Sunday, July 17, 2011

Wizara ya maliasili na utalii yazindua maonyesho ya siku 4 maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru

Mgeni rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Ezekiel Maige akizindua rasmi maonyesho ya siku nne kwa Wizara ya Maliasili na Utalii maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara. hapa tumewaonyesha wananchii kuanzia mawaziri waliopata kuwepo katika wizara hiyo kwa miaka nyuma na kuonyesha mafanikio ya wizara kwa kipindi hicho. Picha hizo zilichukuliwa katika viwanja viwanja vya mnazi mmoja ambako uzinduzi rasmi ulifanyika.
Maadhimisho hao yalitanguliwa na maandamano ya watumishi wa wizara hio hadi ktk viwanja vya mnazi mmoja kama walivyoonekana pichani.Katika picha hizo wako mawaziri wa zamani Sir George Kahama, Mhe. Zakia Meghji, Juma Ngasongwa, Arcado Ntagazwa na Waziri wa sasa wa Maliasili na Utalii Mhe Ezekiel maige pamoja na viongozi mbalimbli ambao walishiriki katika uzinduzi wa maonyesho hayo ambayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja na Sabasaba
Pichani Mawaziri wa zamani Sir George Kahama, Mhe. Zakia Meghji, Juma Ngasongwa, Arcado Ntagazwa na Waziri wa sasa wa Maliasili na Utalii Mhe Ezekiel Maige pamoja na viongozi mbalimbli ambao walishiriki katika uzinduzi wa maonyesho hayo ambayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja na Sabasaba.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Ezekiel Maige akicheza bao na Mh Sir George Kahama.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Ezekiel Maige akipata maelezo mbalimbali kuhusiaa na maonyesho hayo.
Maandamano ya maonyeshoo hayo yakiendelea kuelekea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.jijini Dar Es Salaam.
Habari kwa hisani ya Jiachie Blog