda mfupi baada ya kusaini katika ikulu ya Afrika ya Kusini jijini Pretoria jana huku marais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Jackob Zuma wakishuhudia.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati yeye na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma walipokuwa wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Afrika ya Kusini jijini Pretoria jana.Rais Dr.Jakaya Kikwete yupo nchini Afrika ya Kusini kwa ziara Rasmi ya Kitaifa ya siku mbili.
Picha na Freddy Maro.
No comments:
Post a Comment