Wednesday, July 20, 2011

Sakta ya wizara ya nishati na madini: pinda apata maelekezo, takukuru watia timu, hakuna aliyejiuzulu






WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ana siri nzito kuhusu hatima ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo baada ya jana kusema kuwa Rais Jakaya Kikwete amempa maelekezo mapya kuhusu suala hilo.Pinda alisema hayo, baada ya gazeti la Mwananchi kumtaka aeleze hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi ya katibu mkuu huyo aliyetuhumiwa juzi bungeni kuwa aliziagiza zaidi ya taasisi 20 kuchanga Sh50milioni kila moja kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.


Dkt. Hosea
'Suala hilo bado tunalifanyia kazi,' alisema Pinda alipotakiwa kueleza maagizo aliyopewa na Rais baada ya kuwasiliana naye juzi na jana. 'Ndio niliwasiliana naye lakini, ametoa maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo tunalazimika kuyafanyia kazi kwanza.'

Akizungumzia suala hilo la Jairo bungeni juzi, Pinda alisema: "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.






Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua.'Tuhuma za rushwa katika Wizara ya Nishati na Madini ziliibuliwa juzi na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo alipokuwa akichangia Makadirio ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni juzi.

Shellukindo alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma.'Tena inaagiza kwamba fedha hizo zikishatumwa kwenye akaunti hiyo, wizara ipewe taarifa kupitia Ofisi ya DP kwa ajili ya utaratibu,' alisema Shellukindo akiinukuu barua hiyo.

Habari kamili nenda Mwananchi
BOFYA HAPA

No comments: