Wednesday, July 20, 2011

SERIKALI KULIPA MADENI YA WALIMU



NA MAGRETH KINABO – MAELEZO,DODOMA

SERIKALI imepeleka kiasi cha fedha cha sh. bilioni 15.5 katika halimashauri zote nchini kwa ajili ya likizo na uhamisho kwa walimu wa shule za msingi na sekondari katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2010/2011.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,TAMISEMI) Kassim Majaliwa wakati akijibu swali na mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohamed Dewji(CCM) .

Ambalo lililoulizwa na mbunge wa Viti Maalum(CCM) Singida , Diana Chilolo kwa niaba yake ambaye alitaka kufahamu kuwa serikali ina mapango gani wa kumaliza malalamiko yanayohusu stahili za walimu wa shule za Singida na kungineko nchini.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema kati ya fedha hizo sh.milioni 475.3 zilipelekwa katika mkoa wa huo, ambapo sh.milioni 388.8 ni kwa ajili ya likizo na sh.milioni 68.5 kwa ajili ya uhamisho.

Aliongeza kuwa serikali kwa wakati tofauti imekuwa ikichukua hatua mahsusi ili kuhakikisha kwamba inamaliza malalamiko hayo ya stahili mbalimbali, ambapo mwaka 2009 ili hakiki na kulipa madeni ya walimu , jumla yash. bilioni 32.2 zilitolewa kulipa stahili za walimu wa shule za msingi na sh. bilioni 12.5 kwa stahili mbalimbali za walimu wa shule za sekondari nchini.

Waziri Majaliwa alisema kuanzia mwaka 2009/2010 ,serikali imeweka utaratibu ambao walimu wanapangwa wanalipwa mishahara na stahili zao mara wanaporipoti katika mamlaka ya Serikali za Mitaa. Hivyo ili kufanikisha azma hiyo Februari mwaka huu ilipeleka katika halimashauri zote nchini jumla ya sh. bilioni 15.3 kwa ajili ya malipo ya posho ya kujikimu, nauli, mizigo na wategemezi kwa walimu wapya.

Aidha alisema serikali imetoa maelekezo kwa wakurugenzi wa halimashauri zote nchini kutozalisha madeni na kuzingatia maelekezo ya serikali kwa kulipa stahili za likizo, uhamisho na matibabu.

Alisema madeni ya walimu wa mkoa huo na nchini kote stahili zao zinashughulikiwa na zitalipwa baada ya taratibu kukamilika.mwisho.


SERIKALI imelipa madeni ya vyama vya ushirika 38, ambapo kiasi cha sh. bilioni 15.01 hadi kufikia Desemba mwaka 2010.

Hayo yalisemwa (leo)jana Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini(CCM) lililouliza kuwa katika kufufua vyam vya ushirika serikali iliamua kulipa madeni yote ya vyama vya ushirika nchini ikiwemo SHIRECU.

Je ni lini serikali itakamilisha ulipaji wa mapunjo ya mishahara kwa mamia ya wafanyakazi wa SHIRECU mkoani Shinyanga waliopunguzwa kazi au kustaafu kisheria.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema miongoni mwa madeni yaliyopo ni deni la watumishi wa SHIRECU waliopunguzwa kazi au kustaafishwa la sh. bilioni 3.27 ambapo kati hizo serikali imeshalipa sh. milioni 654.2 sawa na asilimia 20.

Hivyo serikali itaendelea kutenga bajeti zake za kila mwaka hadi deni litakapokwisha.

Waziri Chiza alisema seriklai inalipa madeni hayo ili kuvifufua kwa sababu ndiyo njia rahisi ya kuwafikishia wananchi wengi misaada na huduma kuliko kumhudumia mtu mmojamoja.

Pia vyama hivyo havitaruhusiwa kuilimbikiza madeni tena na wizara yake itafanya ukaguzi, mara kwa mara ili kudhibiti wizi, ubadhilifu wa fedha na mali unaofanywa hususan wakati wa msimu wa ununuzi wa mazao.

No comments: