Wednesday, August 3, 2011

Airtel yasaidia mashindano ya ngumi taifa

Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi T-shirt 100 kwa niaba ya Airtel kusaidia shirikisho la Ngumi Tanzania, anaekabidhiwa ni Katibu wa chama cha Waamuzi wa mchezo wa ngumi Taifa Juma Suleiman (katikati). T-shirt hizo zitatumika katika mashindano ya klabu bingwa ya Ngumi za Ridhaa yanayoendelea sasa mkoani Mwanza kwa kushirikisha vilabu toka mikoa yote na yatafikia kilele siku ya nanenane.wa kwanza kulia pichani ni Makoyo Sangula Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ngumi.

============= =========== ==========
Kampuni ya simu za mkononi ya airtel imedhamini mashindano ya club bingwa ya taifa ya michezo ya ngumi za rithaa yanayoendelea mkoani mwanza katika viwanja vya kirumba ambapo yatafikia kilele siku ya nane nane 8/8/2011 .

Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Katibu wa chama chama cha waamuzi wa michezo ya ngumi taifa, Juma Suleiman alisema.' Tunaishukuru kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kutupatia vifaa hivi vya mazoezi ambazo ni T-shirt zitakazotumika na wachezaji wa vilabu shirika toka mikoa yote wakati wa mashindano.

Hii inaonyesha kuwa mnadhamira ya dhati ya kusaidia na kuinua kiwango cha mchezo wa ngumi nchini Mashindano haya ya club bingwa ya taifa yanahusisha timu za mkoa na vilabu mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kujiaandaa na mashindano ya kimataifa ya All African Game yatakayofanyika msumbiji, hivyo basi tunapenda kuwakaribisha wakazi wote wa jiji la Mwanza kuona mashindano haya ni kivutio kikubwa aliongeza Bw Suleiman

Akikabidhi msaada huo Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema Airtel imejipanga katika kuchangia sekta ya michezo nchini, Airtel tunaendelea na mkakati wetu wa kukuza michezo aina yote nchini Tanzania na ndio maana leo hii tunaanza ushirika huu na wana masumbwi Tayari tumejikita katiaka mashindano mpira wa miguu ya U-17 ya Airtel rising star ambayo kwa sasa yamefikia ngazi ya nusu fainali, ni matumani yetu kuwa ushirikiano mzuri kati yetu na wadau wa michezo kama hawa watatuletea michanganuo endelevu ili tuendelee kuwa na wanamichezo bora watakaoitangaza nchi yetu vyema katika mashindano mbali mbali.

No comments: